Wakuu,
Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,
Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema
wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.
Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Peptemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.
Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.
=====
Asubuhi imeanza kwa taarifa ya
Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.
=============
CHADEMA kupitia akaunti yao ya X wameripoti kuwa Jeshi La Polisi Tangu jana usiku mpaka asubuhi ya leo Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi limefunga barabara zote zinazoelelea nyumbani kwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
CHADEMA imeripoti kuwa watumiaji wote wa barabara hiyo wanasimamishwa na kukaguliwa, wakiulizwa kama wanaenda kwenye maandamano.