Jaji ameingia Mahakamani.
Kesi Na. 16 ya mwaka 2021 inatajwa
Kesi namba 16 ya 2021, jamhuri dhidi ya Khalfan Bwire, Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Jaji anamuita Wakili wa Serikali...
Wakili wa Serikali anatambulisha Jopo lake
- Robert Kidando
- Nassoro Katuga
- Ignas Mwanuka
- Esther Martin
- Tulumanywa Majigo
Pia anawatambulisha mawakili na mawakili wengine watatu.
Mawakili upande wa Utetezi wanatambulishwa
- Peter Kibatala
- Jeremiah Mtobesya
- Fred Kihwelo
- John Malya
- Gaston Garubindi
- Seleman Mtauka
- Michael Mwangasa
- Evaresta Kisanga
- Khadija Aron
- Maria Mushi
- Deogratius Mahinyila
- Nashon Nkungu
- Jebra Kambole
Anasema anamtambulisha Wakili Fredrick Kihwelo kwa sababu maalum
Mawakili wa mshtakiwa wa kwanza ni Jeremiah Mtobesya na Nashon Nkungu.
Mshtakiwa wa tatu atawakilishwa na Dickson Matata na Fredrick Kihwelo
Mshtakiwa wa pili atawakilishwa na John Mallya
Mawakili wengine wote watamwakilisha mshtakiwa wa nne
Jaji anauliza kama mawakili wa serikali wanalolote Juu ya ingizo Jipya la wakili Fredrick Kihwelo kama kuna mgongano wa maslahi.
Wakili wa Serikali anasema hakuna tatizo kwa sababu tangu kesi ianze hajaonekana kwenye Column yoyote.
Jaji: hiyo wakili Fredrick Kihwelo anamshikia mikoba wakili Dickson Matata au atakuwa moja kwa moja kwa mshtakiwa watatu?
Kibatala: kuanzia leo mshtakiwa watatu atawakilishwa na wakili Fredrick Kihwelo na kusaidiana na Dickson Matata ambaye leo hayupo mahakamani
Wakili wa Serikali anahoji mshtakiwa mwenyewe anasemaje baada ya kumsikiliza Kibatala
Jaji: hilo tayari nimeshaliongelea kuwa baada ya utambulisho wa Kibatala nitamuhoji Mshtakiwa
Jaji: Ling'wenya bila shaka umesikia?
Ling'wenya: Nimesikia Mh. nakubaliana na Wakili Kibatala
Jaji: Kuna taarifa gani kuhusiana na Wakili Dickson Matata kutokwepo mahakamani?
Kibatala: Ana appear mbele ya Jaji mwingine wa mahakama Kuu ambaye ni Jaji Senior
Jaji: Kama hakuna session inayoendelea huko mahakamani anaweza kuomba udhuru huko, Otherwise ni mahakama ya Rufaa na pia kama kuna kesi inaendelea huko Seniority inatake place.
Jaji: Ila ni vizuri tukawa tunajua na mjue katika kesi, kesi za Jinai zinapewa kipaumbele kuliko kesi za madai, ni vizuri tujue ni kesi gani aliyopo huko.
Kibatala: Sina Details sana ila ukiniruhusu naweza kumuuliza ili ujaze.
Jaji: Je, mawakili wa serikali kuna jambo lolote la kuongezea?
Wakili wa Serikali: Hatuna mheshimiwa
Jaji: Sawa, upande wa Serikali mpo tayari?
Wakili wa serikali: Nadhani tulikuja kwa ajili ya kesi ndogo na kuna shahidi alihitajika kuendelea, shahidi yupo tayari kuendelea
Jaji: Mawakili wa utetezi, mpo tayari kuendelea?
Kibatala: Ndiyo mheshimiwa.
Jaji: Shahidi aliyebakiza ushahidi wake apande kizimbani tuendeleee
Jaji: siku ya Ijumaa tulikuapisha, Nakukumbusha kuwa kiapo chako kinaendelea
Shahidi: Sawa Mheshimiwa
Kibatala: Unakumbuka mara ya mwisho wakati unatoa ushahidi ulisema mkiwa maeneo ya Boma Ng'ombe washtakiwa walikula Chakula. Je, unakumbuka walikula chakula gani?
