Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Tayari baadhi ya Wadau wa Maendeleo, akiwemo Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada wamewasili Mahakamani.


Hadi saa 3:30 asubuhi hii Watuhumiwa walikuwa bado hawajaletwa Mahakamani.

====

Hatimaye Mbowe na wenzake wameletwa Mahakamani

Jaji Joachim Tiganga ameingia Mahakamani

Wakili wa serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
6. Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo Lake
1. Peter kibatala
2. Jeremiah Mtobesya
3. Michael Mwangasa
4. Nashon Nkungu
5. Dickson Matata
6. Alex Massaba
7. Jonathan Mndeme
8. Hadija Aron 9.
Idd Msawanga

Jaji anaomba Kuwaona Washitakiwa wote 1,2,3 na 4

Wanainuka Kwa kutajwa kwa Namba

Wakili wa Serikali anaomba kesi Kuendelea na Shahidi yupo tayari Lakini Kabla ya Kuendelea anaomba kufuatilia kuhusiana mabadiriko yaliyopalekea mpaka Mheshimiwa Jaji Kuja mwingine kwa mujibu ya kifungu cha 299 CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai).

JAJI: Upande wa utetezi

Peter Kibatala: hatotatumia Haki ya kumuita tena Shahidi kwa kesi Inayoendelea hapa.

Jaji anaandika.

JAJI: wote mnafahamu na mlikwepo siku ya tarehe 20 mwezi huu na Jaji aliyekuwepo alielekeza Jaji Mwingine atakuja kuendelea na Kesi hii, Na Jaji Mwingine Ndiyo Mimi, kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 Kifungu cha 299.

JAJI: Kwamba Upande wa Utetezi Mnahaki ya a Kumuita tena shahidi kwa kuwa Mmesema hamna nia nitawaruhusu Upande wa Jamhuri Kumuita sasa Shahidi wao tuweze Kuendelea. Mawakili wote Wanainuka ishara ya Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji na Kupokea Maelekezo ya Mahakama.

Wakili wa Serikali anatoka Kwenda Kumuita Shahidi wa leo.

Mahakama ipo Kimya

ACP KINGAI anaingia na Kupanda Kizimbani.

Robert Kidando Wakili wa Serikali anamtaarifu Jaji Kuwa Shahidi amefika.

JAJI: Majina yako Tafadhali

SHAHIDI: ACP Ramadhan Kingai

JAJI: Unakumbuka Uliwahi Kufika Mahakamani, ukaapishwa kutoa Ushahidi, Mahakama inakukumbusha Upo chini ya Kiapo hicho. SHAHIDI: sawa Mheshimiwa

JAJI: Mtakumbuka Mawakili kuwa Siku ya Tarehe 20 Jaji alipokea Kielelezo, baada ya Kupokelewa Kinatakiwa Kusomwa Mahakamani. Naomba Kuanzia hapo Shahidi akabidhiwe Kielelezo aweze Kusoma Kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Soma Sasa Kielelezo Kuanzia kurasa ya kwanza.

SHAHIDI: Adama Kasekwa anaishi Chalinze Maelezo ya Onyo Chini kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20. MIMI kingai nakuonya wewe Adam Kasekwa

SHAHIDI: Ulazimishwi kusema lolote Pia unaweza Kualika Ndugu, Jamaa au Mwanasheria Kushuhudia utoajo wako Maelezo. Mtuhumiwa akasaini na Mimi nikasaini.

MAJIBU YA ONYO

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo..

MIMI Adam Kasekwa anaonya na Kingai Chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai Silazimishwi na yoyote Kutoa Maelezo yangu. Je, Upo tayari Kutoa Maelezo Yako.

Jibu, Ndiyo Nipo tayari.

