Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Siku ya waliyosema chadema kufanya maanadamano kwaajili ya kupinga utekaji na watu kuuliwa na watu wasiyojulikana imefika,

Tangazo hili lilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Septemba 11, 2024, ambapo alisema wataingia barabarani endapo wanachama wao waliopotea hawatarudisha na kama serikali haitawajibika ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi husika.

Ratiba ya maandamano ilitolewa Jumamosi tar 21 Peptemba 2024 baada ya kuwa serikali haijatekeleza takwa lolote kati ya yale yaliyotolewa na CHADEMA kuhakikisha kuna uwajibikaji.

Fuatilia uzi huu kwa matukio ya moja kwa moja kwa siku ya leo na yatakayojiri kwenye maandamano hayo.

=====

Asubuhi imeanza kwa kwa taarifa ya Lissu kuzingirwa na polisi na kutakiwa kwenda kuripoti katika ofisi ya RCO Kinondoni, ambapo amekubali kwenda kuitikia wito.
Naungana na Hayati Magu siasa ni kipindi cha uchaguzi na kila mtu jimboni kwake!
 

Attachments

  • Screenshot_20240716_193908_Google.jpg
    Screenshot_20240716_193908_Google.jpg
    382.5 KB · Views: 2
Salaam

Hapa gomz mwisho wanapotengeneza stand ya mwendokasi.

Imepaki chuma moja mpyaa ( Mercedes-Benz) spesho kwa ajili ya kutawanya wanao sema wataandana leo.

Najua kila upande wana point zao na msingi kuandamana/kuzuia maandamano , Kwangu mimi naona ndugu zangu tufanye kazi tu kwa uwaminifu na kufuata sheria za nchi. Mapungufu yapo kwa serikali ila fikiria sana familia yako kabla hujaandamana.

Najua mtanitukana sana kwenye comment ila habari ndio hiyo.


Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom