Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi ndivyo hali ilivyo sasa.

Jana walivamia makazi ya Dr. Slaa Mbweni ili kumkamata, wakakuta ndio anafika kutoka hospitali akiwa ametoka kufanyiwa upasuaji wa jicho.
 
Au labda Wanamchukua ili aisende kwenye maandamano ili jumuiya ya kimataifa isipige kelele… more likely watafanya hivyo Kwa mbowe na Viongozi wengine?
Najiuliza tu…
 
Wakuu,

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Peptemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.

=====

Asubuhi imeanza kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.

=============

CHADEMA kupitia akaunti yao ya X wameripoti kuwa Jeshi La Polisi Tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

CHADEMA imeripoti kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.

CHADEMA .png
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hayo magari ya polisi hayajabebwa askari wa kutuliza ghasia (Field Force Unit (FFU)). Yaani, hao ni makomandoo ndani ya uniform ya FFU!!


ilala-boma-px.jpg
 
Maandamano ya kupanga tarehe na kuhamasishana ni ngumu kufanikiwa especially yanayoongozwa na viongozi wa kisiasa.....
Lakini ipo siku isiyo na jina watu wataingia road bila shuruti wala kuongozwa na hawa polisi watayakimbia makazi yao.
Hapo sasa serikalini ndo itajua nguvu ya umma
 
Back
Top Bottom