Shahidi anasoma kielelezo: Maelezo yamechukuliwa Katika Ofisi ya RCO ilala MIMI Adam Kasekwa Nimezaliwa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Ileje... Mwaka 2011 nilijiunga na Recruting Maktopora. Nikachaguliwa Kujiung na Mafunzo Ukomando 92KJ.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Mwaka 2014 niliteukiwa kwenda kituo cha Msangani Kujifunza ulinzi, amani na nikachaguliwa Kwenda DR Congo. Mwaka 2017 nilimaliza Mkataba na kurejea Nilipata malipo na Kumuoa Mke wangu Lilian ambaye naishi naye Mpaka Leo.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Nimepata naye Mtoto Mmoja. Nilirudi nikaa Miezi 6 kazini Nikaugua Ugonjwa wa aKili Nikaachishwa kazi na kulipwa mafao ya Millioni 4 na Laki 6.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Je unamfahamu Luteni Denis? Ndiyo, nilikuwa Mkinga Mawasiliano hayapatikani. Niliporudi nikaambiwa mwenzangu ananitafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Niliporudi nyumbani nilimpigia Simu Mwenzangu Mohammed Ling'wenya Kwamba Kuna kazi ya VIP protection. Akaniambia inabidi twende Morogoro Kumuona Luteni Urio. Tulipoenda akatuambia Kuna kazi ya VIP protection ya kumlinda Freeman Mbowe

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatupatia TSh 21,000 nauli ya Kwenda Moshi. Siku hiyo hiyo tulirudi Chalinze na kuanza Safari ya kwenda Moshi Tulipokelewa na Dereva wake anayeitwa Willy Alitupokea na Pick Up Nyeupe yenye maandishi ya M4C.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tukaenda Mpaka Kwenye Hotel Ya Mheshimiwa Mbowe Huko tulimkuta Khalfani Bwire aliyetutambulisha kwa Mbowe, "Mkuu wale Vijana tuliowaagiza ndiyo hawa hapa." MBOWE akatueleza Kuwa Sabaya anamvuruga sana na anamvuruga wapiga Kura.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba anawatisha Wapiga kura wake kiasi cha Kuhatarisha Kurudi kwake. Na kwamba, akatuelekeza tumdhuru Kwa Njia yoyote. Akatuelekeza Maeneo yake ya Moshi na Arusha.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tulipanga kumdhuru kwa Spray Spray ya sumu alitafuta Mohammed Ling'wenya

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Siku inayofuata tulikuwa Mimi na Mohammed na wanachana wawili siwakumbuki Majina Baada ya Kufika Dar es Salaam Tulimfikisha Mheshimiwa Mbowe Nyumbani

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatukabidhi TSh Laki 2 kwaaajili ya Kununua Nguo. Kwa sababu Kesho yake tulikuwa tunampokea Mheshimiwa Lissu. Na Siku ya tarehe 27 Julai Mbowe alitutumia Kila moja TSh 78 Elfu ya Nauli Ya Kwenda Moshi.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: SIKU ya Tarehe 01 August Tulienda Moshi Tukamkuta Mbowe akiwa na Khalfani Bwire Akatuelekeza Kuwa tufanye ile kazi yake Haraka Akatuelekeza Maeneo anayokaa Sabaya kama vile Milestone PIA Akatuelekeza Tuje DSM, Kuchoma Vituo Vya Mafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba yeye anatachochea maandamano ILi Serikali ionekane Imeshindwa Kuandaa Uchaguzi. Tulienda Maeneo ya Boma Ng'ombe Njia ya kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumfuatilia.

Siku ya terehe 03 tulienda Maeneo ya RAU madukani kwa ajili ya kubana Matumizi. Kwa sababu Mheshimiwa alituachia Pesa Laki Moja na Nusu kwa ajili ya kukaa, isingetosha. Tulienda Kukaa kwa Dada yake kukaa kwaajili ya Kubana Matumizi.

Swala la Kupanga Ugaidi ni la kweli Na swala la a kukutwa na Silaha ni la kweli Wakati Polisi wananikamata pia walinikuta na Heroine Baada ya kuchukua Vitu hivyo Askari walisaini na Mimi nikasaini na Polisi walichukua Vitu hivyo kwenda Central

Baada ya Maelezo hayo Adam Kasekwa akasaini Na Mimi Kingai nikasaini Baada ya Kuchukua Maelezo hayo Muda ulikuwa ni saaa tatu.

