Yaliyojiri kesi ya Mbowe na Wenzake: Upande wa Mashtaka waendelea kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka Septemba 24, 2021

Yaliyojiri kesi ya Mbowe na Wenzake: Upande wa Mashtaka waendelea kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka Septemba 24, 2021

Huyo ni HAKAINDE wa Zambia, huku kwetu JPM hakutaka hata daraja la chini wala maafisa 2
Mabalozi wanaelewa
Pamoja na JPM kugoma kwenda nje akisema ni matumizi mabaya ya pesa walimtukana na leo wanamsifia haikande


USSR
 
Jaji: Wewe elezea yanayokuhusu tu, sababu mwanzo hukuongelea mambo ya DR ukasema huyakumbuki..

ha ha ha, shahidi kapata kidonge chake kujifanya mjuajiiii
 
Ni hatari sana. Nakumbuka jinsi wakili Lakha alivyosababisha baadhi ya mashahidi kuomba udhuru. Unahojiwa mpaka unajiona wewe sio shahidi bali ni mtuhumiwa wa kesi ya Uhaini!!!
Lakini mwisho wa mchezo hukumu ya Jaji Mzavas ilikuwaje? Kama uliifuatilia kesi ile mimi bado sijaona sababu ya kushangilia isipokuwa utulivu unahitajika
 
Jaji ameingia Mahakamani.

Kesi Na. 16 ya mwaka 2021 inatajwa

Kesi namba 16 ya 2021, jamhuri dhidi ya Khalfan Bwire, Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Jaji anamuita Wakili wa Serikali...

Wakili wa Serikali anatambulisha Jopo lake
  1. Robert Kidando
  2. Nassoro Katuga
  3. Ignas Mwanuka
  4. Esther Martin
  5. Tulumanywa Majigo
Pia anawatambulisha mawakili na mawakili wengine watatu.

Mawakili upande wa Utetezi wanatambulishwa
  1. Peter Kibatala
  2. Jeremiah Mtobesya
  3. Fred Kihwelo
  4. John Malya
  5. Gaston Garubindi
  6. Seleman Mtauka
  7. Michael Mwangasa
  8. Evaresta Kisanga
  9. Khadija Aron
  10. Maria Mushi
  11. Deogratius Mahinyila
  12. Nashon Nkungu
  13. Jebra Kambole
Anasema anamtambulisha Wakili Fredrick Kihwelo kwa sababu maalum

Mawakili wa mshtakiwa wa kwanza ni Jeremiah Mtobesya na Nashon Nkungu.
Mshtakiwa wa tatu atawakilishwa na Dickson Matata na Fredrick Kihwelo
Mshtakiwa wa pili atawakilishwa na John Mallya
Mawakili wengine wote watamwakilisha mshtakiwa wa nne

Jaji anauliza kama mawakili wa serikali wanalolote Juu ya ingizo Jipya la wakili Fredrick Kihwelo kama kuna mgongano wa maslahi.

Wakili wa Serikali anasema hakuna tatizo kwa sababu tangu kesi ianze hajaonekana kwenye Column yoyote.

Jaji: hiyo wakili Fredrick Kihwelo anamshikia mikoba wakili Dickson Matata au atakuwa moja kwa moja kwa mshtakiwa watatu?

Kibatala: kuanzia leo mshtakiwa watatu atawakilishwa na wakili Fredrick Kihwelo na kusaidiana na Dickson Matata ambaye leo hayupo mahakamani

Wakili wa Serikali anahoji mshtakiwa mwenyewe anasemaje baada ya kumsikiliza Kibatala

Jaji: hilo tayari nimeshaliongelea kuwa baada ya utambulisho wa Kibatala nitamuhoji Mshtakiwa

Jaji: Ling'wenya bila shaka umesikia?

Ling'wenya: Nimesikia Mh. nakubaliana na Wakili Kibatala

Jaji: Kuna taarifa gani kuhusiana na Wakili Dickson Matata kutokwepo mahakamani?

Kibatala: Ana appear mbele ya Jaji mwingine wa mahakama Kuu ambaye ni Jaji Senior

Jaji: Kama hakuna session inayoendelea huko mahakamani anaweza kuomba udhuru huko, Otherwise ni mahakama ya Rufaa na pia kama kuna kesi inaendelea huko Seniority inatake place.

Jaji: Ila ni vizuri tukawa tunajua na mjue katika kesi, kesi za Jinai zinapewa kipaumbele kuliko kesi za madai, ni vizuri tujue ni kesi gani aliyopo huko.

Kibatala: Sina Details sana ila ukiniruhusu naweza kumuuliza ili ujaze.

Jaji: Je, mawakili wa serikali kuna jambo lolote la kuongezea?

Wakili wa Serikali: Hatuna mheshimiwa

Jaji: Sawa, upande wa Serikali mpo tayari?

