Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA, Mh Tundu Lissu Mkoani Mara, Serengeti

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA, Mh Tundu Lissu Mkoani Mara, Serengeti

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Instagram media - CFqp2jWAgwJ ( 640 X 640 ).jpg


Wakuu natanguliza salamu za ukombozi, baada ya salamu naingia moja kwa moja kwenye hoja.

Ni siku nyingine tena ambapo Mh Tundu Lissu mgombea urais anayeongoza kwenye kura za maoni anaendelea na safari yake ya kuwaomba watanzania wenzake wampe ridhaa ya kuwaongoza, leo ikiwa bado yuko Mkoani Mara kwenye jimbo la Serengeti.

Pamoja na kufanya kampeni lakini mgombea huyu anayo sifa ya ziada ya uwezo wa kuwafundisha raia kuhusu haki zao walizoporwa kwa miaka mingi, hatukani wala hafokei wapiga kura , amekuwa gumzo kubwa kwenye elimu ya uraia ambayo imesaidia wapiga kura kujiamini na kujiwekea malengo.

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za uhakika ambapo mimi mtumishi wako Erythrocyte nitakuletea kila kinachojiri.

==========
UPDATES 1

Polisi yavurumishia risasi na Mabomu kwenye Msafara wake eneo la Nyamongo

kwa sababu zisizofahamika , video hii hapa



UPDATES 2
Baada ya mabomu Nyamongo ilikuwa hivi

 
Tundu Lissu asonge mbele na ashikilie pale pale.......
1. Watumishi wa umma miaka 5 bila nyongeza.
2. Fao la kujitoa.
3. Waliovunjiwa nyumba zao kufidiwa.
4. Kufumua upya/Kuondoa Misururu mingi ya kodi
5. Kurudisha mikopo ya elimu ya juu bila kujalisha shule aliyosoma mwanafunzi.
6. Wakulima wapate haki yao
7. Kuhuisha Mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
8. Vitambulisho vya Wamachiga.
nk nk nk nk nk nk.

Watanzania tuna jambo letu 28.10
 
Saa ya ukombozi inakaribia kabla jua halijazama kila mtu atakuwa amemuelewa huyu Mwamba kutoka kanda ya kati Tundu Lissu.

Wananchi wa Serengeti msikatishwe tamaa na Polisi CCM.

Ukombozi uko hatua mmoja mbele bado kidogo ,kutapambazuka kwa shangwe kuu.

Tunataka Uhuru Haki na Maendeleo ya Watu.
 
###28 October tuna jambo letu##
Usivunjike moyo Wala kukatishwa tamaa kamanda Lissu
Mzee wangu IGP mh sirro kwa kipekee nimekuweka kwenye mahombi, na kesho naanza ya taifa,kipindi kigumu wapita ila niliagizwa nikuweke kwenye maombi ,sikufaham ila lazima nitekeleze yaliyo yake mkuu,
 
Leteni hizo video polisi wakifyatua risasi na kurusha mabomu ya machozi.
 
Saa ya ukombozi inakaribia kabla jua halijazama kila mtu atakuwa amemuelewa huyu Mwamba kutoka kanda ya kati Tundu Lissu.

Wananchi wa Serengeti msikatishwe tamaa na Polisi CCM.

Ukombozi uko hatua mmoja mbele bado kidogo ,kutapambazuka kwa shangwe kuu.

Tunataka Uhuru Haki na Maendeleo ya Watu.
Hii ni hatari sana
 
Back
Top Bottom