Wakili wa Serikali: ACP Kingai Kutokana na Maelezo uliyoyasoma hapa mahakamani Yeye alikuelza nini Kutokana na Maelezo Uliyoyasoma Mahakamani Shahidi: alikiri kuwa anamfahamu Luteni Urio. Alikiri Kupewa Maelekezo ya kazi kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Alikiri Pia alipewa Maelekezo ya kazi Kutoka akwa Mbowe Kupitia Kwa Luteni Deni Urio. Alikiri Pia kuwapo Moshi tarehe 24 Mwezi wa 07, 2020

Shahidi: Alikiri Pia kuwapo Moshi na wenzake Mohammed Ling'wenya na Mwenzake aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe. Baada ya Ufutailiaji tukamfahamu ni Moses Lijenje. Alikiri Pia kufanya Mkutano yeye na wenzake wanne.

Yeye Mwenyewe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya, Moses Lijenje (Aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe) Khalfani Bwire na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Mkutano huo nini kiliendelea. Shahidi: Mbowe alitoa Maelezo kuwa Sabaya anamfanyia Vurugu, (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai)

Wakili wa Serikali: kitu gani Kingine alikueleza Shahidi: Mtuhumiwa alikiri Kupewa Pesa 150,000/= kukidhi Mahitaji kipindi watakapokuwa hapo Moshi.

Wakili wa Serikali: tueleze Shahidi kuhusiana na kilichofuata Shahidi: Alikiri Kuwa Siku ya Tarehe 01 Mwezi wa Nane saa 11 Alfajiri kabla ya Safari ya Kuja DAR ES SALAAM Aliwaelekeza wamdhuru Ole Sabaya.

Shahidi: Akawaonyesha Picha ya Ole Sabaya Kupitia Simu yake ya mkononi Aliwapa Maelekezo Kufanya kazi hiyo na Kwamba baada ya hapo atawataka warudi Dar es Salaam. Alipanga kuwapa kazi ya kwenda Kulipua Vituo Vya Mafuta. Alipanga kufanya Vurugu kwenye masoko.

Mtobesya: OBJECTION Naomba Shahidi ajielekeze Kwenye kikichoandikwa kwenye Statement Mambo ya Kituo cha Mafuta na Masoko havijatajwa.

Jaji: Kwahiyo a some?

Mtobesya: ajielekeze kikichoandikwa hata kama ana Rudia Kuelezea, Sheria inasema Statement itajielezea Yenyewe.

JAJI: Upande wa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Sahihi Mheshimiwa tutarekebisha.

Wakili wa Serikali: Alikueleza Lengo ilikuwa ni nini

Shahidi: Lengo ni Serikal ionekane imefeli Alikiri Pia kukamatwa na Polisi Siku ya tarehe 05 Mwezi wa 08, 2020 akiwa Rau Madukani.

Alikiri Pia kukamatwa na Pistol aina ya Ruvern ikiwa na Risasi 03.

Shahidi ACP KINGAI: Alikiri kukamatwa na Kete 58 za Madawa aina ya Heroine.

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa umeandika Maelezo hayo, yeye ulimpeleka wapi kwa Siku hiyo.

Shahidi ACP KINGAI: ilikuwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08, 2020 nilimrudisha Mahabusu.

Wakili wa Serikali: Shughuli gani Nyingine ili endelea baada ya Shughuli hii

Shahidi ACP KINGAI: tuliendelea na Upelelezi ya Kuwatafuta watuhumiwa wengine. Maeneo ya Chang'ombe tulimkamata Khalfani Bwire.

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma Gani

Shahidi ACP KINGAI: Kwa tuhuma hizi hizi za Kula Njama kutenda Matendo ya Ugaidi.

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea

Shahidi ACP KINGAI: nikimtaka Khalfani Bwire aandike Maelezo yake

Wakili wa Serikali: elezea Kuhusu Kumkamata kwake

Shahidi ACP KINGAI: baada ya a kuwasiliana na Askari aliyekuwa kwenye Pointi akiwa kwenye gari, tukielekeza Gari iingie Kituo cha polisi Chang'ombe. Tukawa tumeingia pale na Inspector Mahita na ASP Jumamne.

