Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Screenshot_20200820-155016.png
 
Kule
Habari za mchana,.
Ni matumaini haisha yanaendelea hapo mlipo lakini kiukweli polen sana sana mlipambana kupata na kupitisha mliodhani ni watu sahihi kipeperusha bendera ya Ccm!!! Lakini ccm imethibitisha ina wenyewe nyie ni makambale tuuu hamna jipya na mlipoteza muda tuuu!!!!
Poleni na mchana mwema
Jimbo la busanda mkoani Geita,Kurwa Biteko ametendewa haki. Aligawa fedha kama njugu. Huyu kijana ni pacha na Doto biteko waziri wa madini. Mungu anamuona.
 
Kwanza kabisa aliyeteuliwa ndiye aliyeshika namba moja kwenye kura ya maoni. Kwa desturi wa wana Rorya sidhani kama CCM watashinda kwenye uchaguzi ujao kwenye Jimbo hili.. Haya ni maoni yangu. Tunajuta sana ni kwa nini Lakairo hakutia nia licha ya kuchukua fomu na kuirudisha kwa hasira na kutangaza kuwa sasa hatagombea tena. Kwa mawazo yangu tayari Jimbo limekwenda upinzani. Time will tell.
Wana Rorya wajue hawaikomoi CCM, wanajiweka mwisho wa mstari kwenye miradi ya maendeleo. Kupanga ni kuchagua.
 
Gambo mbona kapita Arusha pamoja na Rushwa.

Lowassa Jr. Kapita

Kitila Kibamba

Kawe Gwajima

Kigamboni Ndungiulile
Arusha gambo wangemtoa lile jimbo wangempa ushindi mkubwa lema ccm karata ya kumpa gambo pale wamecheza sana yule ndie anaeweza pambana na lema
 
Kwanza kabisa aliyeteuliwa ndiye aliyeshika namba moja kwenye kura ya maoni. Kwa desturi wa wana Rorya sidhani kama CCM watashinda kwenye uchaguzi ujao kwenye Jimbo hili.. Haya ni maoni yangu. Tunajuta sana ni kwa nini Lakairo hakutia nia licha ya kuchukua fomu na kuirudisha kwa hasira na kutangaza kuwa sasa hatagombea tena. Kwa mawazo yangu tayari Jimbo limekwenda upinzani. Time will tell.
Kwani Lakairo kafanya nini cha maana hapo Rorya?
 
Baada ya kikao cha halmashauri kuu kuketi asubuhi, Katibu mkuu mwenezi wa CCM anaongelea yaliyojiri vikao hivyo mpaka kupata majina ya watu wanaowania ubunge kwa tiketi ya chama hicho kwenye majimbo mbalimbali nchi pia wabunge wa viti maalum.
=======

Polepole: Vikao vyote cha jana na leo vilikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM. Kikao cha halmashauri kuu kilikuwa na lengo moja na limekamilika. Lengo lilikuwa kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea wa majimbo na viti maalum. Napenda kuleta taarifa hiyo kwenu kwa maana hawa walioteuliwa leo kwa majimbo na viti maalum.

Walijitokeza 10,367 nafasi za majimbo 264, chama chetu kimeandika rekodi na historia ya kukubalika. Upande wa uwakilishi leo haukufanyika uteuzi kwa sababu ya muingiliano wa ratiba ya NEC. Wagombea 33,094 waliomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye udiwani ilhali nafasi zipo kama elfu nne na kitu na kufanya jumla ya watu 43,461 waliiomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye nafasi mbalimbali.

Wajumbe wa halmashauri kuu wametimiza wajibu wao na kikao kimeeleza wajibu wao wa kusimamia serikali mpaka tumefika hapa, uamuzi walioufanya leo umezingatia watu wabobevu kusimamia maslahi ya watu wetu watakaofanya kazi sambamba na serikali ya chama cha Mapinduzi ambayo tunaenda kuiombea kura.

Kwa kauli moja wajumbe wamefanya uteuzi baada ya kupokea majina kwa watakaokuwa wagombea wa CCM kwa nafasi ya ubunge. Vilikuwepo vingezo na sifa ambazo tumezitumia ikiwemo wanaCCM wanaojitoa kwa chama, tumetafuta yule ambae atatuleta pamoja, wenye mahusiano mazuri na wananchi na wanakubalika na jamii.

Watu ambao wameteuliwa leo wanatakiwa wanatakiwa wafanye maandalizi ya msingi.

