Baada ya Ijumaa kesi kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani.
Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.
=====
Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa
WS Robert Kidando anasimama
Jaji: Ndiyo
Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Pius Hilla
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
Wote wanawakilisha Jamhuri katika kesi hii...
Wakili Peter Kibatala nae anasimama na anatambulisha Jopo la mawakili wa upande utetezi.
- Maria Mushi Evaresta
- Kisanga Hadija Aron
- Alex Massaba Idd
- Msawanga Seleman
- Matauka Dickson Matata
- Nashon Nkungu
- Fredrick Kihwelo
- John Mallya
- Peter Kibatala
Wakili wa Serikali: Shauri hili linakuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna Shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea
Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali: Mmoja anaenda Kumfuata Shahidi JAJI yupo Kimyaaaa anaandika Kidogo
Peter Kibatala anaomba Radhi kwa Kuchelewa Kidogo
Jaji: Shahidi wa ngapi huyo?
Wakili wa Serikali: Shahidi wa 8
Jaji: Majina yako
Shahidi: Superitendent Jumanne Malangahe
Jaji: Umri
Shahidi: 46
Jaji: Kabila
Shahidi: Msukuma
Jaji: Shughuli yako
Shahidi: Afisa wa Polisi
Jaji: Dini yako
Shahidi: muislam
Shahidi: Wallah wabillah taala nathibitisha kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie
Wakili wa serikali: Kitambulisho Bwa Jummane Unafanya Kazi gani
Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni nini
Wakili wa Serikali: Elezea hapa Mahakamani Tarehe 04 Mwezi August 2020 ulikuwa wapi
Shahidi: 04 August 2020 nilikuwepo katika Kituo Changu cha Kazi, Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Nikiwa Ofisni Kwangu nilipigiwa Simu na Afande Kingai, Akinitaarifu kuna Safari Ni jiandae Ya Kwenda Kufanya Moshi, Mkoani Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: ilikuwa Muda gani wakati anakupigia Simu
Shahidi: Ilikuwa Muda wa Saa 12 na Kitu
Wakili wa Serikali: ya Muda gani
Shahidi: Ya Jioni
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea Kutokana na alichokutaarifu
Shahidi: Alikuwa afande ACP Ramadhan Kingai
Wakili wa Serikali: Katika Majukumu yako ya Upelelezi na Kusimamia Askari waliopo Chini yako no Shughuli gani katika Upelelezi hufanyika
Shahidi: Baada ya Shauri Kufunguliwa, ndipo Upelelezi Unapoanza kwa kuwakamata wa husika, Kupelele Shauri na Kukagua eneo la Tukio Pamoja na Kuku Sanya Vielelezo namambo Mengine kutokana Aina ya tukio
Detective Coplo Francis, Detective Coplo Goodluck pamoja na Dereva wa Gari Detective Constable Azizi
Wakili wa Serikali: Wakati Kingai anaingia Ofisini Kwako hawa wenyewe walikuwa wapi
Shahidi: Wali ingia Wote Ofisini Kwangu
Wakili wa Serikali: Elezea sasa baada ya Kuingia Ofisini nini Kiliendelea
Shahidi: Nilijiandaa na Saa 1 kasoro aliwasili nikiwa Ndani nikasikia Muungurumo wa Gari, nikampokea na Kwenda Ofisini Kwangu Kisha tukaketi
Wakili wa Serikali: Wakati Kingai anafika, Yeye alikuwa na nani?
Shahidi: Alifika na Askari Jumla walikuwa watano akiwemo yeye Mwenyewe, Insp Mahita,
Tukianza Safari ya Kuelekea Moshi
Wakili wa Serikali Pale Moshi Mlifika Saa ngapi?