Wakili wa serikali: Nadhani tulikuja kwa ajili ya kesi ndogo na kuna shahidi alihitajika kuendelea, shahidi yupo tayari kuendelea

Jaji: Mawakili wa utetezi, mpo tayari kuendelea?

Kibatala: Ndiyo mheshimiwa.

Jaji: Shahidi aliyebakiza ushahidi wake apande kizimbani tuendeleee

Jaji: siku ya Ijumaa tulikuapisha, Nakukumbusha kuwa kiapo chako kinaendelea

Shahidi: Sawa Mheshimiwa

Kibatala: Unakumbuka mara ya mwisho wakati unatoa ushahidi ulisema mkiwa maeneo ya Boma Ng'ombe washtakiwa walikula Chakula. Je, unakumbuka walikula chakula gani?

Shahidi: Ndizi, Nyamachoma na MO Energy

Kibatala: Wakati shauri limehairishwa tulituma mtu huko Boma Ng'omba na Siha kutokana na unyeti wa Kesi, Je unakumbuka Jina la Muhudumu?

Shahidi: Hapana sikumbuki.

Kibatala: Je, unakumbuka jinsia yake aliyewahudumia?

Shahidi: Hapana, tulikuwa kwenye gari, Chakula afande Kingai ndiye aliyeleta

Kibatala: Je, ni mara ngapi umekuwa na watuhumiwa na kuwapatia chakula?

Shahidi: Ni jambo la kawaida mkiwa kwenye operesheni kumpatia mtu chakula

Kibatala: unafahamu PGO imetaja utaratibu wa kupatia chakula watuhumiwa?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: unafahamu kuwa PGO ndiyo ina maelekezo ya pekee juu ya utaratibu wa kumpatia chakula Mtuhumiwa?

Shahidi: na sheria mbalimbali siyo tu PGO

Kibatala: Zitaje

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwa Mujibu wa taratibu za Tanzania na kimataifa kuna hotuba inayotambua kuwa na vikosi maalum vya ugaidi Tanzania.. Je unamfahamu?

Shahidi: Ungemfuata aliyesema umuulize

Jaji: Shahidi anakuuliza wewe!

Kibatala: Je, kuna sehemu yoyote umejitambulisha wewe ni mmoja ya kikosi Maalum cha kupambana na magaidi Tanzania?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je, inaruhusiwa wakati wa kumuhoji mtuhumiwa kumchoma choma na bisibisi?

Shahidi: Hapana hairusiwi

Kibatala: Je inaruhusiwa kumchoma choma mtuhumiwa na bisibisi na kumwambia tutakufanya kama tulichokufanya Moshi?

Shahidi: Hairuhusiwi

Kibatala: Je, inaruhusiwa kumfunga mtu pingu miguuni na mikononi na kumining'iza na kumpiga na marungu kwenye unyayopaka hawezi kutembea?

Shahidi: Hairuhusiwi

Kibatala: Je, Tazara ni kituo Class A au B?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Ulizungumzia kuwa ulimtoa mtuhumiwa kutoka Central kwenda Mbweni?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Central ulipomtoa mtuhumiwa ni Class A au B?

Shahidi: Class A

Kibatala: Kwa hiyo ulimtoa kituo Class A kwenda class A?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, unafahamu kuwa taratibu za kumsafirisha mtuhumiwa kwenda popote zimewekwa kwenye PGO?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: PGO inasema kuwa wakati wa kumhamisha mtuhumiwa kutoka Point moja kwenda kwenye point nyingine inatakiwa kuandikwa Detention Register.?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Wewe ulikuwa Arresting Officer.?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jaji akimaliza kuandika mwambie kuwa ni kwa PGO ya ngapi

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Unafanya kazi kwa kutumia PGO au mazoea?

Shahidi: kwa taratibu mbalimbali

Kibatala: ikiwepo PGO

Shahidi: NDIYO

Kibatala: Je, unafahamu lolote kuhusu Moses Lijenje na umezungumzia hapa hatima ya Moses Lijenje?

Shahidi: Sikuzungumzia

Kibatala: Je, unafahamu lolote kuhusu utaratibu wa kumtangaza mtuhumiwa kwa kutumia tangazo?

Shahidi: Hapana

Kibatala: umezungumzia kuhusu KUMFUNGA Pingu mshtakiwa, Je kuna sehemu yoyote umezungumzia KUMFUNGUA pingu mshtakiwa ?

Shahidi: Kwenye maelezo yangu siku zungumzia.

Kibatala: Wakati wakili John Mallya anakuhoji kuhusu chakula alikuhoji kuhusu kiwango cha chakula mtuhumiwa alipewa, unafahamu PGO imezungumzia kiwango, kiasi na aina gani ya chakula ambacho mtuhumiwa anapaswa kupewa akiwa chini ya Ulinzi? je Unafahamu?

Shahidi: Hapana, sifahamu

Kibatala: Umezungumzia kupewa chakula watuhumiwa wakiwa Boma Ng'ombe na Himo, je umezungumzia kuhusu watuhumiwa kupewa chakula wakiwa kituo cha polisi Moshi?