Kwenye majimbo wanaCCM ni nidhamu tuendelee kuwa watulivu, wagombea ni wengi hatuwezi kupata wote lakini nawahakikishia kwamba, chama chetu ni kikubwa na fursa zake ni nyingi tuendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu, chama kina taarifa zenu.

ARUSHA
Arusha mijini- Mrisho Mashaka Gambo

Arumeru Magharibi- Noah Lebrus Molel

Arumeru Mashariki- John Palangyo

Karatu- Daniel Tlemai

Longido- Stephen Kirusya

Monduli- Fred Lowassa

Ngorongoro- Ole Nasha

DAR
Ubungo- Prof Kitila Kitila

Kibamba- Issa Jumanne Mtemvu

Kinondoni- Abass Tarimba

Kawe- Askofu Josephat Gwajima

Kigamboni- Dr. Faustine Ndugulile

Ilala- Mussa Zungu

Segerea- Bonna Kamoli

Ukonga- Jerry Slaa

Temeke- Doroth Kilave

Mbagala- Abdallah Chaurembo

DODOMA
Bahi- Keneth Nolo

Chamwino- Deo Dejembi

Mvumi- Livingstone Lusinde

Chemba- Mohammed Moni

Dodoma Mjini- Anthony Mavunde

Kongwa- Job Ndugai

Kondoa mji- Ally Juma Makoa

Kondoa Vijijini- Dr. Ashatu Kijaji

Kibakwe- George Simbachawene

Mpwapwa- George Nataly Malima

GEITA
Busanda- Tumaini Magesa

Geita Mjini- Consatantine Kanyasu

Geita vijijini- Joseph Kasheku(Musukuma)

