Habari Wakuu,
Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake
Fuatana nami kupata yatakayojiri
UPDATES:
Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka
- Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- Seleman Matauka
- Alex Massaba
- Paul Kisabo
- Sisty Aloyce
- Maria Mushi
- Khadija Aron
- Michael Lugina
- Evaresta Kisanga
- John Mallya
- Nashon Nkungu
- Dickson Matata
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea
Shahidi anapanda Kizimbani
Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo
Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho
Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...
Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje
Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi
Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect
Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?
Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26
Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi
Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time
Malya: Kwa Kazi gani
Shahidi: Ulinzi Ndiyo
Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?
Shahidi: kwenye meseji hazipo
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35
Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?
Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe
Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako
Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari
Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram
Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram
Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua
Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?
Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe
Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?
Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini
Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu
Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani
Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa
Mahakama: (Kicheko)
Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini
Shahidi: Tarehe 20 July 2020
Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini
Shahidi: alikuwa ananipigia Simu
Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi
Shahidi: Kwa Telegram
Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record
Shahidi: Sina Utaalamu huo
Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe
Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu
Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo
Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp
Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram
Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu
Shahidi: Sikuonyesha
Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..
Malya: sitaki sababu hapa
Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu
Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu
Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu
Malya: Naomba Kielelezo Namba 28
Malya anamkabidhi shahidi
Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu
Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka
Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka
Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote
Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi
Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane
Shahidi: Washa wewe
Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako
Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji
Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni
Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe
Shahidi: Sikuonyesha
Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha
Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa
Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke
Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona
Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne
Shahidi: Ndiyo
Malya: Soma hapa
Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu
Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini
Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire
Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza
Shahidi: Ndiyo
Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?
Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe
Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe
Malya: Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi
Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua
Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako
Shahidi: Ndiyo
Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako
Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao
Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?
Shahidi: Sikueleza
Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?
Shahidi: Mimi sifahamu
Malya: Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi
Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi
Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia
Shahidi: Hakuniambia
Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi
Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine
Malya: Bwire alikuja Nyuma yako
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini
Shahidi: 2010
Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora
Shahidi: Hapana
Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki
Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu
Malya: Ulipewa award gani
Shahidi: Sikupewa Award
Malya: Lakini wewe Ulifuzu
Shahidi: Ndiyo
Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?
Shahidi: Ni sahihi
Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi
Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa
Shahidi: Ni Afisa
Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani
Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye
Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?
Shahidi: Hapana
Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi
Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam
Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa
Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi
Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi
Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi
Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi
Shahidi: TSh 199,000
Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi
Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao
Malya: Ulielezea Shahidi Kwenye Ushahidi Wako namba Uliyotumia Kuwasiliana na Bwire ni Namba gani
Shahidi: Sikueleza
Malya: Wakati Mnaenda Kuonana na Swila Mara ya Kwanza Ilikuwa lini
Shahidi: Tarehe 11 August 2020
Malya: Ndiyo Siku hiyo ulitoa Maelezo Yako
Shahidi: Ndiyo
Malya: Nimesikia Siku Unakutana na DCI Mlikutana baadae akaja Kingai
Shahidi: sahihi
Malya: Ulielezea Kuna mtu Yoyote alikuja Kuwa Join Baadae
Shahidi: Kuwa Join wapi?
Malya: Kwenye Kikao cha Siku hiyo na DCI na Kingai
Shahidi: Hakuna Mtu yoyote alikuja Kutujoin Siku hiyo
Malya: Kwenye Meseji ya Mwisho ambayo Mbowe alikutumia, Ukasema Hukueleza, ni kwanini hukutuma Meseji Nyingine Kuuliza Una maana gani
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Baada ya Kupita Muda Hakuna Mawasiliano, Nilimuuliza Bwire Boss wako anajua, Sasa ningejibu Meseji ya Nini
Malya: Na ni Ushahidi Wako Kwamba Ofisi za Swila ni Ghorofa ya Nane Makao Makuu
Shahidi: Ni sahihi
Malya: Mheshimiwa nafikiri Sina Swali la Ziada kwa Shahidi huyu
Anasimama Adv. Dickson Matata
Matata: Nikumbushe Ulionana na Mbowe Tarehe ngapi
Shahidi: Mwezi Wa Saba, 2020 Sikumbuki Tarehe gani
Matata: Na Ulipo Onana naye ndiyo alikwambia anahitaji Vijana Wa Kuambatana naye wa Kuchukua dola
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa Maelezo yako Ndiyo alikwambia anahitaji Vijana hao Vijana Kwa ajili ya Kumsaidia Kuwashambulia Viongozi ambao hawaupendi Upinzani
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Ndipo alipokwambia Kwamba anataka Kuhakikisha anachoma Masoko na Vituo Vya Mafuta
Shahidi: Naomba Ni'refresh alisema Kwamba ataleta Taharuki Kwa Kufanya hayo Uliyo niambia
Matata: juzi Ulisema Kwamba Ulifanya Kitu kinaitwa Tactical appreciation, na Mimi Leo nataka tufanye Tactical appreciation ya Kisheria, Wakati anakwambia Mlikuwa Wawili
Shahidi: Ndiyo
Matata: Kwa Lugha Nyingine Hapakwepo na Watu wengine
Shahidi: Sahihi
Matata: tofauti na Siku hiyo, Kuna Siku yoyote aliwahi Kukwambia Jambo hilo au kukuandikia Barua
Shahidi: Hakuna
Matata: Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine hatutopata ushahidi wa maandishi au wa sauti au meseji unaoweza kuthibitisha kuwa alikwambia hayo maneno?
