Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Salaam

Hapa gomz mwisho wanapotengeneza stand ya mwendokasi.

Imepaki chuma moja mpyaa ( Mercedes-Benz) spesho kwa ajili ya kutawanya wanao sema wataandana leo.

Najua kila upande wana point zao na msingi kuandamana/kuzuia maandamano , Kwangu mimi naona ndugu zangu tufanye kazi tu kwa uwaminifu na kufuata sheria za nchi. Mapungufu yapo kwa serikali ila fikiria sana familia yako kabla hujaandamana.

Najua mtanitukana sana kwenye comment ila habari ndio hiyo.

Nawasilisha.
Mawazo yako ni ya busara. Atakayekupinga ni mpumbavu
 
Salaam

Hapa gomz mwisho wanapotengeneza stand ya mwendokasi.

Imepaki chuma moja mpyaa ( Mercedes-Benz) spesho kwa ajili ya kutawanya wanao sema wataandana leo.

Najua kila upande wana point zao na msingi kuandamana/kuzuia maandamano , Kwangu mimi naona ndugu zangu tufanye kazi tu kwa uwaminifu na kufuata sheria za nchi. Mapungufu yapo kwa serikali ila fikiria sana familia yako kabla hujaandamana.

Najua mtanitukana sana kwenye comment ila habari ndio hiyo.

Nawasilisha.
Akili za kijinga Kabisa Hizi, nipo Mwembechai
 
Ulivyo muoga umeogopa hata kupiga ka picha???

Habari bila picha ni sawa na mke kukunyima unyumba.

Kataa ndoa.
20240923_082130.jpg
 
WANANCHI wanaendelea na shughuli zao kama Kawaida

Leo ni siku ya Amani jijini DSM Mungu wa mbinguni awabariki nyote

Ahsanteni sana 😄
 
“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa uadilifu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mashahidi kwa uadilifu. Wala chuki ya watu isikufanyeni kutenda isivyo haki. Tendeni haki; hiyo ndiyo iliyo karibu zaidi na ucha Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye khabari za yale myatendayo.

”Aya hizi zinafundisha kuwa haki lazima ipewe kipaumbele katika hukumu, na kuhukumu kwa usawa ni sehemu ya ucha Mungu. Qur'an inaweka msingi thabiti wa maadili ya haki katika hukumu na inawataka Waislamu kuwa waaminifu na waadilifu katika kila jambo la hukumu na maamuzi.
 
Polisi hebu tumieni hekima kidogo ili kuimarisha taswira nzuri ya Mama Samia Suluhu Hassan kitaifa na kimataifa.

Msitumie nguvu kuzuia maandamano, bali imarisheni ulinzi ili maandamano yafanyike kwa amani.

Dunia nzima Leo macho yako Tanzania. Hii ndio nafasi pekee ambapo Polisi wetu wanaweza kuionyesha dunia kwamba Tanzania hakika ni kisiwa cha amani na utulivu.
 
Back
Top Bottom