Shahidi: Saa 2 Usiku
Shahidi: Afande Kingai akasema anaendelea Kupokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wake Kutoka Kwa Msiri wake. Na hivyo Miongoni Mwa Wahalifu hao watatu walikuwa wameshawasili Moshi kwa ajili ya kutekeleza Uhalifu huo Akasema Jukumu letu ni Kuzuia Uhalifu huo Kutendeka na Kuhakikisha Wahalifu hao tunawakamata Baada ya Kumalizia kutoa Maelekezo hayo ilikuwa ni Takribani saa Moja
Shahidi: Afande Kingai Alianza Kutoa Taarifa Kwamba Kipo Kikundi Cha Kihalifu ambacho kinatarajia Kufanya Matukio ya Kihalifu hapa Nchini Ambayo ni Kulipua Vituo Vya Kuzuia Mafuta, Kuanzisha Vurugu na Maandamano, Kukata Miti na Magogo na Kuyaweka katika Barabara Kuzia Magari
Akatuambia amepata Taarifa wale Wahalifu Wapo Maeneo ya RAU Madukani, Walikuwa watatu na akatuelekeza Mwonekano wao na aina ya Nguo walizo vaa
Wakili wa Serikali: Elezea Sasa Kesho yake Asubuhi nini Kiliendelea
Shahidi: Tulikutana Kituo cha Mjini Kati pale Moshi akasema, Tuendelee Kupokea Taarifa Mpaka atakapojiridhissha Mazingira Yamekaaje
Shahidi: Tuliendelea Kuwepo Maeneo yake Mpaka Takribani Saa 6 Mchana Afande Kingai akatuita tena
Wakili wa Serikali: Kuhusiana na hicho alichowaambia Kingai Kuhusiana na Mwonekano wa Nguo ulikuwaje
Shahidi: Alisema Wawili Kati yao Wanamaumbo Madogo Madogo lakini wa mevaa Masharti Mekundu Kati ya wale wawili Mmoja Amevaa Shati la Maua Mekundu Mekundu, Mmoja amevaa Shati la
Maua Maua ya Kijani iliyopauka Na Watatu alivaa Jezi ya Mpira ya Taifa Stars ambayo ilikuwa na Rangi ya Blue
Wakili wa Serikali: baada ya Kuwa eleza Mwonekano wao.?
Shahidi: Alituambia tuelekee katika Eneo hilo Haraka tuweze Kufanya Ukamataji, Ndipo tuliondoka Kuelekea Eneo la Rau Madukani
Wakili wa Serikali: Mlipoondoka kuelekea Rau Madukani mlikuwa nani na nni?
Shahidi: Ramadhan Kingai Mimi Mwenyewe Inspector Mahita GOODLUCK Francis Na Dereva wa Gari Azizi
Wakili wa Serikali: Mlifika Saa ngapi?
Shahidi: Mchana Takribani Saa Saba
Shahidi: Tukaelekea Gari ambapo Afande RCO alikuwa ameelekezwa Eneo ambalo Wahalifu Wamekaa. Alisema Kwenye Grocery
Wakili wa Serikali: Grocery ilikuwa wapi?
Shahidi: Palepale Rau Madukani, Ambapo Kwenye Kona ya Barabara, Yenyewe ipo kando kabisa ya hiyo Barabara
Shahidi: Tuliegesha Gari yetu, Ndipo Afande RCO akamtuma Kwanza Inspector Mahita Kwenda Kujiridhisha Kama Watu wenye Mavazi na Mwonekano huo wapo
Wakili wa Serikali: Mahita alifanya nini
Shahidi: alishuka Kwenye gari, a Kapita Kwenye lile eneo na baada ya Muda Mfupi akarudi
Wakili wa Serikali: Baada Ya Kurudi Majibu yalikuwa nini?
Shahidi: Amewaona wamekaa Katika Kibanda
Wakili wa Serikali: Walikuwa wa ngapi
Shahidi: Watatu
Wakili wa Serikali: Nini kilofuata
Shahidi: Afande RCO katuamuru tushuke kwenye gari, Akatugawa. Makundi Mawili
Shahidi: kundi moja lilikuwa Kingai, Mimi na Goodluck, lingine Mahita na Coplo Francis
Shahidi: Alitoa Maelezo Kwamba Mahita Aelekee Upande wa Kushoto na Sisi tuelekee Upande wa Kulia
Shahidi: Mwonekano wa Eneo hilo ni kama hivi, Hapa Bara Bara imepita, Kuna Uwazi, Hapa pembeni Kuna Uwazi, na Ndipo Maduka Yanatizana Babarabarani, Kuna Banda lipo ambapo Lenyewe kuna uwazi Katikati na Limepakana na hiyo Glocery (Shahidi anaelekeza kwa ishara za mikono yake) Vilevile Kwenye Banda Kuna Uwazi wa Kuingilia, na Kwenye haya Maduka Kuna Choo lililopakana na Grocery
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa ile Taarifa aliyowapatia Mahita, Elezea ni wapi walikuwa watu hao
Shahidi: Walikuwa ndani ya eneo hili, Walikuwa wamekaa Grocery
Wakili wa Serikali: Sasa Ulisema Mpangilio wenu ulikuwa Mgawanyiko mara mbili, Je akina nani walipita Kushoto na akina nani walipata Kulia?
