Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa ndio mumewaongezea umaarufu mbele za Mungu na Wanaadamu, na CCM watashudhwa hadi pande za mwisho za shimo, yajayo yanafurahisha...
 
Kwa ushuhuda aliotoa Mnyika kilichomtokea Mbeya, Kwa aliyemwelewa sidhani kama Kuna mtu angepeleka pua yake kwenye maandamano.
 
UJINGA kabisa, si ndio waliosema CHADEMA imekufa??🤣😅🤣😅
 
Yaani wana ccm wengi ni wajinga!
Wanashindwa kujiuliza ni kwanini wamelazimika kutumia gharama kubwa kuzuia maandamano ya upinzani!

Kama wanajiamini kiasi hicho ni kwanini hawakuwaacha upinzani waandamane?
 
Huyu jamaa alijidai kulima vitunguu iringa vimemshinda sasa karudia kazi ya uchawa kaona inalipa... maishaa mchezo kilimo tuachieni sisi.
 
 

Attachments

  • IMG-20240924-WA0033.jpg
    101.2 KB · Views: 5
Kinacho shangaza zaidi ni hao hao wanaofanya maovu ndio wanao himiza "utulivu, amani"!
Watu wasiotaka wananchi wawachague viongozi wao bila ya kufanyiwa mizengwe, ndio hao hao wanao hakikisha uchaguzi hauwi wa haki.

Yote haya wanayasema hadharani kana kwamba raia hawana akili za kujua kinacho fanyika!

Labda nimalize kwa kuuliza swali: Hivi hilo jeshi, wao hawawezi kamwe angalao hata kuhakikisha tu kuwa uchaguzi unapo fanyika ni lazima uwe wa haki? Tuseme wao wawepo tu kuhakikisha jambo dogo kama hilo linafanyika, hata bila ya kutaka kuingilia mambo ya siasa, na kutaka kuchukua madaraka wao wenyewe.

Hilo Jeshi, likiamua kufanya hivyo; kwa nini lilaumiwe; na nani alaumu jambo kama hilo mbali tu ya hao wasiotaka watu wawe huru kuchagua viongozi wao.

Gabon, nchi ya Afrika Magharibi, jeshi lilikataa ushindi wa wizi aliokuwa ameunyakua Omar Bongo, rais wa huko aliyekuwa na yeye karithi toka kwa baba yake. Sasa kwa nini sisi huku, CCM iwe imeteka nchi nzima, hata vyombo vyote vya dola vinavyotakiwa kuwa huru na kulinda maslahi ya nchi?
Hivi vyombo sasa ndio vimekuwa vya kuwakandamiza wananchi kwa niaba ya CCM?
 
Tundu aliamua kukwepa kuongelea maandamano akakimbilia tigo. Very unfortunate kwa siasa za bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…