Shahidi: Hakuna sauti
Matata: Baada ya Kukwambia Ukaona Inafaa ukatoe Taarifa, Ukaenda kwa DCI, Kwanza Ulimpigia Simu halafu akakupa appointment
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Kwamba Baada ya Kumueleza akamuita Kingai
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba DCI ni Mtu Mwenye Ujuzi Katika Upelelezi
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kingai alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Unafahamu Kwamba anakuwa na uzoefu wa Upelelezi
Shahidi: Kwanza Nilikuwa sijui kuwa ni Mpelelezi
Matata: Mtu akiwa Mpelelezi Wa Mkoa ana uzoefu au hana Uzoefu
Shahidi: anakuwa na Uzoefu
Matata: Wewe Kama Komandoo, Katika Kikao hicho na Baada ya Hapo, Hukuona wewe au DCI na Kingai, Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu kuwa Msiridhike Kile ambacho umesema, Je Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu Wa Kurekodi Voice Notes
Shahidi: Mamlaka labda Ndiyo haikuona Umuhimu
Matata: Wewe Uliona Kuna Umuhimu au Hakuna Umuhimu, Kwamba Usiridhike na Maneno Utengeneze Voice Record
Shahidi: Niliona Kuna Umuhimu
Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia
Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko
Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti
Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?
Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"
Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko
Shahidi: Hakuna mahali inasema
Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?
Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo
Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta
Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo
Matata: Tutoke hapo, Unasema Ulienda Kwa DCI na Kabla ya kwenda Ulimpigia Simu,
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulielezea Mahakama Kwamba Ulikuwa Unafahamiana na DCI
Shahidi: Nilieleza, Kuna Mtu aliuliza Kama Nilienda Ofisi ya DCI Mara ngapi
Matata: Mimi Sitaki Habari ya Kwenda Ofisini, DCI Anabadirika, nakuuliza Kama Ulielezea Kwamba Unafahamiana na DCI
Shahidi: Sikueleza
Matata: Ulieleza Mahakamani hapa Kwamba Namba yake Ulipata Wapi
Shahidi: Sikueleza
Matata: Hata hiyo namba yenyewe Ulitaja
Shahidi: Sikutaja
Matata: Ushahidi gani Unathibitisha Kwamba Ulimpigia Simu
Shahidi: Ushahidi ninao kwa sababu nina namba zake na Nilifika Ofisini Kwake
Shahidi: Je ulivitaja hivyo Vitu Wakati Unahojiwa na Upande wa Mashitaka
Shahidi: Sikuvitaja
Matata: Unasema Kwamba Ulienda Kesho Ukasema Una Appointment naye Ukakutana na Secretary Wake
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa Maana hiyo Ulifuata Utaratibu wa Umma Wa Jinsi ya Kuingia Ofisi Fulani
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulisema Kwamba Ulipofika Ulifuata taratibu za Ofisi za Umma
Shahidi: Nilieleza Kwamba, Nilionyesha Kitambulisho kama Askari
Matata: Ulisema Kwamba Askari apaswi Kufuata Utaratibu Wa Kuingia Ofisi Za Umma
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mimi Nilieleza Kuwa ni Askari, yeye Ndiye alitakiwa aniambie Kufuata Utaratibu
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, Ulisema Kwamba Nyie Askari hamfuati Utaratibu
Shahidi: Sikueleza
Matata: Ulileta Visitors Book Kuonyesha Kweli Ulienda Ofisi Za DCI
Shahidi: Hapana Sikuleta
