Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
1. Police wameshindwa kumpata Mbowe hadi amefika kwenye maandamano na kurekodiwa na vyombo vyote vya ndani na nje.
2. Jeshi la police limekuwa barabarani wakiwa na silaha na magari kwa siku 3 nchi nzima.
3. Watanzania wote wamejua chadema inaandamana na inazuiwa na serikali .
4. Watanzania wamefikishiwa ujumbe wa waliotekwa na waliupotezwa.
5. Serikakali imefikishiwa ujumbe, watanzania wanajua haki zao, ni watu wa amani, police wanatakiwa kuwalinda hata kwenye maandamano.
Ahahahahaha! Mabingwa wa kuandamana nyuma ya keyboards at work! Ahahahahaha!!Waandamanaji wa leo walikuwa polisi, mabango yalikuwa mitutu ya bunduki ya polisi na mic za waandishi wa habari
Kiongozi wa maandamano alikuwa Mh. Mbowe aliyefanikiwa kutoa hotuba kabla ya kutiwa nguvuni
Kimantiki ujumbe waliokusudia kuutoa umefika sehemu iliyokusudiwa na waliosaidia kuufikisha ni askari polisi na waandishi wa habari. Kufikisha ujumbe hilo ndio lengo kuu la maandamano yoyote yale duniani.
CHADEMA wanatakiwa kuwashukuru viongozi wa serikali na polisi kuwasaidia kufikisha ujumbe wao pengine kuliko ambavyo wangeandamana wenyewe tu bila hiki kilichotokea leo
Wengi mnaogopa kuumizwa na kufa na vinginevyo!.Ahahahahaha! Mabingwa wa kuandamana nyuma ya keyboards at work! Ahahahahaha!!
Linapokuja swala la kuandamana nchi hii inawaandamanaji maalum, ni swala la kuwa-switch tu muwaamrishe waandamane nchi nzima, mkoa mmoja au wilaya moja! Hawajawahi kushindwa hao. Hujaona leo walivyoandamana kwa magari, wengine kwa miguu na wengine wakiwa na mbwa tena wakiwa na sare zao safiii kabisa. Wako smart!Ahahahahaha! Mabingwa wa kuandamana nyuma ya keyboards at work! Ahahahahaha!!
halafu watu wanasema hapakuwa na maandamano, hii ni nini sasa? Au maandamano maana yake nini?