Jaji: ASP nani? Shahidi: Jumanne

Wakili wa Serikali: baada ya Kumkamata Mlimpeleka wapi

Shahidi: tuliekeza Superitendent Lukangira wa hapo hapo Chang'ombe. Hii ni baada ya Mtuhumiwa kutuelekeza hana Makazi hapa Dar es Salaam ni Mkazi wa Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Nia ya Kuuliza kwake ni wapi ilikuwa ni ya nini

Shahidi: nia ilikuwa kufanikisha Shughuli za kiupepelezi

Wakili wa Serikali: baada ya Lukagingira kuandika Maelezo yake nini Kilifuata

Shahidi: Tukawa tunaendelea Kufuatilia Makazi yake, Tofauti na Taarifa alivyokuwa ametoa yeye kwakuwa tulijua haiwezekani awe kila Siku anaenda Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Wakati Unapata Taarifa ana makazi Wilaya ya Temeke, elezea Sasa Maelezo yalikuwa yanaandikiwa wapi

Shahidi: Maelezo yalikuwa yanachukuliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe na Mimi niliweka Bass Central polisi (Ilala).

Wakili wa Serikali: baada ya Kutoa Maelekezo Hatua Kuchukua Maelezo Isimame, nini kilifuata

Shahidi: tulipata Taarifa Mtuhumiwa anakaa Temeke Makangarawe, Tuliungana na Detective John wa Temeke na RCO kwa ajili ya kwenda Kumpekua Makazi yake.

Wakili wa Serikali: Mlienda sehemu ipi haswa huko Mkangarawe

Shahidi: Ule Mtaa Jina Limenitoka

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kuutambua sasa

Shahidi: tukielekezwa na Watu hadi Nyumba alipokuwa amepanga Mtuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa hiyo Shughuli ilifanyikaje na Khalfani Bwire alikuwa wapi.

Shahidi: Tuliongozana na Mtuhumiwa, Tukamtafuta Mwenyekiti wa Ule mtaa, Tukamkuta na Mwenye nyumba aliyempangisha Khalfani Bwire na hata Mke wake alikwepo.

Wakili wa Serikali: huyu Mwenyekiti ni wanini?

Shahidi: Ni Mwenyekiti wa Mtaa

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Nilimuelekeza ASP Jumanne Kwa Kushirikiana na Detective John Kutoka Ofisi ya RCO Temeke na kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa na hata Mke wake.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa Katika Upekuzi huo Mlikuta nini?

Shahidi: Vitu mbalimbali vilipatikana kama Uniforms za JWTZ, Masharti ya JWTZ, Tshirt za JWZT, name tags za kwake za JWTZ.

Wakili wa Serikali: baada ya Kupata Uniforms na Vifaa Mbalimbali nini Kilifanyika baada ya Kupata Vitu hivyo.

Shahidi: Viliorodheshwa katika Hati ya Uchukuaji Mali. Wakati wa Upekuzi tulikuta Kidaftari kilichokuwa na Ramani na Majina ya Vituo Vya Mafuta.

Wakili wa Serikali: baada ya kuorodhesha kitu gani kilifanyika

Shahidi: baada ya Kuwa Viliorodheshwa yaliandikwa Majina ya walioshuhudia Upekuzi huo. Pia wakasaini Hati ya Uchukuaji Mali. Mtuhumiwa pia alisaini Hati ya Uchukuaji Mali na aliyepekua alisaini Hati hiyo.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Hati ya Uchukuaji Mali, Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Nilikuwa nimeelekeza Mashahidi walioshuhudia waandikwe Maelezo pale pale

Wakili wa Serikali: baada ya Kukamilisha

Shahidi: Tulichukua Vitu tulivyo orodhesha na Mtuhumiwa akarudishwa a kituo Cha Polisi.

Wakili wa Serikali: Kituo gani cha Polisi Shahidi: Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Baada ya kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe Kitu gani pia Kiliendelea.

Shahidi: Mtuhumiwa tulimkamata na Kidaftari chenye Ramani ya Vituo Vya Mafuta Dar es salaam, Soko la Kilombero Arusha.

Tukachukua Sampuli za Miandiko ya Watuhumiwa wote. Lakini pia tuliendelea na hatua ya kuwatafuta watuhumiwa wengine

Wakili wa Serikali: watuhumiwa gani wengine Mlikuwa mnawatafuta

Shahidi: Watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawafutilia ni Mtu alikuwa anaitwa Gabriel, Lijenje, Malima, Khalid na Jamaa Mmoja anaitwa Kaaya.

Wakili wa Serikali: nini hatima ya hao mliokuwa mnawafuatilia

Shahidi: Ukimuondoa Mtu Mmoja anaitwa Malima, Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani.