Shahidi: Inspector Mahita na Coplo Francis Walipitia Upande wa Kushoto, Mimi na Afande Kingai na Goodluck tulipitia Upande wa Kulia ambapo Kuna Banda hilo
Shahidi: Tukianza Kuelekea Katika Maeneo hayo Mawili Kama ambavyo Afande RCO alikuwa anaelekeza
Wakili wa Serikali: RCO ndiyo nani
Shahidi: Afande Mahita
Shahidi: Na pale tuliokuwa tunaenda watu walipokuwa karibu ni Coplo Francis na Inspector Mahita. Sisi wakati tunaelekea Kwenye hilo Eneo hatukuona Watu, tulipotaka Kuingia Kwenye huo Uchochoro hatukuona Watu Ghafla tukasikia Sauti, ambayo ilikuwa Sauti ya Inspector Mahita
Wakili wa Serikali: Ukisikia Mahita akisema nini?
Shahidi: "KAA CHINI, UPO CHINI YA ULINZI" kwa Sauti ya Juu
Wakili wa Serikali: Elezea Mlipofika Pale nini Kiliendelea pale
Shahidi: Baada ya Kufika Pale ACP Ramadhan Kingai aliwauliza Majina Yao Nao walijitambulisha kwa Majina ya Adam Hassan Kasekwa na Mwingine Mohammed Ling'wenya
Shahidi: tulitembea Kwa Haraka Kuelekea Kwemye hilo Eneo ambapo tuliwakuta
Wakili wa Serikali: Mliwakuta walifanya Nini?
Shahidi: Watu wawili walikuwa wamekaa chini
Kibatala: OBJECTION hiyo ni Leading
Shahidi: Coplo Francis alikuwa na silaha
Wakili wa Serikali: Silaha ya aina gani
Shahidi: SMG
Wakili wa Serikali: Kwa Upande wenu je
Shahidi: alikuwa nayo Goodluck
Wakili wa Serikali: Wakati mmesikia Amri ya a kukaa Chini Kitu gani Kingine alichofanya
Shahidi: Tulikutana anamalizia Kuwaambia Kwa Sauti kwamba wanatuhumiwa Kula Njama za Kufanya Vitendo Vya Kigaidi
Wakili wa Serikali: Wakasemaje?
Shahidi: hawakujibu Kitu wakati ule, Lakini Afande Kingai akasema ndiyo wenyewe, Na baada ya hapo a kawaambia kuwa Wanatuhumiwa Kula Njama kutenda Makosa ya Kigaidi, Baada ya Maelezo hayo aliniamuru Mimi Kufanya Upekuzi wa Maungoni
Wakili wa Serikali: Mwanzoni Mlisema Mlikuwa Mnaenda Kukamata watu watatu Je Mwingine Yupo wapi
Shahidi: Mtu wa tatu pale hakuonekana, Mpaka Afande Kingai aliulizwa Pale Mwingine Yupo wapi,
Wakili wa Serikali: Alikuwa anamuuliza nani?
Shahidi: Aliwauliza Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Eneo lipi walikuwa wamewekwa Chini ya Ulinzi Katika Eneo hilo
Wakili wa Serikali: Ukisema Upekuzi wa Maungoni Unamaanisha Nini?
Shahidi: Kupekua Ndani ya Nguo na Sehemu za Maungo yao
Wakili wa Serikali: baada ya hapo Ulifanya nini?
Shahidi: Nikamwambia Afande Kingai kuwa Ngoja Nikaite Watu kwa ajili ya kushuhudia
Wakili wa Serikali: Ukawafuata wapi?