Bukombe- Dotto Bisheko

Chato- Medard Kalemani

Mbogwe- Nicodemas Maganga

Nyang'alwe- Hussein Amar

IRINGA
Iringa Mjini- Jesca Msavatambangu

Kalenga- Jackson Kiswaga

Isimani- William Lukuvi

Kilolo- Lazaro Nyamoga

Mafinga mji- Cosato Chumi

Mufindi Kaskazini- Exaud Kigahe

Mufindi Kusini- David Kihenzile

KAGERA
Bukoba mjini- Stephen Byabato

Bukoba vijijini- Jackson Rweikiza

Nkenge- Frolent Kyombo

Karagwe- Innocent Bashungwa

Kyerwa- Innocent Bilakwate

Ngara- Ndaisaba Luhoro

Bihalamuro- Ezra Chiwelesa

Muleba Kaskazini- Charls Mwijage

Muleba Kusini- Oscar Kikoyo

KATAVI
Mlele- Isack Kamwele

Kavuu- Geophrei Mizengo Pinda

Mpanda Mjini- Sebastian Kapufi

Nsimbo- Anna Lupembe

Mpanda Vijijini- Moshi Kakoso

KIGOMA
Kasuli Mjini- Prof Joyce Ndalichako

Manyovu- Dr. Philip Mpango

Buyungu- Aloyce Kamamba

Muhambwe- Atashasta Nditiye

Kigoma Mjini- Kirumbe Shabani Ng'enda

Kigoma Kaskazini- Asa Nelson Makanika

Kigoma Kusini- Nashon William

Kasulu vijijini- Augustine Hole

KILIMANJARO
Vunjo- Charls Kimei

Siha- Dr. Godwin Mollel

Moshi Vijijini- Prof. Patrick Ndakidemi

Hai- Salasisha Mafue

Same Mashariki- Anne Kilango Malecela

Same Magharibi- Dr. Mathayo David Mathayo

Rombo- Prof. Adolf Mkenda

Moshi Mjini- Priscus Tarimo

Mwanga- Anania Tadayo

LINDI
Kilwa Kaskazini- Ndulane Franscis

Kilwa Kusini- Kasinge Mohammed Ally

Liwale- Zuberi Kuchauka

Lindi Mjini- Hamida Mohammed Abdallah

Mchinga- Salma Kikwete

Mtama- Nape Nnauye

Nachingwea- Amandus Julius Chinguiye

Ruangwa- Kassim Majaliwa

MANYARA
Babati Mijini- Paulina Gekul

Babati vijijini- Daniel Silo

Hanang- Samwel Kadai

Mbulu mji- Isai Paulo

Mbulu vijijini- Flatei Gregory

Kiteto- Edward Kisau

Simanjiro- Christpher Ole Sendeka

MARA
Musoma Mjini- Vedastus Manyinyi

Musoma Vijijini- Prof. Sospeter Muhongo

Bunda Mjini- Robert Chacha Maboto

Bunda Vijijini- Boniface Getere

Mwibara- Charls Kajege

Butiama- Jumanne Sagini

Rorya- Jaffary Wambura Chege

Tarime Mjini- Mwita Michael Kembaki

Tarime Vijijini- Mwita Waitara

Serengeti- Dr. Jeresabi Mkimi

MBEYA
Busekelo- Atupele Mwakibete

Kyela- Ally Jumbe

Lupa- Masache Kasaka

Mbalali- Franscis Mtega

Mbeya Mjini- Dk. Tulia Akson

Mbeya Vijijini- Oran Njeza

Rungwe- Anthony Mwantona

MOROGORO
Mlimba- Godwin Kunambi

Kilombero- Abubakar Asenga

Morogoro mjini- AbdulAziz Abood

Gairo- Ahmed Shabiby

Malinyi- Antipas Mgungusi

Morogoro Kusini- Innocent Kalogeres

Morogoro Mashariki- Hamis Shaaban Taletale

Mvomero- Jonas Vanzilad

Mikumi- Deniss Lazaro Londo

Kilosa- Prof. Palamaganda Kabudi

Ulanga- Salim Hasham

MTWARA
Mtwara Mjini- Mtenga Hassan Selemani

Mtwara Vijijini- Hawa Ghasia

Nanyamba- Abdallah Chikota

Tandahimba- Katani Katani

Newala mjini- George Mkuchika

Newala Vijijini- Maimuna Mtanda

Masasi- Geofrey Mwambe

Lulindi- Issa Mchungahela

Ndanda- Cecil David Mwambe

Nanyumbu- Yahaya Ali Mhata

MWANZA
Ukerewe- Joseph Mkundi

Ilemela- Dkt. Angelina Mabula

Sengerema- Tabasamu Hamis Mwagao

Buchosa- Erick Shigongo James

Nyamagana- Stanslaus Mabula

Misungwi- Alexander Mnyeti

Sumve- Kasalali Emmanuel Mageni

Kwimba- Shanif Mansour

Magu- Bonaventura Kiswaga
Niangalizieni Jimbo la Meatu mkoa wa Simiyu kapita nani?
 
Tulia wewe, sisi ndio tuna dola, Mkurugenzi tunamlipa mshahara, DC tunamlipa, RC tunamlipa na mpaka NEC yakwetu...
 
Wana Rorya wajue hawaikomoi CCM, wanajiweka mwisho wa mstari kwenye miradi ya maendeleo. Kupanga ni kuchagua.
Hayo maendeleo mnayotoa kwa upendeleo kwani hizo pesa mnazitoa kwenye mifuko yenu?

Akili zenu sijui zinafanya kazi gani.
 
Wana JF sisi tuliokatwa kwa sababu ya kutotoa rushwa katika maeneo mengi tumeumia sana kuona vinara wengi wa rushwa ndo wamepenya.

Kwa kuwa nia yetu ilikuwa ni kuwatumikia watanzania tunaomba vyama vya upinzani vitupokee kwa kipindi hiki kifupi.

Kwa wale waliochukua fomu za NEC tunaomba mtuwekee hapa tuanze kuzijaza ili kama kuna makosa tuweze kuzirekebisha mapema. Lengo lingine ni kuandaa viambatanisho vinavyotakiwa kwa mfano background ya picha ya passport nk

Tumebaki na siku 5 zinatosha sana kukamilisha ujazaji wa fomu na kurudisha.

Tunaomba namba za viongozi wa upinzani kwa kila kata au jimbo ambalo vyama vya upinzani hawajateua bado wagombea wao ili sisi watia nia masikini tuweze kuonesha vipawa vyetu vya uongozi huko.

Chonde chonde msitubeze....tupendane

Wajumbe oyee
 
Wana Rorya wajue hawaikomoi CCM, wanajiweka mwisho wa mstari kwenye miradi ya maendeleo. Kupanga ni kuchagua.

dah hatari sana, futa hii mentality chief tena tupambane kama jamii iliyostaarabika hili lisiwepo kamwe..

Kodi hulipwa na Watanzania wote kwa serikali moja..
 
Back
Top Bottom