Shahidi: Ndizi, Nyamachoma na MO Energy
Kibatala: Wakati shauri limehairishwa tulituma mtu huko Boma Ng'omba na Siha kutokana na unyeti wa Kesi, Je unakumbuka Jina la Muhudumu?
Shahidi: Hapana sikumbuki.
Kibatala: Je, unakumbuka jinsia yake aliyewahudumia?
Shahidi: Hapana, tulikuwa kwenye gari, Chakula afande Kingai ndiye aliyeleta
Kibatala: Je, ni mara ngapi umekuwa na watuhumiwa na kuwapatia chakula?
Shahidi: Ni jambo la kawaida mkiwa kwenye operesheni kumpatia mtu chakula
Kibatala: unafahamu PGO imetaja utaratibu wa kupatia chakula watuhumiwa?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: unafahamu kuwa PGO ndiyo ina maelekezo ya pekee juu ya utaratibu wa kumpatia chakula Mtuhumiwa?
Shahidi: na sheria mbalimbali siyo tu PGO
Kibatala: Zitaje
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwa Mujibu wa taratibu za Tanzania na kimataifa kuna hotuba inayotambua kuwa na vikosi maalum vya ugaidi Tanzania.. Je unamfahamu?
Shahidi: Ungemfuata aliyesema umuulize
Jaji: Shahidi anakuuliza wewe!
Kibatala: Je, kuna sehemu yoyote umejitambulisha wewe ni mmoja ya kikosi Maalum cha kupambana na magaidi Tanzania?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je, inaruhusiwa wakati wa kumuhoji mtuhumiwa kumchoma choma na bisibisi?
Shahidi: Hapana hairusiwi
Kibatala: Je inaruhusiwa kumchoma choma mtuhumiwa na bisibisi na kumwambia tutakufanya kama tulichokufanya Moshi?
Shahidi: Hairuhusiwi
Kibatala: Je, inaruhusiwa kumfunga mtu pingu miguuni na mikononi na kumining'iza na kumpiga na marungu kwenye unyayopaka hawezi kutembea?
Shahidi: Hairuhusiwi
Kibatala: Je, Tazara ni kituo Class A au B?
Shahidi: Hilo sifahamu
Kibatala: Ulizungumzia kuwa ulimtoa mtuhumiwa kutoka Central kwenda Mbweni?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Central ulipomtoa mtuhumiwa ni Class A au B?
Shahidi: Class A
Kibatala: Kwa hiyo ulimtoa kituo Class A kwenda class A?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je, unafahamu kuwa taratibu za kumsafirisha mtuhumiwa kwenda popote zimewekwa kwenye PGO?
Shahidi: Hilo sifahamu
Kibatala: PGO inasema kuwa wakati wa kumhamisha mtuhumiwa kutoka Point moja kwenda kwenye point nyingine inatakiwa kuandikwa Detention Register.?
Shahidi: Hilo sifahamu
Kibatala: Wewe ulikuwa Arresting Officer.?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Jaji akimaliza kuandika mwambie kuwa ni kwa PGO ya ngapi
Shahidi: Hapana sifahamu
Kibatala: Unafanya kazi kwa kutumia PGO au mazoea?
Shahidi: kwa taratibu mbalimbali
Kibatala: ikiwepo PGO
Shahidi: NDIYO
Kibatala: Je, unafahamu lolote kuhusu Moses Lijenje na umezungumzia hapa hatima ya Moses Lijenje?
Shahidi: Sikuzungumzia
Kibatala: Je, unafahamu lolote kuhusu utaratibu wa kumtangaza mtuhumiwa kwa kutumia tangazo?
Shahidi: Hapana
Kibatala: umezungumzia kuhusu KUMFUNGA Pingu mshtakiwa, Je kuna sehemu yoyote umezungumzia KUMFUNGUA pingu mshtakiwa ?
