Habari Wakuu,
Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake
Fuatana nami kupata yatakayojiri
UPDATES:
Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
Seleman Matauka
Alex Massaba
Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Khadija Aron
Michael Lugina
Evaresta Kisanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Dickson Matata
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea
Shahidi anapanda Kizimbani
Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo
Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho
Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...
Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje
Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi
Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect
Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?
Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26
Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi
Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time
Malya: Kwa Kazi gani
Shahidi: Ulinzi Ndiyo
Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?
Shahidi: kwenye meseji hazipo
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35
Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?
Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe
Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako
Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari
Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram
Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram
Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua
Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?
Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe
Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?
Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu
Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani
Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa
Mahakama: (Kicheko)
Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini
Shahidi: Tarehe 20 July 2020
Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini
Shahidi: alikuwa ananipigia Simu
Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi
Shahidi: Kwa Telegram
Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record
Shahidi: Sina Utaalamu huo
Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe
Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu
Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo
Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp
Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram
Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu
Shahidi: Sikuonyesha
Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..
Malya: sitaki sababu hapa
Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu
Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu
Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu
Malya: Naomba Kielelezo Namba 28
Malya anamkabidhi shahidi
Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu
Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka
Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka
Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote
Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi
Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane
Shahidi: Washa wewe
Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako
Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji
Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni
Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha
Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa
Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke
Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona
Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne
Shahidi: Ndiyo
Malya: Soma hapa
Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu
Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini
Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire
Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza
Shahidi: Ndiyo
Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?
Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe
Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe
Malya: Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi
Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua
Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako
Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao
Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?
Shahidi: Sikueleza
Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?
Shahidi: Mimi sifahamu
Malya: Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi
Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi
Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia
Shahidi: Hakuniambia
Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi
Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine
Malya: Bwire alikuja Nyuma yako
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini
Shahidi: 2010
Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora
Shahidi: Hapana
Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki
Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu
Malya: Ulipewa award gani
Shahidi: Sikupewa Award
Malya: Lakini wewe Ulifuzu
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?
Shahidi: Ni sahihi
Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi
Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa
Shahidi: Ni Afisa
Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani
Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye
Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?
Shahidi: Hapana
Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi
Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam
Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa
Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi
Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi
Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi
Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi
Shahidi: TSh 199,000
Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi
Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao