Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waiteni wakenya wawasaidie, hapa boma polisi kidogo tu watu wamekula kona
 
Siku mbili kabla ya kufanyika maandamano ya Dibagula yaliyohusu kupinga tamko la kuwa Yesu ni Mungu,maalim Ali Basaleh alitangaza wazi kabisa mbele yetu msikitini siku ya Ijumaa kuwa angeshiriki japo polisi walikwishayapiga marufuku
Sheikh Ali Basaleh alisema yeye angekaa mbele kabisa na angevaa sanda ili akipigwa risasi basi azikwe na sanda hiyo.Na kweli siku ilipofika alivaa sanda na akakaa mbele akitoa takbir.Alipigwa lakini pamoja na kuumia hakulia.
Tukija upande wa Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema yeye kasema kupitia twiter kuwa ataandamana na akatoa ramani ya maeneo maandamano yatakapoanzia na kuishia.Mwenyekiti huyo kupitia akaunti yake hiyo alisema akipigwa risasi watu wamuombee dua na wasonge mbele.
Watu wetu kwenye vituo vyote wanasema bado hawajamuona mwenyekiti wa Chadema.
 
Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.

Hata hao askari wenyewe ni waoga tu. Kama wasingekuwa waoga wangekataa kutumika na ccm. Au wangekaza kukubali maagizo toka juu.

Bado hakijatokea kizazi ambacho kipo tayari kupigwa, kufungwa, kufa juu ya masuala ya kisiasa.

Hakuna vijana wa kufatilia au kutaka kuhusika na masuala ya aina hiyo.
Vijana wako bize na mipira, miziki, mitandao,mikeka ya kubeti, minguvu ya kiume, mapenzi, kukata mauno, matamasha, tamthilia na misambwanda

Narudia tena

Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.
Watu wanasaka pesa na wanatoboa, we kaa usubiri kama Dj Mbowe space atakuletea pesa zaidi ya kukutolea mikengeza yake.
 
Kutoboa ni mpaka walizoozaliwa 1999 kurudi nyuma watoweke wooote
Kutoboa labda siku itokee mgogoro kati ya ccm na vyombo vya ulinzi na usalama. Hao ndio wakiamua na kuungana ndio wanaweza kuwatoa ccm madarakani systematically au kwa kupindua.

Hapo kije kizazi kipya cha maaskari.

Zaidi ya hapo narudia, hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania hata mimi ni muoga sana.
 
Pamoja na yote, serikali imejaa woga. Unapita sehemu unaona defender, askari kama kumi hivi kila mtu kashika smg yake, wanasubiri tu kundi la watu walirushie risasi za moto.

Hakuna mtu anaweza kuandamana mbele ya kundi lililojaa cowards, kama ingekuwa peaceful demonstration naamini wengi wangejitokeza, ila hii ya kutaka kuua watu kwa kutaka kutimiza haki yao kikatiba, sio rahisi kujitokeza.

Autocracy is real in Afrika, there's no way myu akamsema Magu tofauti na mama, kwenye swala la utawala bora wote ni failure tu.
 
Siku mbili kabla ya kufanyika maandamano ya Dibagula yaliyohusu kupinga Yesu si Mungu,maalim Ali Basaleh alitangaza wazi kabisa mbele yetu msikitini siku ya Ijumaa kuwa angeshiriki japo polisi walikwishayapiga marufuku
Sheikh Ali Basaleh alisema yeye angekaa mbele kabisa na angevaa sanda ili akipigwa risasi basi azikwe na sanda hiyo.Na kweli siku ilipofika alivaa sanda na akakaa mbele akitoa takbir.Alipigwa lakini pamoja na kuumia hakulia.
Tukija upande wa Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema yeye kasema kupitia twiter kuwa ataandamana na akatoa ramani ya maeneo maandamano yatakapoanzia na kuishia.Mwenyekiti huyo kupitia akaunti yake hiyo alisema akipigwa risasi watu wamuombee dua na wasonge mbele.
Watu wetu kwenye vituo vyote wanasema bado hawajamuona mwenyekiti wa Chadema.
We ulisha wahi kuona wapi commander wa kikosi anaka frontline?
 
Hakuna mtu muoga sana kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana.
Nadhani la maana ni kupata unachokitaka na si kuonekana tu si muoga, unaweza ukaandamana ukachezea kipigo na bado hayo maandamano yasiwe na manufaa yeyote katika kubadili au kupata ulichotaka na ukaishia kuonekana si muoga tu basi. Haya maandamano yanashindikana si kwa sababu ya uoga bali ni kukosa muamko tu na huo ndio uhalisia.
 
Back
Top Bottom