Shahidi: Kwenye maelezo yangu siku zungumzia.
Kibatala: Wakati wakili John Mallya anakuhoji kuhusu chakula alikuhoji kuhusu kiwango cha chakula mtuhumiwa alipewa, unafahamu PGO imezungumzia kiwango, kiasi na aina gani ya chakula ambacho mtuhumiwa anapaswa kupewa akiwa chini ya Ulinzi? je Unafahamu?
Shahidi: Hapana, sifahamu
Kibatala: Umezungumzia kupewa chakula watuhumiwa wakiwa Boma Ng'ombe na Himo, je umezungumzia kuhusu watuhumiwa kupewa chakula wakiwa kituo cha polisi Moshi?
Shahidi: Hapana sikuzungumzia
Kibatala: Je, umezungumzia kuhusu kuwapekua watuhumiwa mauongoni ulipowakuta, Je kwa mujibu wa PGO inaruhusiwa kumfanyia mtu Upekuzi maungoni mbele za Watu?
Shaidi: Ndiyo inaruhusiwa
Kibatala: PGO ipi?
Shahidi: sifahamu
Kibatala: nakusomea PGO 272(5) inayozungumzia kumpekua mtu mauongoni, PGO inasema kwa Kuanzia Kichwani, Kushuka chini... hapa mwisho inasema nobody search in Public view.
Shahidi: mheshimiwa inaruhusiwa Kwa mujibu wa PGO
Kibatala: Je, PGO inaruhusu kumpekua mtu maungoni hadharani?
Shahidi: inaruhusu
Kibatala: Nikikupa PGO utaonyesha ni wapi?
Shahidi: ndiyo..
Peter Kibatala anamkabidhi shahidi PGO
Shahidi: PGO inaruhusu isipokuwa kama utamvua mtu nguo, kuchuchumaa inakatazwa.
Jaji: ungesoma kama wakili Kibatala anavyosoma au ungependa kuelezea?
Shahidi: Ningependa kuelezea tu..
Kibatala: Je, UNASOMA PGO au HUSOMI?
Shahidi: SISOMI Mheshimiwa JAJI
Kibatala: Ahsante, sasa ngoja Jaji aaandike umekataa kusoma PGO kwa unachokisema.
Kibatala: Unafahamu Diary ya Afisa wa Polisi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wewe ni Gazetted au siyo Gazetted Officer?
Shahidi: Siyo Gazetted Officer
Kibatala: Unafahamu PGO inazungumzia Afisa wa Polisi wa cheo kama cha kwako anapotoka eneo la kazi?
Shahidi: Siyo Gazetted Officer
Kibatala: Je unafahamu RPC anatakiwa kukupa wewe ruhusa?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je unafahamu RPC anatakiwa kukupa wewe ruhusa?
Shahidi: Siyo RPC pekee yake
Kibatala: Je nani mwingine?
Shahidi: RPC, RCO na Staff Officer
Kibatala: Je Ruhusa ya kipolisi inatolewa kwa maandishi au kwa mdomo?
Shahidi: maandishi
Kibatala: Je umetoa nyaraka (Movement Order) Mahakamani.?
Shahidi: PGO inasema Officer ambaye ni Gazetted haitaji Movement Order na kwa cheo changu Movement yangu ilikuwa inabeba Wengine.
Kibatala: Tuokoe muda, Sijakuuliza hicho
Shahidi: Muda tunao Mheshimiwa
Jaji: Jibu kuwa ulikuwa na kibali au hukuwa na kibali
Shahidi: Ndiyo nilikuwa namjibu
Kibatala: Wakati unatoa ushahidi wako hapa na ulionyesha hiyo Movement Order?
Shahidi: Ukimaloza inarudishwa ofisini
Kibatala: Ulitoa mahakamani au hukutoa?
Shahidi: Haikuhitajika, sikuulizwa lakini ipo..
Kibatala: Ulitoa au hukutoa?
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Je, unafahamu hata RCO kama afande kingai anasehemu anatakiwa kuripoti?
Shahidi: Siwezi kumuongelea Afande wangu.
Kibatala: Ongelea concept unaifahamu au huifahamu, kwa sababu hata mimi nafahamu juu ya mawakili Senior taratibu zao zikoje.
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Umezungumzia mtuhumiwa kuwa na Jacket
Shahidi: ndiyo
Kibatala: Je, unafahamu kuwa hilo Jacket ndilo lililotumika kumfungia machoni asione mtuhumiwa?
Shahidi: Hapana sifahamu
Kibatala: Je, unafahamu anayetakiwa kufanya upekuzi ni afisa wa Polisi mkamataji
Shahidi: Yeyote anaweza kufanya upekuzi
Kibatala: Je nikikupa PGO unaweza kunionyesha popote ambapo polisi yeyote anaweza kufanya upekuzi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wakati wote wa kazi yako ulishawahi kufuata PGO ukawa nayo karibu na kuitumia?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mh. Jaji ni hayo tu, sina swali lingine
Jaji: Ahsante, kila siku naona mtuhumiwa mmoja tu ndiyo anakunywa maji, mmewapa wengine? wapeni Maji wanywe,Askari Magereza Myakague ni haya tunayokunywa wote
Jaji: Mawakili wa Serikali kuna lolote kwa ajili ya Re: examination?
Wakili wa serikali: Tupo tayari
Wakili wa Serikali: Nitakuhoji kwa ufafanuzi. Je, Ijumaa wakati Kibatala anakuhoji ulisema anachanganya PGO ulikuwa una maana gani?
Shahidi: Wakati wakili Kibatala ananihoji alitaka PGO ya 272 leo nashukuru kafanya Research kidogo kwa sababu alikuwa anaongela kuhusu kuchukua Maelezo, Leo ndiyo kanihoji kwa usahihi kuhusu ukamataji.
Wakili wa Serikali: Hiyo PGO inayozungumzia kuhusu maelezo eleza ni kwa namna gani?
Shahidi: wakati unamchukulia maelezo ndiyo unamuhoji kwa kumuonya kama utatumia mahakamani Kama ushahidi
Wakili wa Serikali: Wakati Kibatala anakuhoji kuhusu kumtoboa na bisibisi kila kitu ulikuwa unasema hairuhusiwi
Shahidi: Hairuhusiwi kwa mujibu wa katiba zetu, kama torture na vinginevyo.
Wakili wa Serikali: Fafanua kuhusiana kumfunga na mtu kwa Jacket
Shahidi: Kama nilivyomuuliza wakili Kibatala hairuhusiwi na hakuna haja ya kufanya hivyo
Wakili wa Serikali: Hakuna sehemu uliomba ruhusa kufuata Notebook yako hapa Mahakamani, kwanini ulifanya hivyo?
Shahidi: Sikuhitaji kwa sababu yote niliyoyaeleza nilikuwa nayakaumbuka
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuwa hukuandika katika maelezo yako kama mliwapatia chakula Adam kasekwa mkiwa Boma Ng'ombe na Himo
Shahidi: Sikuandika katika maelezo yangu kwa sababu nili' focus katika mambo ya ukamataji
Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa pia kuhusiana na uhitaji wa movement Order kutoka kituo chako cha kazi, Kwanini hukuileta hapa mahakamani?
Shahidi: Kwa mujibu wa taratibu, Polisi ukimaliza kuitumia Movement Order umarudisha ofisini, nikaendelea na kazi.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mimi ni hayo hatuna kingine..
Jaji: Shahidi tunashukuru umemaliza ushahidi wako unaweza kwenda sasa..
Shahidi anatoka kizimbani.
Jaji: Upande wa Serikali.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tunaomba kuendelea na shahidi wa tatu..
Jaji: sawa Mleteni Shahidi wa 3 Mahakama ipo kimya.
---
Shahidi wa tatu amefika
Jaji: Shahidi jitambulishe
Shahidi: Naitwa Askari namba H2343, afande Msemwa
Jaji: Apa
Shahidi: Mimi Afande H2343 naapa Ninachosema kitakuwa kweli, Eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie
Jaji: Anayehoji nani upande wa serikali?