Wakili wa Serikali: vipi kuhusu moses Lijenje Shahidi: bado hatujafanikiwa Kumpata

Wakili wa Serikali: Hapa Mahakamani kuna Washitakiwa Wanne inakuwa je hao wengine hawapo Mahakamani kama Walifumgukiwa Mashitaka

Shahidi: walifutiwa Mashitaka baada ya Kuonekana Ushahidi hakuwa wakutosha ukilinganisha na wenzao.

Wakili wa Serikali: ACP kingai katika Ushahidi wako tangu Mwanzoni umezungumzia kukamatwa Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Bwire Vipi ukamatwaji wake Mshitakiwa wa Nne.

Shahidi: Freeman Mbowe alikamatwa 21 July 2020 akiwa Mwanza

Shukrani kwa taarifa mkuu
 
Labda kama wewe ni mgeni na siasa za Tanzania, na poliCCM. Haya maelezo sio mapya hata CUF wakati wanaisumbua CCM , walipewa kesi ya UGAIDI na poliCCM wakaonyesha mapanga yamefungwa bendera za CUF. hakuna jipya hapo kwa sisi wazamani.
CCM wamashakwama na mbinu zile zile .
Dont panick, mchezo hautaki hasira huu! Kesi bado mbichi sana, kuna ushahidi wa mawasiliano na transactions huko mbele...Tuendelee kufuatilia!
 
Dont panick, mchezo hautaki hasira huu! Kesi bado mbichi sana, kuna ushahidi wa mawasiliano na transactions huko mbele...Tuendelee kufuatilia!
Siwezi kupanic kwa hii kesi ya uongo, hamna kesi hapo, kama lengo ni kumfunga Mbowe ili CHADEMA ifutwe wafanye tu. na kwa umri nilionao na siasa za Tanzania na poliCCM hao.

Kwangu sio mageni haya . Au kupanick ni vile nakuelezea usioyajua.
 
Sema wafadhili wa chanjo ya corona
KWA USHAHIDI ANAOTOA HAPO WATUHUMIWA BOR TU WASEME WAFUNGWE TU MAANA WANAISUMBUA TU MAHAKAMA WAKATOI WALITENDA MAKOSA KWELI YAANI HUWEZIKUAMINI KAMA MBOWE NI MTUHATARI NAMNA HIYO WALIWALISHA MANENOWAJE WAFUNGUE KESI NDOGO WAJILALAMISHE WAMETESWA KUMBE JANJA YAO TU
 
Siwezi kupanic kwa hii kesi ya uongo, na umri nilionao na siasa za Tanzania na poliCCM hao.
Kwangu sio mageni haya . Au kupanick ni vile nakuelezea usioyajua.
AISEE MBOWE GAIDI KWELI NILIKUWAGA SIAMINI HUYU NI GAIDI WENZAKE WAMEANIKA YOTEE ATAKWEPA WAPI MBOWE ANANYONGWATAFUTENI MWENYEKITI MWINGINE TU HAINA JINSI
 
Shahidi: Mtuhumiwa tulimkamata na Kidaftari chenye Ramani ya Vituo Vya Mafuta Dar es salaam, Soko la Kilombero Arusha.
Ha ha ha ha

Jamani kweli dunia hadaa.... !! Kigai we ni noma
 
AISEE MBOWE GAIDI KWELI NILIKUWAGA SIAMINI HUYU NI GAIDI WENZAKE WAMEANIKA YOTEE ATAKWEPA WAPI MBOWE ANANYONGWATAFUTENI MWENYEKITI MWINGINE TU HAINA JINSI
Akili yako haina akili.
Hivi wale MAGAIDI wa CUF wapo jela gani, maana poliCCM walituonyesha mapanga yaliofungwa na bendera za CUF.
Acha kutuona wote humu tumezaliwa jana kama wewe.
 