Shahidi: Palikuwa na Maduka na Mabanda kwa hiyo niliamini kuna watu wanaoendelea na Shughuli zao Na hapo watu watu walikuwa Wamesha Anza Kusogea
Wakili wa Serikali: Zoezi la Kutafuta Mashahidi lilifanyikaje
Shahidi: Nili angalia Maeneo Kadhaa Nikaenda Kwenye Banda, Ni kauliza nani anaye husika hapa, Kwamba Kwakuwa Kulikuwa wazi basi Kuna Shughuli zilikuwa zinaendelea Baada ya Kuuliza hivyo alijitokeza Dada Mmoja kwa Jina la Anita Mtaro
Wakili wa Serikali: yeye alikuwa wapj
Shahidi: ikiwa amesimama Mbele ya Banda lake Kidogo
Shahidi: Hatua Kidogo Katika Banda, Katikati ya hayo Maduka na Pembeni Kidogo Kuna hayo Maduka
Shahidi: Pia nikijambulisha kuwa Mimi ni Afisa wa Polisi nikamuonyesha Kitambulisho Changu akakubali Kusogea
Wakili wa Serikali: palikuwa na Hatua ngapi au Umbali gani
Shahidi: Hatua Sita au Saba
Shahidi: Yule Dada alisita Kidogo, akaniuliza ataamini Vipi Kama Mimi ni Afisa wa Polisi Nikamtolea Kitambulisho Changu Cha kazi ambacho ni Chekundu, akakubali Nikaenda pia pale Grocery nikamkuta Dada Mmoja anaitwa Esther Nduhul
Wakili wa Serikali: Kuna Umbali gani Kutoka Watuhumiwa walipowekwa Chini ya Ulinzi?
Shahidi: Hapakuwa mbali sana Takribani kama Hatua 5
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea
Shahidi: Nilijitambulisha Kwake kwamba Mimi ni Afisa wa Polisi na baada ya hivyo nilimuomba asogee kuja Kushuhudia
Ni kawaambia Wanatuhumiwa Kwa Vitendo Vya kula Njama ya Kutenda Makosa ya Ugaidi na hivyo nahitaji kuwapekua katika Maungo yao
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupata Mashahidi nini Kiliendelea
Shahidi: Nikiwa uliza tena Majina watuhumiwa ambao walikuwa bado wamekaa Chini Wakajitambulisha tena kwamba ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Na Mimi Nikajitambulisha kwao kwamba naitwa ASP Jumanne Malangahe
Wakili wa Serikali: Wakati huo Anita Mtaro na Esther Nduhulu walikuwa wapi?
Shahidi: Walikuwa palepale Wakishuhudia
Shahidi: nikatoa Vitu vyangu na Kunyoosha Mikono yangu Nikamwambia Mtuhumiwa wa Kwanza asimame,
Wakili wa Serikali: Ambaye ni Nani?
Shahidi: Adam Kasekwa
Shahidi: Nilimwambia ageuke Nyuma, Anyooshe Mikono Juu, alitii na nilianza kumpapasa Kuanzia Kichwani, Shingoni, Kifuani na Nilipo fika Sehemu ya Kiunoni nilihisi Kitu kigumu Upande wa Kushoto, Nilipitisha Mkono wangu nikishika kitu Kigumu na Kukichomoa, kilikuwa ni silaha
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni sehemu gani?
Shahidi: Kwenye Mkanda au Pindo la Silaha
Wakili wa Serikali: Ikafuata nini Shahidi Nikaichomoa na Kuonyesha hii ni salaha, Ni Bastola na Nichomoa Magazine, ilikuwa na Magazine na Ndani ya Magazine Ilikuwa na Risasi tatu
S
hahidi: Baada ya Kuuliza Mikono Mifukoni Mwake, Upande wa Kushoto sikuoata Kitu, Ila Upande wa Kulia Niliingiza nikatoa Simu Ndogo aina ya Itel Ila Pia nikatoa Kinailoni baada ya Kukitoa, ambacho Kilionekana kimeviringishwa nikakitoa nikakinyoosha ambacho Kilikuwa ni Kirefu Na Kilikuwa na Vitu Mfano wa Karanga
Wakili wa Serikali: Vilikuwa ni Vitu gani
Shahidi: Nilihisi ni Madawa ya Kulevya. Nikampatia Goodluck Nikaendelea kupapasa zaidi nikaingiza Mifukoni Mwake
Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vingapi
Shahidi: Nili Sogea kwa Mtuhumiwa Nikaanza Kuhesabu Nilihesabu Zikawa 58 Ndani ya Simu palikuwa na Line Mbili Nilituma Goodluck aende kwenye Kuchukua Fomu ya Hati ya Kuchukulia Mali Nilianza Kujaza kwa kuitambua Ile Silaha.
