Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu Jana ameingia Kigoma kwa kishindo kikuu.
Alilakiwa na Maelfu Elfu ya watu waliojipanga majiani huku wakitandika mikeka chini shujaa huyo wa karne hii apite juu yake.
Akihutubia umati mkubwa unaokadiriwa kuwa na watu zaidi ya Elfu 30 katika viwanja vya Community Centre Lissu alisema alichokishuhudia Kigoma ni kwamba wananchi wameamua kuondoa utawala wa kidhalimu na kuweka utawala utakaojali #UTUHAKINAMAENDELEOYAWATU#
Tundu Lissu alisema Chadema kinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Zitto Kabwe ambaye ni mzaliwa wa Mkoa huo.Lissu aliuambia umati huo Chadema na ACT ni kitu kimoja katika uchaguzi huu na kwamba wananchi wamchague mgombea anayeweza kuitoa CCM madarakani ambaye ana ushawishi Hoja na anayeungwa mkono na watu.
Huku wakimjibu kwa kelele za Shangwe wananchi hao walipaaza sauti na kusema ni Zitto Kabwe watakayemchagua kuwa mbunge wao na kura zote za Urais wataelekeza kwa Tundu Lissu
Awali Lissu aliwaambia wananchi hao kwamba wakati anaumwa alipata Salaam kutoka kwa watu wa Kigoma walizomtuma kijana wao Zitto Kabwe.
Mara baada ya kuhutubia Shujaa huyo akisindikizwa Kifalme na umati mkubwa uliokuwa ukiimba Rais Rais Rais mpaka Hotelini kwake.
Siku moja kabla ya Tundu Lissu Kuwasili Kigoma Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe alitoa tangazo rasmi la kunikaribisha mkoani humo na kuwataka wananchi kumpokea kwa Shangwe