Akili yako haina akili.
Hivi wale MAGAIDI wa CUF wapo jela gani, maana poliCCM walituonyesha mapanga yaliofungwa na bendera CUF.
Acha kutuona wote humu tumezaliwa jana kama wewe.
YAANI NDUGU HNAHAJA YA KUPANIC MAELEZO MBONA YANAJIELEZA MBOWE NI MTU HATARI SANA HIVI WEWE HUJIULIZI KWANINI KABLA MBOWE HAJAKAMATWA ALIKUWA HAFUATILII KESI YA HAO JAMAA YAANI ALIKUWA KAWATELEKEZA SASA WAMESEMA UKWELI HATA KAMA NI SHABIKI WA MBOWE KUBALI MATOKEO MBOWE GAIDI UKIBISHA UNAONEKANA HUNA AKILI HATA YA KUVUKIA BARABARA
 
Siwezi kupanic kwa hii kesi ya uongo, hamna kesi hapo, kama lengo ni kumfunga Mbowe ili CHADEMA ifutwe wafanye tu. na kwa umri nilionao na siasa za Tanzania na poliCCM hao.
Kwangu sio mageni haya . Au kupanick ni vile nakuelezea usioyajua.
Nayajua mengi mnoo kuliko wewe, hamna chochote unaweza kunielezea
 
KWA USHAHIDI ANAOTOA HAPO WATUHUMIWA BOR TU WASEME WAFUNGWE TU MAANA WANAISUMBUA TU MAHAKAMA WAKATOI WALITENDA MAKOSA KWELI YAANI HUWEZIKUAMINI KAMA MBOWE NI MTUHATARI NAMNA HIYO WALIWALISHA MANENOWAJE WAFUNGUE KESI NDOGO WAJILALAMISHE WAMETESWA KUMBE JANJA YAO TU
Haa haa just haa haaa eti ushaidi yaani yaani kesi feki iandikwe na Sabaya na Kingai Hai , yapewe baraka na Magufuli ili kuifuta CHADEMA, mnaning’niza watu kama mshikaki na kuwaminya makende ili wasaini ,ndio mnaita mmechukua maelezo ya watuhumiwa?!
MaCCM mmekwama sana.
 
Nayajua mengi mnoo kuliko wewe, hamna chochote unaweza kunielezea
Kaa kwa kutulia si mnataka ushabiki wa kisiasa twende tu😄😃😄😃
Mnaotaka kutufunga na kutufutia CHADEMA yetu tumetulia. Nyie tu wakati wenu huu.
 
Wazee wa "PGO" leo ni aibu kwao, maelezo ya komando yapo straight, no chenga chenga, wakishuka na watu wa mawasiliano na transactions itakuwa balaa zaidi! Kumuepusha na aibu hii Mkiti ni vyema hii kesi sasa ifanyike kwa usiri, kama zile za ubakaji wa watoto..
 
Haa just haaa eti ushaidi yaani yaani kesi feki iandikwe na Sabaya na Kingai Hai yapewe baraka na Magufuli ili kuifuta CHADEMA, mnaning’niza watu kama mshikaki na kuwaminya makende ili wasalimie,ndio mnaita mmechukua maelezo ya watuhumia?!
MaCCM mmekwama sana.
Yaani unapoteza mudakwa hizo hasirazako hapo hakuna aliyelazimishwa wale walishatoswa na mbowe wakaamua kuusema ukweli kwa maelezo yao polisi baadae mkawalisha maneno waseme waliteswa ndipo kibatala wakili njaa akafungua kesi ndogo ambayo nayo imekama maana ni janja janja tu ili kuwanasua na uhalifuwao unajisumbua tu najuwa unaakili ila kama huna akili endelea kubisha mwisho wa siku nimiaka mingi sana jela wacha tuka mlisi mkewake maana alitaka kuangamiza taifa
 
Wazee wa "PGO" leo ni aibu kwao, maelezo ya komando yapo straight, no chenga chenga, wakishuka na watu wa mawasiliano na transactions itakuwa balaa zaidi! Kumuepusha na aibu hii Mkiti ni vyema hii kesi sasa ifanyike kwa usiri, kama zile za ubakaji wa watoto..
Kabisa mkuu yaani jamaa alieleza straight hakuna chenga onampaka mashahidi wa ukamataji upekuzi mwenyekiti wa mtaa walishuhudia unakwepaje hapo sasa uje useme uliteswa ili useme yaani kibatala kwaakili yake ndogo aliwalisha maneno wadanganye mahakama wakafeli sasaushahidi mwaaaaaaaaaaaaaa gaid jela
 
Back
Top Bottom