Shahidi: Lakini Pia Nilijaza fomu Nyingine ambapo Nilijaza hizo Kete za Huo Unga ambao nilihisi ni Madawa ya Kulevya
Wakili wa Serikali: Ulifanya nini kwenye hiyo Fomu
Shahidi: Nilimuonyesha Mtuhumiwa akaangalia akasaini na Anita na Esther na wao wakasaini katika fomu zote Mbili
Shahidi: Ambayo ilikuwa imeandikwa Luger A5340 na namba hizo zilikuwa zimeandikwa Upande wa Kulia, Na pia niliorodhesha Risasi Tatu ndani ya hiyo Magazine Pamoja na Simu na line zake
Wakili wa Serikali: Ulikuwa unaorodhesha wapi?
Shahidi: Katika fomu hiyo, Hati ya Kukamatia Mali
Wakili wa Serikali: Ulifanya nini Kuhusu Mtuhumiwa Mohammed Ling'wenya
Shahidi: Kwanza baada ya Kumalizia Kujaza nilitoa Carbon Nakala ya Ile Fomu nikampa Adam Kasekwa ambaye nilimwambia akae Chini Nikamsimamisha Mtuhumiwa wa Pili na Yeye Nikamwambia ageuke
Shahidi: Naye nilianza Kumpekua Kichwani Na Kiwili wili chake sikuona kitu Nikaanza Kuingiza Mikono yangu Mifukoni Mwake Nikakutana na Simu Kubwa aina ya Tecno, Yeye pia nilimkuta na Vikaratasi Ambayo nilihisi ni Madawa ya Kulevya, nikavihesabu Mbele ya Mashahidi Vilikuwa 25
Vilevile nilifungua ile simu Nikaikuta ina line Mbili, za Hallotel na Airtel niliwaonyesha Mashahidi na Kuendelea Kuteremka Sehemu za Miguu lakini sikuona Kitu Nilichukua Fomu nikajaza na Fomu Nyingine Nilijaza hizo Kete ambazo nilihisi ni Dawa za Kulevya
Shahidi: Baada ya Kumalisha nilimpa Nakala mbili Nakala niliyojaza simu na Nakala ya fomu niliyojaza kete, Mtuhumiwa aliviona karidhika akasaini na Mashahidi wakasaini nikampa Nakala zake
Wakili wa Serikali: na Hivi Vitu ambavyo unasema Ulijaza eneo la Rau Baada ya hapo ulivipeleka wapi
Shahidi: Nilimkabidhi Goodluck ambaye nilikuwa namkabidhi tangu Mwanzo, na Pia Nikachukua fomu nikajaza na Kumkabidhi.
Wakili wa Serikali: Leo hii ukiiona ile Pistol Unaweza Kuitambuaje?
Shahidi: Kwa Serial Namba A5340
Shahidi: Na Jina lake lililoandikwa Luger
Wakili wa Serikali: Luger imeiona wapi
Shahidi: Luger Ipo Kushoto
Kibatala: OBJECTION naomba hilo Jibu liondolewe Kwenye Kumbukumbu za Mahakama
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi hatuoni tatizo, na Pingamizi Halina Mashiko
Kibatala: Nasema hivi Shahidi aliulizwa kabla hajashika Kielelezo na akaulizwa Utatambuaje akasema Kwa Serial Na Na hapa akaulizwa Umeitambuaje akasema Kwa Kuona Serial Na Wakili akasema Luger Ipo wapi Kitu ambacho Shahidi hakutaja, Ndiyo nasema huko nikumlisha Majibu Shahidi
Anasimama WS mwingine Pius Hilla
Kibatala: Hana haki Kusimama, Nimeweka Pingamizi, Amejibu Wakili Robert Kidando na Nimejibi tena huyu anasimama Kufanya nini?
JAJI: Ngoja tu tumsikilize...
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Baada ya Kutaja Na Kuonyesha Serial Namba, Wakili akauliza Neno +Luger lipo wapi, Ni swali tu ambalo Shahidi anatakiwa Kujibu kuwa Neno Luger lipo wapi, Kwa Maelezo Hayo ni swali Genuine, Na Kama litazuiliwa haiwezi kuwa sawa na hili Jibu naliondoa Kwenye rekodi, Labda Urudie Upya Swali
Jaji: Shahidi aliulizwa Vigezo ambavyo anaweza Kutambua Kielelezo, Kwa Serial Namba na Mahala ya hiyo serial Namba na Baada ya Hapo Wakili akauliza hilo Neno Luger Lipo wapi akasema hili hapa, ndiyo alichosema Kwa namna ambavyo Kibatala ameweka hoja yake nakubalina na Kibatala
Wakili wa Serikali: Shahidi Unakitu gani Kingine Unachiweza Kutambua Silaha hiyo?