Shahidi: Hapana sikuzungumzia

Kibatala: Je, umezungumzia kuhusu kuwapekua watuhumiwa mauongoni ulipowakuta, Je kwa mujibu wa PGO inaruhusiwa kumfanyia mtu Upekuzi maungoni mbele za Watu?

Shaidi: Ndiyo inaruhusiwa

Kibatala: PGO ipi?

Shahidi: sifahamu

Kibatala: nakusomea PGO 272(5) inayozungumzia kumpekua mtu mauongoni, PGO inasema kwa Kuanzia Kichwani, Kushuka chini... hapa mwisho inasema nobody search in Public view.

Shahidi: mheshimiwa inaruhusiwa Kwa mujibu wa PGO

Kibatala: Je, PGO inaruhusu kumpekua mtu maungoni hadharani?

Shahidi: inaruhusu

Kibatala: Nikikupa PGO utaonyesha ni wapi?

Shahidi: ndiyo..

Peter Kibatala anamkabidhi shahidi PGO

Shahidi: PGO inaruhusu isipokuwa kama utamvua mtu nguo, kuchuchumaa inakatazwa.

Jaji: ungesoma kama wakili Kibatala anavyosoma au ungependa kuelezea?

Shahidi: Ningependa kuelezea tu..

Kibatala: Je, UNASOMA PGO au HUSOMI?

Shahidi: SISOMI Mheshimiwa JAJI

Kibatala: Ahsante, sasa ngoja Jaji aaandike umekataa kusoma PGO kwa unachokisema.

Kibatala: Unafahamu Diary ya Afisa wa Polisi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wewe ni Gazetted au siyo Gazetted Officer?

Shahidi: Siyo Gazetted Officer

Kibatala: Unafahamu PGO inazungumzia Afisa wa Polisi wa cheo kama cha kwako anapotoka eneo la kazi?

Shahidi: Siyo Gazetted Officer

Kibatala: Je unafahamu RPC anatakiwa kukupa wewe ruhusa?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je unafahamu RPC anatakiwa kukupa wewe ruhusa?

Shahidi: Siyo RPC pekee yake

Kibatala: Je nani mwingine?

Shahidi: RPC, RCO na Staff Officer

Kibatala: Je Ruhusa ya kipolisi inatolewa kwa maandishi au kwa mdomo?

Shahidi: maandishi

Kibatala: Je umetoa nyaraka (Movement Order) Mahakamani.?

Shahidi: PGO inasema Officer ambaye ni Gazetted haitaji Movement Order na kwa cheo changu Movement yangu ilikuwa inabeba Wengine.

Kibatala: Tuokoe muda, Sijakuuliza hicho

Shahidi: Muda tunao Mheshimiwa

Jaji: Jibu kuwa ulikuwa na kibali au hukuwa na kibali

Shahidi: Ndiyo nilikuwa namjibu

Kibatala: Wakati unatoa ushahidi wako hapa na ulionyesha hiyo Movement Order?

Shahidi: Ukimaloza inarudishwa ofisini

Kibatala: Ulitoa mahakamani au hukutoa?

Shahidi: Haikuhitajika, sikuulizwa lakini ipo..

Kibatala: Ulitoa au hukutoa?

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Je, unafahamu hata RCO kama afande kingai anasehemu anatakiwa kuripoti?

Shahidi: Siwezi kumuongelea Afande wangu.

Kibatala: Ongelea concept unaifahamu au huifahamu, kwa sababu hata mimi nafahamu juu ya mawakili Senior taratibu zao zikoje.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Umezungumzia mtuhumiwa kuwa na Jacket

Shahidi: ndiyo

Kibatala: Je, unafahamu kuwa hilo Jacket ndilo lililotumika kumfungia machoni asione mtuhumiwa?

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Je, unafahamu anayetakiwa kufanya upekuzi ni afisa wa Polisi mkamataji

Shahidi: Yeyote anaweza kufanya upekuzi

Kibatala: Je nikikupa PGO unaweza kunionyesha popote ambapo polisi yeyote anaweza kufanya upekuzi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati wote wa kazi yako ulishawahi kufuata PGO ukawa nayo karibu na kuitumia?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mh. Jaji ni hayo tu, sina swali lingine

Jaji: Ahsante, kila siku naona mtuhumiwa mmoja tu ndiyo anakunywa maji, mmewapa wengine? wapeni Maji wanywe,Askari Magereza Myakague ni haya tunayokunywa wote

Jaji: Mawakili wa Serikali kuna lolote kwa ajili ya Re: examination?

Wakili wa serikali: Tupo tayari

Wakili wa Serikali: Nitakuhoji kwa ufafanuzi. Je, Ijumaa wakati Kibatala anakuhoji ulisema anachanganya PGO ulikuwa una maana gani?

