Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Wakili wa Serikali: Hebu Kiangalie hiki kitu hapa, Iambie Mahakama ni nini

Shahidi: anaingilia bila Kushika, ni Bastola

Wakili wa Serikali: ambayo Imetoka wapi

Shahidi: Imetoka Kwa Adam

Wakili wa Serikali: Uliona wapi?

Shahidi: iliyotoka kwa Adam

Wakili wa Serikali: ni Kitu gani Kilichokufanya ukagundua

Shahidi: kwa namba

Wakili wa Serikali: Namba gani

Shahidi: A5340


Hapa tumepigwa na kitu kizito,mfanyabiashara wa kawaida kabsa kutoka kitaa anawezaje kukalili namba za bastora toka siku ya tukio mpk leo mahakaman[emoji848]
Hadi line za simu. Hata angeulizwa namba za hizo line angezitaja. Aibu tupu ukizingatia mwenyewe eti ni muuza mbege.
 
Kwani dhalimu wenu bado yupo?

Si mlikuwa mnashangilia juzi juzi tu hapa kwamba kaondoka?
Haya yote yaliyotokea kipindi chake
Na tutaendelea kushangilia kwa wema wake mungu kuliondosha lile dubwasha JPM kwa uso wa hii dunia.
Kama inakukera kalifufue uzikwe wewe.
Juha wewe
 
Huyo shahidi Rau muuza pombe anajua na kukumbuka mpaka number ya bastola na kila kitu kilichoandikwa kwenye form na mpaka line za simu 🤣 , alionyeshwa hizo details kama nani na kwa sababu gani na kwa sheria ipi? wangapi walionyeshwa hizo details na kwanini alichaguliwa yeye kuonyeshwa? kuna maswali mengi sana ya kumuuliza huyu muuza pombe,Kibatala akipigilia misumari ya kutosha huyo mama atakuwa exposed kirahisi sana, hizi kesi za kupika dawa ni kumtoa shahidi kwenye line zake alizokariri na nina uhakika watapigilia hapo hapo
 
Kingai alisema yeye ndiye aliyekuwa kiongozi kwenye ukamataji nk...Shahidi huyu anatofautiana naye!

Mallya: Kwenye Maelezo Yako umeeleza Mahali Kiongozi wao, Afande nani

Shahidi: Afande Jumanne

Mallya: akitokea Mtu akisema yeye ndiyo Kiongozi aliyekwepo atakuwa Muongo

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unamfahamu Kingai

Shahidi: Hapana


Imeisha hiyo.... Mashahidi hawajawahi kuonana.. jaj kazi anayo.
 
  • Shahidi kajitanda baibui kavaa na barakoa kubwa kumziba sura
  • Shahidi Kajitambulisha jina ... ... Mtali, wakili wa serekali kwakua ana majina kwenye fomu akauliza tena "ni Mtali?" Shahidi akabadili jina like la mwisho, akasema ... ... Mtalo
  • Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 45
  • Mkristo RC
  • Anauza pombe, mbege!

Kwanini ajizibe sura? Anayeweza kumtambua ni watu wa rau madukani wanaomfahamu kama hawapo mahakamani basi ni washatakiwa Adamoo na Moh'd Lingwenya. Nani amethibitisha aliyepanda kizimbani ndiye shahidi ... ... Mtalo mwenyewe haswa?

Mtu (mwenye umri wa miaka 45) anawezaje kukosea kutamka silabi ama irabu ya jina lake na kupoteza tamko zima la jina? Yani Mallya aseme yeye ni Mallyo ama Siyani aseme yeye ni Siyana?

Vazi la baibui si ni vazi la stara kwa wanawake wa dini ya kiislamu? Vp Sasa kuvaliwa na mkristo anayekiri mahakani kuwa anauza pombe?( bia na mbege). Hii ina tofauti gani na mtu anayevaa barakashee na anauza kitimoto?

Ni hayo tu ndugu zangu
 
Hivi si amekula kiapo Cha kusema kweli... Hawezi kushtakiwa huko siku za mbele?..
Huyu ushahidi wake utabatilishwa. Serikali dhalim ndiyo kazi yake kubambikia watu kesi za kutunga na kuchonga mashahidi wa uongo. Shame!!!!!
 
Back
Top Bottom