Shahidi: Kwa Serial number zake, A5340 NA Kwa Jina la Silaha hiyo lipo Upande wa Kushoto Luger
Wakili wa Serikali: Naomba Kupatiwa exhibit P3 Mahakama inampatia
Wakili wa Serikali, Robert Kidando, anaifungua
Wakili wa Serikali: angalia Kielelezo hiki kama unakitambua, na Ukikitambua Utasema Kama unakitambua
Shahidi: Nakitambua
Wakili wa Serikali: Unakitambuaje
Shahidi: A5340
Wakili wa Serikali:: Ipo wapi
Shahidi: ANAONYESHA KWA KIDOLE
Wakili wa Serikali: na Risasi 3 zilikuwa wapi?
Shahidi: Zilikuwa ndani ya hii Magazine
Wakili wa Serikali: Sasa wakati Unatoa Ushahidi Wako Ukasema Baada ya Kupata Pistol hii kutoka Kwa Mtuhumiwa Adam kasekwa na Ukapata Risasi tatu, Onyesha Risasi hizo Umetoa wapi
Shahidi: Nilipata kwenye Magazine,
Wakili wa Serikali: Magazine hiyo Ipo wapi?
Shahidi: Hii hapa (ANAONYESHA KWA KIDOLE)
Kibatala: Mshtakiwa wa kwanza anaomba Kwenda uani kidogo
Jaji: kwenda kwake kutasimamisha Shughuli za Mahakama
Kibatala: suala la kukubaliana tu
Nashon: Kwa kuwa wakili wake nipo naomba Mahakama iendelee wakati anaenda uani
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba niendelee
Wakili wa Serikali: Kuna hitaji la Kisheria 196 cha CPA wakati Ushahidi Unachukuliwa, Mshtakiwa Anatakiwa awepo
Jaji: katika Mazingira anamwakilisha na ameridhia Kama wakili wake yupo inatosha, Je unahisi bado Kuna ulazima
Wakili wa Serikali: Tunaomba Guidance yako Mheshimiwa
Jaji: Kwanza Kwa staha, Ombi Lenyewe la Kwenda Uani, Records haiwezi Kuonyesha Kwenye records zangu, Kwanza ameshaingia
Wakili wa Serikali: Shahidi Umesema Wakati unampekua Mtuhumiwa Adam kasekwa Ukijaza Hati ya Kukamatia Mali, Je Leo Mahakamani Ukiiona unaweza Kuitambuaje
Shahidi; Kwa Mwandiko wangu, Majina yangu, Sahihi yangu na Vitu Nilivyo Orodhesha Hapa, Pamoja na Saini za Walioshuhudia Wakati wa Upekuzi na Majina yao
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tunaweza Kupatikana Exhibit IP1 Mahakama inampatia Nyaraka
Wakili wa Serikali: Shahidi hebu Shika Nyaraka hiyo na uangalie na uweze Kuiambia Mahakama.
Shahidi, ANASOMA
Shahidi: nimeitambua ni Hati ya Vielelezo Nilivyo Pata kwa Mshitakiwa Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali: Umeitambuaje?
Shahidi: Kwa Majina Yangu Sahihi yangu Mwandiko wangu Na Majina ya mashahidi Yapo. Pia Mtuhumiwa Mwenyewe Majina yake Niliandika ambayo yamo pamoja na Sahihi yake
Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini hiyo Hati ya Kukamatia Mali
Shahidi: ningeomba Mahakama Ipokee Hati ya Kukamatia Mali kama Sehemu ya Ushahidi wangu Hati inapelekwa kwa mawakili wa utetezi
Mawakili wa upande wa utetezi wanaikagua!
