Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ila Chadema ni next level kwa kweli, wamewapigisha kwata hawa manjagu kwa wiki nzima sasa na kuufikisha ujumbe wao kwa gharama za serikali yenyewe, akili kubwa ni akili kubwa tu .
Huku ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.

Hiki kilichotokea leo Dunia nzima ilijua kitatokea, unext level wa CHADEMA unatokea wapi?

Watanzania kuogopa kuandamana baada ya kuwaona POLISI wametanda barabarani ni suala la kuisifia CHADEMA?

Hili ni suala la kuisikitikia CHADEMA, nguvu yao ya ushawishi haijai hata kwenye kisoda.
 
  1. Hali ilivyo katika eneo la Dar es Salaam wakati ambapo maandamano yalliyotangazwa na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yakitarajiwa.
    .

    .

    Mshirikishe mwenzako, Kwa Picha: Hali ilivyo katika mji wa Dar es Salaam
  2. Dakika 11 zilizopitaHabari za hivi punde,Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akamatwa​

    Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam .Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.
    Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao.
    Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.
    Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.
    Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo CREDIT: BBC
 
Huku ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.

Hiki kilichotokea leo Dunia nzima ilijua kitatokea, unext level wa CHADEMA unatokea wapi?

Watanzania kuogopa kuandamana baada ya kuwaona POLISI wametanda barabarani ni suala la kuisifia CHADEMA?

Hili ni suala la kuisikitikia CHADEMA, nguvu yao ya ushawishi haijai hata kwenye kisoda.
Akili kubwa tu ndiyo inaweza kuelewa, akili kisoda kama yako haiwezi kuelewa kamwe.
 
Baba mlezi wa Deusdedith Soka amejitokeza katika maandamano ya amani Ilala Sokoni. Azungumzia kupotea kwa Soka.

Your browser is not able to display this video.​
Pole sana mzee, si vizuri kila kitu tukakifanyia siasa...

Wakati wenzako wanatafuta milliage za kisiasa wewe unapata maumivu ya kweli...

Haya maandamano yasingekua na slogan ya "Samia must go", sidhani kama yangezuiwa...

Bado naamini haya maandamano yamefelishwa na slogan...

Ni vyema baada ya leo yaitishwe maandamano ya watu wote kupinga utekaji na mauaji ya watanzania, yakiwa na slogan zinazoendana na maumivu tunayopitia sio slogan za kisiasa...
 
CHADEMA waache kutusemea.Maana nafikiri maumivu hayajatupata ipasavyo.Siku tukichoka huu upumbavu tutaandaamana pasipo kuongozwa na chama chochote.CHADEMA tumeona juhudi zenu ila kwa sasa acheni kuwatetea wasiojielewa.
 
Back
Top Bottom