Matata: Shahidi Wewe ni Mwanajeshi, Ulitakiwa Kufuata Taratibu zote za Kijeshi
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Unapotoka Mkoa Mmoja Kwenda Mkoa Mwingine, unatakiwa Kuwa na Movement Order
Shahidi: Inategemea na Siku Ngapi, Kama Chini ya Siku Tatu unaweza Kwenda bila Movement Order kama zaidi ya Siku Nne Unatakiwa Kuwa na Movement Orde
Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili Abdallah Chavula Uliyasema hayo
Shahidi: sikuyasema
Matata: Unapokuwa Askari Unapoenda Ofisi za Umma si lazima Uwe na Pass
Shahidi: Ni kwenye Kitabu Unachotaka,
Matata: Si lazima uonyeshe Pass
Shahidi: Ndiyo ni lazima
Matata: Umeleta Mahakamani hapa Pass Kwamba Umeruhusiwa Kutoka kazini Kwako
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sijaleta Sikujua I nahitajika Mahakamani
Matata: Tarehe 11 ulienda kwa Inspector Swila na Tarehe 12 Ulimpelekea Simu
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Ulileta Mahakamani Hapa Pass za Umeruhusiwa
Shahidi: Sikuleta, Sikupewa Maelezo
Matata: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 20
Matata: Naomba Nikuonyesha Kielelezo namba 20 ambacho Kina Miamala yako ya namba ya Airtel
Matata: Jana Wakati Unahojiwa ulisema Freeman Mbowe alikurushia Kwa Mara ya Kwanza TSh 500,000
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Ukatoa TSh 499,000
Shahidi: Kweli
Jaji: Umeelewa Swali? Anasema Umetumiwa TSh 500,000, Swali Ukatoa kwenye hiyo Fedha kiasi gani?
Shahidi: Ni TSh 499,000
Matata: Kwa Mantiki Nyingine Hukutoa yote Kwa sababu Kuna Makato kidogo
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Kwa hiyo Ulichukua TSh 500,000 Ukatoa TSh 499,000 Je Makato TSh ngapi?
Shahidi: TSh 1000
Matata: Naomba Nikuonyeshe Kwa Siku hiyo, Mheshimiwa Jaji Namuonyesha Muamala Wa Siku hiyo ambapo anasema alitoa Muamala Wa TSh 499,000
Matata: Sasa Shahidi angalia Tarehe 20 July 2020, Kwenye Miamala sehemu ambayo Umeenda Kwa Wakala Ukatoa TSh 499,000
Jaji: anakuuliza Hapo Hapo hapo Kwenye hiyo Nyaraka
Shahidi: Hapa Kwenye Miamala Haipo hiyo 499,000
Matata: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe Hapo hapo, Kuna Majedwali ambayo Yanaonyesha Receiver Balance kabla ya kutumiwa TSh 500,000 kutoka Kwa Mbowe.. Utakubaliana na Mimi Kwenye akaunti yako palikuwa na TSh 49,646
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Baada ya Kuweka TSh 500,000 balance Ikawa TSh 549,646
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Tarehe hiyo hiyo Ukatoa TSh 300,000
Shahidi: Ni sahihi
Matata: Na Balance Yako Ikabakia 243,646
Shahidi: Ni sahihi
Matata: hebu chukua salio uliokuwa nalo la 549,646 Kutoa 300,000 ukabaki na 243,646 tuone Makato ni TSh ngapi
Amesimama Mmoja Wakili wa Serikali Robert Kidando
Wakili wa Serikali Robert Kidando: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Naona Hajajengewa Misingi Kwamba wakili anauliza ikiwa hayo Makato yapo au hayapo..
Matata: Mheshimiwa Jaji Mimi lengo langu nikutaka kujua kwanini Shahidi atoe TSh 499,000 akatwe TSh 1,000 na atoe TSh 300,000 akatwe Elfu Sita na usheeee..
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hicho ndicho alichopaswa Kuulizwa
Matata: Je Shahidi Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukitoa TSh 300,000 ikibakia TSh 243,646 Je Elfu 6 inaenda Wapi?