Shahidi: Wakati wakili Kibatala ananihoji alitaka PGO ya 272 leo nashukuru kafanya Research kidogo kwa sababu alikuwa anaongela kuhusu kuchukua Maelezo, Leo ndiyo kanihoji kwa usahihi kuhusu ukamataji.

Wakili wa Serikali: Hiyo PGO inayozungumzia kuhusu maelezo eleza ni kwa namna gani?

Shahidi: wakati unamchukulia maelezo ndiyo unamuhoji kwa kumuonya kama utatumia mahakamani Kama ushahidi

Wakili wa Serikali: Wakati Kibatala anakuhoji kuhusu kumtoboa na bisibisi kila kitu ulikuwa unasema hairuhusiwi

Shahidi: Hairuhusiwi kwa mujibu wa katiba zetu, kama torture na vinginevyo.

Wakili wa Serikali: Fafanua kuhusiana kumfunga na mtu kwa Jacket

Shahidi: Kama nilivyomuuliza wakili Kibatala hairuhusiwi na hakuna haja ya kufanya hivyo

Wakili wa Serikali: Hakuna sehemu uliomba ruhusa kufuata Notebook yako hapa Mahakamani, kwanini ulifanya hivyo?

Shahidi: Sikuhitaji kwa sababu yote niliyoyaeleza nilikuwa nayakaumbuka

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuwa hukuandika katika maelezo yako kama mliwapatia chakula Adam kasekwa mkiwa Boma Ng'ombe na Himo

Shahidi: Sikuandika katika maelezo yangu kwa sababu nili' focus katika mambo ya ukamataji

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa pia kuhusiana na uhitaji wa movement Order kutoka kituo chako cha kazi, Kwanini hukuileta hapa mahakamani?

Shahidi: Kwa mujibu wa taratibu, Polisi ukimaliza kuitumia Movement Order umarudisha ofisini, nikaendelea na kazi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mimi ni hayo hatuna kingine..

Jaji: Shahidi tunashukuru umemaliza ushahidi wako unaweza kwenda sasa..

Shahidi anatoka kizimbani.

Jaji: Upande wa Serikali.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tunaomba kuendelea na shahidi wa tatu..

Jaji: sawa Mleteni Shahidi wa 3 Mahakama ipo kimya.

---

Shahidi wa tatu amefika

Jaji
: Shahidi jitambulishe

Shahidi: Naitwa Askari namba H2343, afande Msemwa

Jaji: Apa

Shahidi: Mimi Afande H2343 naapa Ninachosema kitakuwa kweli, Eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie

Jaji: Anayehoji nani upande wa serikali?

Wakili wa Serikali: MIMI NASSORO KATUGA

Wakili wa Serikali: Shahidi ungependa kusimama au kukaa?

Shahidi: Kusimama

Wakili wa Serikali: Kituo chako cha Polisi ni wapi?

Shahidi: Kituo cha Polisi Oysterbay

Wakili wa Serikali: upo tangu lini?

Shahidi: Mwaka huu January/February

Mawakili wa Serikali: Umeajiriwa mwaka gani? Shahidi: 2013 Wakili wa Serikali: Ulianzia kituo gani?

Shahidi: Nilianzia Polisi Ilala na baadae nikahamia Central Polisi

Wakili wa Serikali: Central ulikuwa mpaka lini?

Shahidi: 2014 Mwanzoni Mpaka Mwaka jana mwishoni kuanzia January 2021 nikaenda Oysterbay

Wakili wa Serikali: Oyesterbay upo kitengo gani?

Shahidi: Upelelezi

Wakili wa Serikali: Ukiwa Central Polisi Ilala ulikuwa unafanya kazi gani?

Shahidi: Nilikuwa General Duty sisi ambao tunavaa uniform kawaida tofauti na wale wa kofia nyekundu FFU

Wakili wa Serikali: Ulikuwa na Jukumu gani?

Shahidi: Nilikuwa nalinda raia na mali zao.

Shahidi: Doria na ukaaji wa point pamoja na kuwa chumba cha mashtaka

Wakili wa Serikali: Umezungumzia chumba cha mashtaka ni nini?

Shahidi: Ni pale wanapokaa Askari (CRO) kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali na ufunguaji wa kesi na kupokea watuhumiwa wanaoletwa

Wakili wa Serikali: Watuhumiwa wanaoletwa kutoka wapi?

Shahidi: Sehemu mbalimbali

Wakili wa Serikali: Unasema ulikuwa kwenye chumba cha mashitaka, ufanyaji kazi unakuwa ni Vipi?

Shahidi: Kwanza lazima kiwe na CRO incharge kazi utakazofanya ni zile utazopewa na CRO incharge

Jaji: naona Joto ni kali, naomba madirisha yafunguliwe.

Wakili wa Serikali: Naweza kukumbushwa alipoishia?

Jaji: CRO panakuwa na Incharge

Wakili wa Serikali: Enheee Endelea...

