Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Usiamini wanasiasa. Hata Museven na Kagame waliwahi tangaza mara kibao kuwa ni misimu yao mwisho.
Siwaamini 100% Ila Hilo wamelisisitiza mno
Siwezi kuwafananisha na Museven na Kagame Sababu siasa za Tanzania Ni tofauti, hao waliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na katika Historia ya nchi yao hakuna kiongozi aliyeachia madaraka kwa njia za kawaida, Ni kitu Kigeni kwao

Tofauti na Tz ambalo imezoeleka na Magufuli akirefusha Basi ndio atakuwa amevunja mwiko, na kuweka precedence mbaya, na hili linaweza kukigawa chama

Sisemi kuwa Haiwezekani Ila Ni ngumu Sana
 
Kawe Halima hatoboi, kule Ndanda kwa Cecil Chadema kama kuna mtu mwenye ushawishi jimbo wanalichukua mapema tu..

Arusha ngoma nzito.. Lema anapendwa na vijana wa kiume ila Gambo wamama na wasichana wanamkubali sana..
Amini nakwambia, Gwajima Kawe hatoboi. Kawe sio watu wa kumpapalikia mtu. Ni jimbo la wasomi wengi sana na watu wenye uwezo wa kifedha. Gwajima na mascandal yake Kawe hawezi toboa
 
Waooooo!!! Wapi mwenye digrii nne?? Wajumbe bwana. Mtu wa darasa la saba ata bishanaje na mwenye digrii nne??
 
Yani hawa watu wajiandae kutafuta kura za mawe tu.
1. David Silinde
2. Pauline Gekul
3. Salvatory Makundi
4. Cecil Mwambe
5. Pateobas Katambi

Save my content!
Wanapita bila shida, katambi anamaliza mchezo mapema pale shy town.Masele alikuwa mzigo sana na mtu wa kujisikia sana
 
Wadau:
Huko mkoa wa Mara vipi huyo aliyekuwa Waziri Mkata viuno?
 
Acha udini wewe
Gwajima kuna kipindi aliikashifu iman ya Kislam na ushahidi wa video upo,pili lile pilau lake kule kwenye site za UTAMU alilo lipika na kondoo wake,linatosha kummaliza.

Kwa kifupi historia yake ina mkaanga mwenyewe,ndio maana sometimes kama una plan za kuwa kiongozi kuwa makini na kauli pamoja na matendo yako.

Kwani ipo siku watu wata kuhukumu kwa kauli na matendo yako ya nyuma.


KAWE mbunge ni MDEE,itunze comment hii.
 
Kama hawana mvuto mbona mmeingia mchecheto ghafla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…