Wakili wa Serikali: MIMI NASSORO KATUGA
Wakili wa Serikali: Shahidi ungependa kusimama au kukaa?
Shahidi: Kusimama
Wakili wa Serikali: Kituo chako cha Polisi ni wapi?
Shahidi: Kituo cha Polisi Oysterbay
Wakili wa Serikali: upo tangu lini?
Shahidi: Mwaka huu January/February
Mawakili wa Serikali: Umeajiriwa mwaka gani? Shahidi: 2013 Wakili wa Serikali: Ulianzia kituo gani?
Shahidi: Nilianzia Polisi Ilala na baadae nikahamia Central Polisi
Wakili wa Serikali: Central ulikuwa mpaka lini?
Shahidi: 2014 Mwanzoni Mpaka Mwaka jana mwishoni kuanzia January 2021 nikaenda Oysterbay
Wakili wa Serikali: Oyesterbay upo kitengo gani?
Shahidi: Upelelezi
Wakili wa Serikali: Ukiwa Central Polisi Ilala ulikuwa unafanya kazi gani?
Shahidi: Nilikuwa General Duty sisi ambao tunavaa uniform kawaida tofauti na wale wa kofia nyekundu FFU
Wakili wa Serikali: Ulikuwa na Jukumu gani?
Shahidi: Nilikuwa nalinda raia na mali zao.
Shahidi: Doria na ukaaji wa point pamoja na kuwa chumba cha mashtaka
Wakili wa Serikali: Umezungumzia chumba cha mashtaka ni nini?
Shahidi: Ni pale wanapokaa Askari (CRO) kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali na ufunguaji wa kesi na kupokea watuhumiwa wanaoletwa
Wakili wa Serikali: Watuhumiwa wanaoletwa kutoka wapi?
Shahidi: Sehemu mbalimbali
Wakili wa Serikali: Unasema ulikuwa kwenye chumba cha mashitaka, ufanyaji kazi unakuwa ni Vipi?
Shahidi: Kwanza lazima kiwe na CRO incharge kazi utakazofanya ni zile utazopewa na CRO incharge
Jaji: naona Joto ni kali, naomba madirisha yafunguliwe.
Wakili wa Serikali: Naweza kukumbushwa alipoishia?
Jaji: CRO panakuwa na Incharge
Wakili wa Serikali: Enheee Endelea...
Shahidi: Unakuwa unafanya majukumu unayopewa na Incharge.
Wakili wa Serikali: Iambie mahakama sasa kwa ufupi sana mnapokuwa mnapokea watuhumiwa nini kinafanyika?
S
hahidi: Mnapopolea watuhumiwa kuna taratibu zake ukiwa CRO kinakamilishwa na kitu kinaitwa DR (Detention Register)
Wakili wa Serikali: Iambie mahakama ni kitu gani
Shahidi: Ni kitabu kinachotunza kumbukumbu za kituo cha Polisi
Wakili wa Serikali: Kwa namna gani!?
Shahidi: Kuna taratibu zake za kumpokea mtuhumiwa na askari anayekuwa chumba cha mashtaka uzifahamu.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ni taratibu gani..
Shahidi: Kwanza wakati unamuhoji ni Kumpekua ili wakati unampekua unakuwa mpo nae salama
Wakili wa Serikali: Wakati mnampekua mnafanya utaratibu gani?
Shahidi: Chochote kinaweza kuanza kuhojiwa na kumpekua
Shahidi: Kiuhalisia nilichofundishwa CCP kuwa mtu anapokuwa amekamatwa anakuwa na Mawazo yeye mwenyewe
Wakili wa Serikali: Mimi sitaki mawazo yako, sasa wewe unafanya kitu gani?
Shahidi: kuhakikisha haingii na kitu chenye madhara Mahabusu..
Wakili wa Serikali: Kingine?