Shahidi: Unakuwa unafanya majukumu unayopewa na Incharge.

Wakili wa Serikali: Iambie mahakama sasa kwa ufupi sana mnapokuwa mnapokea watuhumiwa nini kinafanyika?

Shahidi: Mnapopolea watuhumiwa kuna taratibu zake ukiwa CRO kinakamilishwa na kitu kinaitwa DR (Detention Register)

Wakili wa Serikali: Iambie mahakama ni kitu gani

Shahidi: Ni kitabu kinachotunza kumbukumbu za kituo cha Polisi

Wakili wa Serikali: Kwa namna gani!?

Shahidi: Kuna taratibu zake za kumpokea mtuhumiwa na askari anayekuwa chumba cha mashtaka uzifahamu.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ni taratibu gani..

Shahidi: Kwanza wakati unamuhoji ni Kumpekua ili wakati unampekua unakuwa mpo nae salama

Wakili wa Serikali: Wakati mnampekua mnafanya utaratibu gani?

Shahidi: Chochote kinaweza kuanza kuhojiwa na kumpekua

Shahidi: Kiuhalisia nilichofundishwa CCP kuwa mtu anapokuwa amekamatwa anakuwa na Mawazo yeye mwenyewe

Wakili wa Serikali: Mimi sitaki mawazo yako, sasa wewe unafanya kitu gani?

Shahidi: kuhakikisha haingii na kitu chenye madhara Mahabusu..

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Kumuingiza kitabu cha mahabusu (Detention Register)

Wakili wa Serikali: Unampekuaje?

Shahidi: Unampekua kwa kumwambia nyoosha mikono Juu, kwa kugeukia ukuta na kuushika, na mwisho wa kumpekua ni kumwambia kaa chini

Wakili wa Serikali: unamhoji kwa namna gani

Shahidi: Kama Mtuhumiwa analetwa kwa kesi ambayo imeshafunguliwa anatakiwa awe na Case reference namba yake

Wakili wa Serikali: Kesi inayokuwa imefunguliwa wapi?

Shahidi: Popote pale ndani ya Tanzania

Wakili wa Serikali: Hiyo Reference inahusisha vitu gani?

Shahidi: Reference ndiyo kitu kinafahamila sana Mtaani RB, mfano kesi za Oysterbay zinakuwa na neno Kifupisho OB kwa maana Oysterbay Mkwaju, RB kwa maana imeripotiwa

Wakili wa Serikali: Hiyo ya Oysterbay je ya Central?

Shahidi: Cental ni neno CD na reference namba kesi ilianza kupelelezwa inakuwa na IR badala ya RB

Wakili wa Serikali: Baada ya namba nini kingine analeta?

Shahidi: na Jina la kosa analokuwa ametenda

Wakili wa Serikali: Vitu gani Vingine?

Shahidi: Unapata Particulars kwa aliyemleta mtuhumiwa na zingine kwa mtuhumiwa mwenyewe.

Wakili wa Serikali: zipi hizo?

Shahidi: Majina, Miaka yake, Jinsia yake..

Wakili wa Serikali: Jinsia ukimaanisha?

Shahidi: Kama ni mwanamke au mwanaume

Jaji: Wewe unajuaje?

Shahidi: Namkagua pia kuthibitisha

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Hali yake ya Ki afya

Wakili wa Serikali: Akikujibu wewe unafanyaje?

Shahidi: Lazima ujiridhishe kama mgongoni unaweza kumkagua

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama kwenye ukaguzi wa jinsia mnafanya kitu gani?

Shahidi: Ni kujihakikishia physically

Jaji: Ina maana mwanamke unamkagua wewe?

Wakili wa Serikali: Ndiyo nilichotaka ila niliogopa nisije kuonekana namuongoza

Shahidi: CRO panakuwa na Askari wa kike kwa Ukaguzi wa Mwanamke. Akiletwa mwanamke ukaguzi utafanywa na Askari wa Kike

Wakili wa Serikali: Tarehe 7 Mwezi wa 8 2020 Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa bado sijahamia Oysterbay nilikwa bado mkoa wa kipolisi Ilala, Central

Wakili wa Serikali: Unakumbuka nini siku hiyo?

Shahidi: Niliiingia kazini, nilikuwa na zamu ya CRO shifti

Wakili wa Serikali: Unaposema CRO shift unamaana gani?

Shahidi: Pale CRO panakuwa na Shift sababu tunafanya kazi masaa 24 kwa hiyo tunafanya kazi kwa zamu

Wakili wa Serikali: Ulipoingia kazini ulifanya nini?

Shahidi: Niliingia kazini Alfajiri na askari wengine watano

Wakili wa Serikali: Unaweza kuwataja kama unawakumbuka Shahidi: WP fatuma,Aziz na wengine

Wakili wa Serikali: Mliingia kazini Saa ngapi?

Shahidi: 12 Alfajiri

Wakili wa Serikali: Siku hiyo CRO Incharge alikuwa ni nani?

Shahidi: Palikuwa na Inspector msaidizi wa Polisi

Wakili wa Serikali: Siku hiyo wewe ulikuwa na jukumu gani

Shahidi: nilikuwa ni mtunza mahabusu, mahabusu wa kiume ni mimi, na wakike wata dili na WP SEMENI

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Jukumu la Kufungua kesi.?

Shahidi: Nakumbuka Afande Emmanuel na Afande Samuel

Wakili wa Serikali: Ulikuwa na majukumu gani

Shahidi: ilikuwa saa 12 kasoro nilifika na kupangiwa majukumu na wengine

Wakili wa Serikali: Kitu gani ulifanya

Shahidi: Baada ya kukabidhiwa mahabusu naenda kuhakiki kule mahabusu chini kwa kutaja jina mojamoja

Wakili wa Serikali: Nini Unakumbuka kikafuata?

Shahidi: Siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo baada ya kukagua mahabusu nikamuona Afande Kingai akiwa anaingia na Mahabusu

Wakili wa Serikali: Mahakama ingependa kujua ulikuwa unamfahamu kabla?

Shahidi: Ndiyo nilikuwa namfahamu

Wakili wa Serikali: alikuwa na nani?

Shahidi: Afande Jumanne

Wakili wa Serikali: ulikuwa unamfahamu Jumanne?

Shahidi: ndiyo, alikuwa makao Makuu ya polisi kabla

Wakili wa Serikali: nini kilifuata?

Shahidi: Akaniambia ni watuhumiwa kesi yao imefunguliwa hapa

Wakili wa Serikali: Unakumbuka RB yao?

Shahidi: Sikumbuli RB ila kosa nakumbuka

Wakili wa Serikali: Unakumbuka kosa gani Shahidi Kula njama za kutenda makosa ya ugaidi

Jaji: Naona tunge' break kidogo... Tutarudi saa saba na nusu kuendelea...


TUENDELEE BAADA YA BREAK FUPI


Wakili wa Serikali: Ikupemdeze Mheshimiwa jaji column yetu ya kwanza ipo vilevile tupo tayari kuendelea.

Kibatala: Tupo tayari kuendelea.

Jaji: Wakili aliyekuwa anamuongoza shahidi aendelee.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa naomba kukumbushwa na mahakama tuliishia wapi.

Jaji: Wakati wa kuandika RB na IR namba

Wakili wa Serikali: Unazikumbuka?

Shahidi: Hapana lakini zile namba CD za Central haziwezi kujirudia na kufanana

Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea hizo reference kiliendelea nini?

Shahidi: Afande kingai na Afande Jumanne walitoka

Wakili wa Serikali: Kiliendelea nini baada ya kupokea hizo reference?

Shahidi: Taratibu zingine zilifuatwa baada ya kuwa na watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Eleza mahakama nini kilifuata

Shahidi: Nilianza kumpekua mmoja mmoja, namwambia nyoosha mikono juu, kaa chini anakaa.

Wakili wa Serikali: Iambie mahakama baada ya Afande Jumanne kuwaleta watuhumiwa wakiwa na pingu nini kilifuatia kuhusu pingu?

Shahidi: Baada ya kufungua pingu kila mmoja na pingu yake, alisema akituachia pingu zitapotea

Wakili wa Serikali: Hujasema nani alifungua pingu

Shahidi: Mimi nilifungua siyo lazima nitumie pingu za afande Jumanne kwa sababu funguo za pingu zinaingiliana

Jaji: Unaposema koti unamaanisha nini?

Shahidi: Namaanisha Jacket

Jaji: Naamini wakina Kibatala mnaelewa!?

Kibatala: Ndiyo Mheshimiwa

Wakili wa Serikali: Baada ya kuwapekua nini kilifuata?

Shahidi: Nilianza kuchukua taarifa zao

Wakili wa Serikali: Kama zipi?

Shahidi: Kama Jina, Miaka, Jinsia na Dini

Wakili wa Serikali: unaweza kukumbuka majiina yake

Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Wakati huo unaandika wapi?

Shahidi: Kwenye Detention Register

Wakili wa Serikali: Ulimuuliza nini kingine?

Shahidi: Alijibu ki Afya yupo vizuri

Wakili wa Serikali: Akakuambiaje kuhusu Afya?

Shahidi: Mzima

Wakili wa Serikali: Ulijiridhishaje?

Shahidi: Tunajiridhisha kwa vitu kama majeraha, vitu kama Malaria ngumu sana

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea baada ya kujiridhisha?

Shahidi: Nikaendelea na mtuhumiwa wa pili

Wakili wa Serikali: Unakumbuka majina yake?

Shahidi: Alinitajia matatu lakini nakumbuka moja

Wakili wa Serikali: Lipi ?

Shahidi: Adam kasekwa

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo nini kilifuata?