Nashon Nkungu: Kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza tunapinga uchukuliwaji wa nyaraka hii Na msingi wetu ni kwamba nyaraka hii imendaliwa kwa sheria ambayo haipo kwenye nchi yetu Hii siyo nyaraka ya kawaida, Bali msingi wake ni sheria tu
Nashon Nkungu: Lakini Nyaraka hii imenukuu Kifungu cha Sheria 38(3) Sura ya 20 ya mwaka 1985 iliyorekebishwa mwaka 2005 ambayo haijulikani, naomba isipokelewe sababu haijulikani sheria hiyo
Nashon anakaa chini baada ya kumuomba Mheshimiwa Jaji asipokee
Mallya: Kwa niaba ya mshtakiwa wa pili tunapinga kupokelewa kwa nyaraka hii kwa mawasilisho aliyosema Wakili Nashoni Nkungu Na Kuongezea tu hakuna marejeo ya sheria hii mwaka 2018 na hakuna mapitio ya sheria hii ya 38 imefanyiwa marekebisho Mwaka 2019. Na hatuwezi kujua kwamba walimaanisha kwamba ni 2019 na mara ya mwisho Kifungu cha 38 kimefanyiwa Mwaka 1993 baada ya hapo Hakuna Kama Kielelezo kinahusu Mahakama lakini siyo Ya Tanzania Ambayo Kwa MAHAKAMA yako Tukufu haina Sheria hii yenye Marejeo ya Mwaka 2018 Kusimama bila Sheria, Na Sidhani kama Wenzetu watabisha kwamba Kuna Marekebisho ya Sheria hii ya Mwaka 2018, Hii ni Nyaraka isiyo halali kwa Maana hiyo haiwezi kuishi Katika Nyaraka za Mahakama, Na Mallya amesema hapa Kwamba hata hawakuomba kama Kuna Marekebisho tunaomba Upitie
Fredrick Kihwelo: kwa niaba ya Mshtakiwa namba 03 tunapinga pia Kielelezo Kwa Njia ileile ya Kupinga kwa sababu Nyaraka imeletwa kwa Sheria ambayo Haipo kwenye Vitabu Vya Sheria zetu Tanzania Wakili Fredrick anaketi.
Kibatala: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne Tunaunga Mkono Pingamizi la wakili wa Mshtakiwa Wa kwanza, Kwa ufafanuzi ni kwamba... Nyaraka hii imeundwa Chini ya msingi wa Kisheria ndiyo Maana yenyewe inasema IMETOLEWA CHINI YA KIFUNGU..... inaonyesha wenyewe wanajua kuwa haiwezi
Kibatala: civil Appeal ya Mwenderosi VS Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ilisema Kwamba Overriding Objective haikuletwa Mahakamani Dhidi ya wadawa. Na Kuhusu Madhara ya Kuleta Nyaraka iliyonukuliwa Kinyume na Sheria usome...
Kibatala: Kesi ya Ardhi ya John Marco VS Joshua Malimbe ni Uamuzi wa Mahakama Kuu, lakini Mahakama ilirejea Mashauri kadhaa, Maamuzi hayo Robert VS Shibeshi Abebe, Na akarejea Mahakama ya Rufaa ya Mgonja Dhidi ya..... Na Kesi ya Anthony Tesha VS Anita Tesha ya Mahakama Ya Rufaa
Kibatala: Nisikuchoshe Mheshimiwa Jaji, Ni hayo tuh Na Nyaraka hii isipokelewe
Jaji: upande wa Serikali!
Wakili wa Serikali: Kutokana na Pingamizi hilo na Wamerejea Mashauri Kadhaa, ku support Hoja zao, Tunaomba Hairisho fupi tuweze Kulipitia, tuweze Kujibu na pia tunaomba Nakala ya Kesi hizo.
Wakili wa Serikali: Tukipata Hairisho la Saa Moja Linatosha
Jaji: Utetezi
Kibatala: Kwakuwa ni haki yao sisi hatuwezi Kuwapinga
Kibatala: Kuhusu Kuwapa hizo kesi, Tumetoa kwenye Tanzii ambayo ni Kifaa Kazi ila tunaweza Kuwasaidia wao Kupata
Jaji: Sahihi
Wakili wa Serikali: Kama zote zipo Tanzii haina shida tutazipata
Jaji: Kufuatia Maombi ya Wakili wa Serikali Robert Kidando Mahakama Inahairiswa Mpaka saa 7 na Dakika 20 Jaji anatoka Saa 6 Na Dakika 20
---------
Mawakili wa upande wa serikali wameonba kuongezwa muda wa dakika 30, mahakama ilikuwa irejee saa 7:20 saa za Afrika ya mashariki. Wameongezewa muda huo, Sasa Mahakama itarejea saa 7:50