Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Urio ndiyo kabeba kesi yenyewe - na ndiyo maana alikumbushwa kwamba baada ya ushahidi wake anaweza kuwa Shujaa ama mtu wa hovyo kabisa kutokea hapa duniani...
Lt. Denis Leo Urio kasababisha watu wajifikirie upya kuhusu uLuteni, uKomandoo na JWTZ kwa ujumla...
 
sasa maswali kama haya yamesaidia nini mbowe? kama eye witness na mtu aliyekuwa anawasiliana naye na kukutana naye anasema mpango wa ugaidi ulikwepo, hata kama kamati ya ulinzi na usalama au yeyote hata kuwa na taarifa inahusu nini? ndio wanasheria wenu hao. hapo laymen huko mtaani wanashangilia ati ameuliza maswali magumu.
 
Kweli kazi polisi imelaaniwa. Hivi hao askari wa chini ya Kingai wanamchukuliaje kwa ujinga alioufanya katika kesi hii. Huyu mungu ampe mateso makali sana siku zake za mwisho zikikaribia.
 
sasa maswali kama haya yamesaidia nini mbowe? kama eye witness na mtu aliyekuwa anawasiliana naye na kukutana naye anasema mpango wa ugaidi ulikwepo, hata kama kamati ya ulinzi na usalama au yeyote hata kuwa na taarifa inahusu nini? ndio wanasheria wenu hao. hapo laymen huko mtaani wanashangilia ati ameuliza maswali magumu.
shahidi ndiye alikuwa anaratibu ugaidi.anatakuwa akamatwe chap ashitakiwe kwa njama za kuratibu ugaidi
 
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

Seleman Matauka
Alex Massaba
Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Khadija Aron
Michael Lugina
Evaresta Kisanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Dickson Matata

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda Kizimbani

Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo

Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho

Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...

Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi

Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect

Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?

Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26

Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi

Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time

Malya: Kwa Kazi gani

Shahidi: Ulinzi Ndiyo

Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?

Shahidi: kwenye meseji hazipo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35

Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?

Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe

Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako

Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari

Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram

Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram

Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua

Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?

Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe

Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?

Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu

Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani

Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa

Mahakama: (Kicheko)

Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini

Shahidi: alikuwa ananipigia Simu

Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi

Shahidi: Kwa Telegram

Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record

Shahidi: Sina Utaalamu huo

Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe

Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu

Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo

Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp

Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram

Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu

Shahidi: Sikuonyesha

Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..

Malya: sitaki sababu hapa

Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu

Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu

Jaji: Shahidi sililiza swali ndiyo ujibu
hivi hawa ni mashahidi wa jamhuri kweli? Mbona kila shahidi anamtetea mbowe na wenzake? Maana waliochunguza walisema hawakuona viashiria vya ugaidi mbali na matendo yenyewe, huyu wasasa anasema vijana alioombwa nikwaajili ya ulinzi na sio ugaidi
 
Urio ndiyo kabeba kesi yenyewe - na ndiyo maana alikumbushwa kwamba baada ya ushahidi wake anaweza kuwa Shujaa ama mtu wa hovyo kabisa kutokea hapa duniani.

Wacha tuone leo maana jana hakutoka hata na point moja..alishidwa kabisa kumshawishi achilia mbali Jaji lakini mtu yoyote anayefuatilia hii kesi.
sijui kwa kibatala itakuwaje,hapo ndio ataapa viapo vya dini zote
 
lazima watanzania wote kwa pamoja tuungane kupinga na kuondoa viashiria vyote vinavyo weza kuharibu Amani ya Nchi.

Vitendo vya kigaidi vya ndani ni chanzo kikubwa cha kuhatarisha usalama na utulivu wa nchi.

Hivyo ni lazima viashiria vyote vitokomezwe bila ajizi.
Unaonekana hata hufuatilii kesi... uki post huu utumbo uwe una weka na hoja
 
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

Seleman Matauka
Alex Massaba
Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Khadija Aron
Michael Lugina
Evaresta Kisanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Dickson Matata

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda Kizimbani

Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo

Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho

Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...

Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi

Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect

Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?

Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26

Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi

Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time

Malya: Kwa Kazi gani

Shahidi: Ulinzi Ndiyo

Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?

Shahidi: kwenye meseji hazipo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35

Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?

Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe

Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako

Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari

Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram

Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram

Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua

Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?

Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe

Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?

Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu

Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani

Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa

Mahakama: (Kicheko)

Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini

Shahidi: alikuwa ananipigia Simu

Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi

Shahidi: Kwa Telegram

Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record

Shahidi: Sina Utaalamu huo

Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe

Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu

Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo

Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp

Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram

Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu

Shahidi: Sikuonyesha

Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..

Malya: sitaki sababu hapa

Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu

Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu

Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu

Malya: Naomba Kielelezo Namba 28

Malya anamkabidhi shahidi

Malya:
Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu

Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka

Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka

Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote

Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi

Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane

Shahidi: Washa wewe

Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako

Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji

Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni

Malya:
Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha

Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa

Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke

Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona

Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne

Shahidi: Ndiyo

Malya:
Soma hapa

Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu

Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini

Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire

Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza

Shahidi:
Ndiyo

Malya:
Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?

Shahidi:
Mimi sifahamu anafahamu Mbowe

Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe

Malya:
Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua

Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako

Shahidi:
Ndiyo

Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao

Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?

Shahidi: Sikueleza

Malya:
Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?

Shahidi: Mimi sifahamu

Malya:
Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi

Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi

Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia

Shahidi: Hakuniambia

Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi

Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine

Malya: Bwire alikuja Nyuma yako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini

Shahidi: 2010

Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora

Shahidi: Hapana

Malya:
Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu

Malya: Ulipewa award gani

Shahidi: Sikupewa Award

Malya:
Lakini wewe Ulifuzu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?

Shahidi: Ni sahihi

Malya:
na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi

Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa

Shahidi: Ni Afisa

Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani

Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye

Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?

Shahidi:
Hapana

Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi

Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam

Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa

Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi

Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi

Shahidi:
Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi

Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi

Shahidi:
TSh 199,000

Malya:
hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi

Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao
Huyu shahidi Leo anaweza akatoa uharo hapo maana mambo yamebana
 
shida yote mnapata kwa sababu mfadhili wenu wa vitendo vya kihalifu kabanwa kooo.
safari hii hamna ujanja....moto umemuwakia na lazima utamuunguza.
 
Urio maskini, laah !! akina Kingai kweli ni watu wabaya sana - jamaa hata hajielewi afanye lipi aache lipi hadi anatia huruma.

Malya:
Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Back
Top Bottom