Shahidi: nilichukua majina yake na taarifa zingine

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo?

Shahidi: watuhumiwa wote wawili niliwapeleka mahabusu

Wakili wa Serikali: Unakumbuka muda?

Shahidi: Ilikuwa saa 12 na nusu Wakili wa

Serikali: Kilifuatia nini?

Shahidi: Baada ya muda Afande Kingai alirudi tena

Wakili wa Serikali: Alisemaje?

Shahidi: Nitoleee mtuhumiwa, nikamuhoji Nimamuuliza yupi? akaniambia Adam

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo

Shahidi: Niliandika maelezo na kuandika kuwa Mtuhumiwa ametoka mahabusu, nikamwambia afande kwakuwa nimtoa huyu mtu inabidi usaini isije kuonekana ametoroka

Wakili wa Serikali: alikutaka umpelekee wapi?

Shahidi: Nilimkuta palepale Counter, akasema nimwachie aende na mtuhumiwa

Shahidi: Afande SEMENI akaniambia niongozane nae

Wakili wa Serikali: Mlienda wapi?

Shahidi: Ofisi ya RCO floor ya kwanza

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea?

Shahidi: Nilirudi kuendelea na majukumu yangu

Wakili wa Serikali: Baada ya kurudi huyo Afande kingai ikawaje?

Shahidi: Alikaa naye kama masaa mawili akamrudisha. Nilimuhoji majina yake akaniambia, nikamuhoji Jinsia yake, hali yake ya Kiafya yupo vizuri na kumpekua kuhakikisha aingii na chochote mahabusu

Wakili wa Serikali: Baada ya kujaza taarifa zake?

Shahidi: Nilimrudisha mahabusu

Wakili wa Serikali: Ukiwaona unaweza kuwakumbuka?

Shahidi: Nawakumbuka nikiwaona

Wakili wa Serikali: Kitu gani kitakufanya uwakumbuke?

Shahidi: Upekee wa siku hiyo, tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kuona Magaidi, ikabidi niwaangalie vizuri.

Wakili wa Serikali: Hapa mahakamani unaweza kuwatambua?

Shahidi: Ndiyo nikiwaona naweza kuwatambua.

Wakili wa Serikali: Kwa idhini ya mahakama unaweza kwenda kuwagusa na kuwatambua?

Jaji: Nenda sasa au UNAWAOGOPA?

Shahidi: Hapana naweza kwenda.

Shahidi: Ni hawa wawili

Wakili wa Serikali: Unaweza kusema huyu ni nani na huyu ni nani?

Shahidi: Labda wavue barakoa.

Jaji: Sasa Barakoa ni kifaa cha mtu cha Afya, sioni shida kama amewagusa wawili otherwise awaguse na kuwataja majina.

Wakili wa Serikali: Mahakama Imeonyesha kuwavua kifaa cha Afya si sawa, tuendelee

Jaji: Mimi kama mimi nimeelewa watu aliofanya nao kazi siyo Mshtakiwa nne wala wa kwanza

Wakili wa Serikali: Baada ya kuwapokea mtuhumiwa afande Kingai ukamrudisha mahabusu nini kingine kilitokea?

Shahidi: hakuna kitu kingine kilichotokea, nilipopeleka chakula cha mchana nilimuona Wakili wa Serikali: Huyu ulimpelekea chakula kutoka wapi? Shahidi: Kuna vyakula vya mahabusu na vingine kutola kwa ndugu zao Wakili wa Serikali: mimi nauliza specific kwa huyu wa Kingai

Shahidi: chakula cha mahabusu Jaji: ulipeleka chakula saa ngapi? Shahidi: saa nane na nusu Jaji: uliposema ulimuona mara ya mwisho wakati wa chakula unamaana gani? Shahidi: Narudia tena kuwa alipeleka chakula cha mchana na kumuona mara ya mwisho, lakini ilikuwa tayari Jioni

Jaji: Hebu rudia vizuri hapo, RELAX! Shahidi: Mchana Jukumu langu ni kupeleka chakula, Mchana tena napeleka chakula, jioni kwa wanaoingia jioni ndiyo wanapeleka chakula cha jioni Wakili wa Serikali: Unasema ikawa mara ya mwisho kuona, kwanini unasema mara yako ya mwisho?

Shahidi: baada ya kutoka siku ile, siku inayofuata sikuwakuta wakili wa Serikali: Kwanini hukuwakuta? shahidi: Kwa sababu siku inayofuata niliingia shift ya 3 Wakili wa Serikali: hiyo Detention Register ulioona mahakamani unaweza kuikumbuka? Shahidi: unajua....