Shahidi: Kumuingiza kitabu cha mahabusu (Detention Register)
Wakili wa Serikali: Unampekuaje?
Shahidi: Unampekua kwa kumwambia nyoosha mikono Juu, kwa kugeukia ukuta na kuushika, na mwisho wa kumpekua ni kumwambia kaa chini
Wakili wa Serikali: unamhoji kwa namna gani
Shahidi: Kama Mtuhumiwa analetwa kwa kesi ambayo imeshafunguliwa anatakiwa awe na Case reference namba yake
Wakili wa Serikali: Kesi inayokuwa imefunguliwa wapi?
Shahidi: Popote pale ndani ya Tanzania
Wakili wa Serikali: Hiyo Reference inahusisha vitu gani?
Shahidi: Reference ndiyo kitu kinafahamila sana Mtaani RB, mfano kesi za Oysterbay zinakuwa na neno Kifupisho OB kwa maana Oysterbay Mkwaju, RB kwa maana imeripotiwa
Wakili wa Serikali: Hiyo ya Oysterbay je ya Central?
Shahidi: Cental ni neno CD na reference namba kesi ilianza kupelelezwa inakuwa na IR badala ya RB
Wakili wa Serikali: Baada ya namba nini kingine analeta?
Shahidi: na Jina la kosa analokuwa ametenda
Wakili wa Serikali: Vitu gani Vingine?
Shahidi: Unapata Particulars kwa aliyemleta mtuhumiwa na zingine kwa mtuhumiwa mwenyewe.
Wakili wa Serikali: zipi hizo?
Shahidi: Majina, Miaka yake, Jinsia yake..
Wakili wa Serikali: Jinsia ukimaanisha?
Shahidi: Kama ni mwanamke au mwanaume
Jaji: Wewe unajuaje?
Shahidi: Namkagua pia kuthibitisha
Wakili wa Serikali: Kingine?
Shahidi: Hali yake ya Ki afya
Wakili wa Serikali: Akikujibu wewe unafanyaje?
Shahidi: Lazima ujiridhishe kama mgongoni unaweza kumkagua
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama kwenye ukaguzi wa jinsia mnafanya kitu gani?
Shahidi: Ni kujihakikishia physically
Jaji: Ina maana mwanamke unamkagua wewe?
Wakili wa Serikali: Ndiyo nilichotaka ila niliogopa nisije kuonekana namuongoza
Shahidi: CRO panakuwa na Askari wa kike kwa Ukaguzi wa Mwanamke. Akiletwa mwanamke ukaguzi utafanywa na Askari wa Kike
Wakili wa Serikali: Tarehe 7 Mwezi wa 8 2020 Ulikuwa wapi
Shahidi: Nilikuwa bado sijahamia Oysterbay nilikwa bado mkoa wa kipolisi Ilala, Central
Wakili wa Serikali: Unakumbuka nini siku hiyo?
Shahidi: Niliiingia kazini, nilikuwa na zamu ya CRO shifti
Wakili wa Serikali: Unaposema CRO shift unamaana gani?
Shahidi: Pale CRO panakuwa na Shift sababu tunafanya kazi masaa 24 kwa hiyo tunafanya kazi kwa zamu
Wakili wa Serikali: Ulipoingia kazini ulifanya nini?
Shahidi: Niliingia kazini Alfajiri na askari wengine watano
Wakili wa Serikali: Unaweza kuwataja kama unawakumbuka Shahidi: WP fatuma,Aziz na wengine
Wakili wa Serikali: Mliingia kazini Saa ngapi?
Shahidi: 12 Alfajiri
Wakili wa Serikali: Siku hiyo CRO Incharge alikuwa ni nani?
Shahidi: Palikuwa na Inspector msaidizi wa Polisi
Wakili wa Serikali: Siku hiyo wewe ulikuwa na jukumu gani
Shahidi: nilikuwa ni mtunza mahabusu, mahabusu wa kiume ni mimi, na wakike wata dili na WP SEMENI
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Jukumu la Kufungua kesi.?
Shahidi: Nakumbuka Afande Emmanuel na Afande Samuel
Wakili wa Serikali: Ulikuwa na majukumu gani
Shahidi: ilikuwa saa 12 kasoro nilifika na kupangiwa majukumu na wengine
Wakili wa Serikali: Kitu gani ulifanya
Shahidi: Baada ya kukabidhiwa mahabusu naenda kuhakiki kule mahabusu chini kwa kutaja jina mojamoja
Wakili wa Serikali: Nini Unakumbuka kikafuata?
Shahidi: Siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo baada ya kukagua mahabusu nikamuona Afande Kingai akiwa anaingia na Mahabusu
Wakili wa Serikali: Mahakama ingependa kujua ulikuwa unamfahamu kabla?
Shahidi: Ndiyo nilikuwa namfahamu
Wakili wa Serikali: alikuwa na nani?
Shahidi: Afande Jumanne
Wakili wa Serikali: ulikuwa unamfahamu Jumanne?
Shahidi: ndiyo, alikuwa makao Makuu ya polisi kabla
Wakili wa Serikali: nini kilifuata?
Shahidi: Akaniambia ni watuhumiwa kesi yao imefunguliwa hapa
Wakili wa Serikali: Unakumbuka RB yao?
Shahidi: Sikumbuli RB ila kosa nakumbuka
Wakili wa Serikali: Unakumbuka kosa gani Shahidi Kula njama za kutenda makosa ya ugaidi
Jaji: Naona tunge' break kidogo... Tutarudi saa saba na nusu kuendelea...
TUENDELEE BAADA YA BREAK FUPI
Wakili wa Serikali: Ikupemdeze Mheshimiwa jaji column yetu ya kwanza ipo vilevile tupo tayari kuendelea.
Kibatala: Tupo tayari kuendelea.
Jaji: Wakili aliyekuwa anamuongoza shahidi aendelee.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa naomba kukumbushwa na mahakama tuliishia wapi.
Jaji: Wakati wa kuandika RB na IR namba
Wakili wa Serikali: Unazikumbuka?
Shahidi: Hapana lakini zile namba CD za Central haziwezi kujirudia na kufanana
Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea hizo reference kiliendelea nini?
Shahidi: Afande kingai na Afande Jumanne walitoka
Wakili wa Serikali: Kiliendelea nini baada ya kupokea hizo reference?
Shahidi: Taratibu zingine zilifuatwa baada ya kuwa na watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Eleza mahakama nini kilifuata
Shahidi: Nilianza kumpekua mmoja mmoja, namwambia nyoosha mikono juu, kaa chini anakaa.
Wakili wa Serikali: Iambie mahakama baada ya Afande Jumanne kuwaleta watuhumiwa wakiwa na pingu nini kilifuatia kuhusu pingu?
Shahidi: Baada ya kufungua pingu kila mmoja na pingu yake, alisema akituachia pingu zitapotea
Wakili wa Serikali: Hujasema nani alifungua pingu
Shahidi: Mimi nilifungua siyo lazima nitumie pingu za afande Jumanne kwa sababu funguo za pingu zinaingiliana
Jaji: Unaposema koti unamaanisha nini?
Shahidi: Namaanisha Jacket
Jaji: Naamini wakina Kibatala mnaelewa!?
Kibatala: Ndiyo Mheshimiwa
Wakili wa Serikali: Baada ya kuwapekua nini kilifuata?
Shahidi: Nilianza kuchukua taarifa zao
Wakili wa Serikali: Kama zipi?
Shahidi: Kama Jina, Miaka, Jinsia na Dini
Wakili wa Serikali: unaweza kukumbuka majiina yake
Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya
Wakili wa Serikali: Wakati huo unaandika wapi?
Shahidi: Kwenye Detention Register
Wakili wa Serikali: Ulimuuliza nini kingine?
Shahidi: Alijibu ki Afya yupo vizuri
Wakili wa Serikali: Akakuambiaje kuhusu Afya?
Shahidi: Mzima
Wakili wa Serikali: Ulijiridhisheje?