Shahidi: unajuaaaa..... Jaji: Shahidi jibu swali unaweza kuikumbuka au lah Shahidi: naweza Kuikumbuka Wakili wa Serikali: kitu gani kitakufanya ukumbuke? Shahidi: ni taarifa ya pale juu ya kitabu Imeandikwa Detention Register na Ministry of Home Affair,tuliandika kwa Makapeni

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu shika hiki kitu, ukipata wasaa kiangalie.. Shahidi: anakikagua na kuanza kufungua ndani Shahidi: Tayari Wakili wa Serikali: umekitambua Shahidi'Ndiyo Wakili wa Serikali: kwa kuona nini? Shahidi: kuona mwandiko wangu

Wakili wa Serikali: kwa nje imeandikwa nini? Shahidi: Ministry of Home affair..... Wakili wa Serikali: Muonyeshe Jaji kwa kunyanyua... Shahidi: Mheshimiwa hii ndiyo DR na mbele inaandikwa kwa mwaka fulani....

Jaji: Wewe elezea yanayokuhusu tu, sababu mwanzo hukuongelea mambo ya DR ukasema huyakumbuki.. Shahidi: Ndiyo Mheshimiwa wakili wa Serikali: Unataka mahakama ifanye nini kuhusu kitabu hiko? Shahidi: naomba mahakama ikubali kukitumia kama kielelezo.

Jaji: Sasa mawakili wa serikali mnataka nini? Wakili wa Serikali: tunaomba kiiingie kama kielelezo cha ushahidi Jaji: Mawakili wa Utetezi? Wakili Mtobesya: kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza sina kipingamizi Wakili Kihwelo: kwa naiaba ya mshtakiwa wa pili sina kipingamizi

Wakili John Mallya: kwa niaba ya mshtakiwa watatu sina kipingamizi Wakili Peter Kibatala: Kwa niaba ya mshtakiwa wa nne sina kipingamizi.. Jaji: sawa Jaji: Detention Register imepokelewa kama kielelezo namba 1 kwa upande wa Jamhuri kwenye kesi ndogo..

Wakili wa Serikali: Kama wataitumia naomba watumie page husika Jaji: Upande wa utetezi Mawakili wote wa utetezi hawana pingamizi.. Wakili wa Serikali: Kama kuna Jambo lolote ungependa kulielezea shahidi, karibu

shahidi: mtuhumiwa wa kwanza kumpokea alikuwa na entry namba 392 lakini RB yake ni CD/RB 3093/2020 Mohammed Abdilahi Ling'wemya kosa lilikuwa kula njama za kutenda makosa ya ugaidi IR ni CD/IR 2097/2020

aliingia tarehe 07.8.2020 Saa 12 na dakika 7 asubuhi na baadae ni saa 2 na dakika 10 aliyemtoa nje ni ASP Jumanne... Sababu za kumtoa nje ni upelelezi..

Shahidi:Mtuhumiwa wa pili Entry namba 393 na Column ya report Book palikuwa na CD/RB 3093/202 Majina ni Adam kasekwa IR /CD/ IR 2097/2020. Aliingia tarehe 07.8.2020 aliingia Saa 12 na dakika 9 na siku anatoka alitolewa na ASP KINGAI. nikawapokea tena watuhumiwa..

Shahidi: mtuhumiwa wa kwanza alikuwa Adam Kasekwa akiwa RB /CD/RB/ 3093/2020 Miaka yake aliniambia ni ileile 31 Condition ni Good na IR no CD/IR/2097/2020 nilimpokea Saa 3 dakika 5, anaitwa Adam Hassan Kasekwa, na baadae anaonekana alitolewa 08.8.2020 na alitolewa saa 4 na dakika 5 asubuhi, Mtu aliyemtoa anaitwa Inspector Mahita, sababu za kumtoa ni nje kwa upelelezi..

Shahidi: Mtuhumiwa mwingine nilimpokea tarehe hiyo hiyo Mohammed Abdilah CD Ling'wenya, Miaka 34 na jinsia ni mwanaume na Physical Condition aliniambia yupo Good IR /CD/2097/2020. mtu huyu tarehe 08.8.2020 Saa 4 na dakika 5 alitolewa nje na aliyemtoa ni Inspector Mahita na Sababu za kumtoa ni nje kwa Upelelezi. Jaji: sawa mawakili wa serikali
Kumbe watuhumiwa wote walikuwa in good condition Sasa kelele za kuteswa vya mawakili vilaza kina kiba-tala wanavitoa wapi?

USSR
 
Acha kujivika ngozi ya kondoo wewe chui!

Kuna haja gani ya kutumia neno la MUNGU ukijuwa fika upo upande wa dhulma?

Wewe na mwenzio Yehodaya mkiachana na uchumia tumbo ni wanawake mnaooneka mpo fresh tu upstair lakini njaa zinawatia aibu!
Ingekuwa heri wangeenda kudanga kuliko kudhurumu haki za watu.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Jaji: Wewe elezea yanayokuhusu tu, sababu mwanzo hukuongelea mambo ya DR ukasema huyakumbuki..

ha ha ha, shahidi kapata kidonge chake kujifanya mjuajiiii
Hapo unaona umeshinda kesi

USSR
 
Back
Top Bottom