Shahidi: Siwezi Kujua Kama ni Makato au imeenda wapi
Matata: Kwani hiyo Tsh 1000 Mwanzo Ulijuaje Kama ni Makato
Shahidi: (Kimya)
Jaji: Swali lako la Mwisho liasema Kuhusu Elfu 6 nimesharekodi
Mallya anasaidia kufafanua kidogo
Matata: Shahidi Ulitoa maelezo hii TSh 1,000 Ilienda wapi
Shahidi: Sijawahi Kutoa
Matata: Shahidi sasa ulitoa...sorry Mheshimiwa Jaji Kidogo
Matata anapekua Nyaraka hapa
Matata: Shahidi Umesema Freeman Aikael Mbowe alikuwa na Mpango Wa Kulipua Vituo Vya Mafuta, Je Wakati Unahojiwa ulitaja Majina ya Vituo Vya Mafuta
Shahidi: Hakuniambia Vituo Vya mafuta anavyoenda Kulipua Bali alitaja Mikoa tu
Matata: Kwa hiyo ukiulizwa Alitaka Kulipua Vituo gani Morogoro hutakuwa na Majibu
Shahidi: Sitokuwa na Majibu kwa kweli
Matata: Tukisema Utaje Vituo Vya Mafuta alivyo taka Kulipua Mkoa wa Mwanza Utakuwa na Majibu au hutakuwa na Majibu
Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu atakuwa nayo Freeman Mbowe
Matata: Ukiulizwa pia Kuhusu Mkoa wa Dar es Salaam Vituo Vipi Vya Mafuta alitaka Kulipua
Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu anayo Freeman Mbowe, Mimi alinificha
Matata: Ukiulizwa ni eneo gani alipanga Kukata Miti kati ya Mkoa wa Morogoro na Iringa
Shahidi: Hakuniambia ni Eneo gani
Matata: Ukiulizwa, Ukiachana Na Sabaya ni Viongozi gani wengine Walipanga Kuwashambulia
Shahidi: Sikutaja Jina la Kiongozi Yoyote, Hakuniambia Kiongozi Yupi
Matata: Mpaka anakushirikisha bila Shaka alikuwa anakuamini
Shahidi: Ndiyo
Matata: Ukiachana na suala la Kumtafutia Vijana, Je alikueleza kuhusu kumtafutia vilipuzi
Shahidi: Hakunieleza
Matata: Kuhusu kumtafutia silaha za kuwashambulia viongozi
Shahidi: Hakunieleza
Matata: Naomba Kurejesha Kielelezo cha simu .. Ahsante
Mallya: Mheshimiwa Jaji, hata hivyo haiwaki.
Matata anaketi..
Anasimama Wakili Peter Kibatala
Kibatala: Shahidi Nikikuita baba Careen ni sawa?
Shahidi: Ni sawa
Kibatala: Baba Junior
Shahidi: Ni Sawa
Kibatala: Baba Jackson
Shahidi: Ni sawa
Kibatala: Jackson amezaliwa Lini
Shahidi: 17 December 2020
Kibatala: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali Ya Mkoa Morogoro
Kibatala: Nani na nani alikwepo
Shahidi: Mke wangu na Jirani
Kibatala: Wewe ni Mkristo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: unasali Kanisa lipi
Shahidi: Parokia Ya Ngerengere, Kigango cha Kizuka
Kibatala: Paroko wako Unamfahamu
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Kwani Kanisani Umeenda Mara ya Mwisho lini?
Shahidi: Juzi juzi
Kibatala: Paroko anayehudumu Ngerengere Unamfahamu
Shahidi: Simfahamu
Kibatala: Katekista anayemsadia Paroko
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: narudia tena Mara ya Mwisho Kanisani Umeenda Lini
Shahidi: Sikumbuki Kusema Kweli
Kibatala: Una Gari ya silver
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Aina gani
Shahidi: Rav 4
Kibatala: Namba zake zipi
Shahidi: T 114 DHL
Kibatala: Toka Mwaka 16 August 2020 hiyo Gari ipo Wapi
Shahidi: Kazini Kwangu Ngerengere
Kibatala: Toka Tarehe 16 August 2020 Gari hii ilikuwa parked Wapi
Shahidi: Nilikuwa natumia, Kila Nilipo ipo
Kibatala: Baada Tarehe 16 August 2020 Gari hii umeitumia
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Umekuja kutoka Morogoro kutoa ushahidi kwenye hii Kesi, na kwamba siyo kutoka kambi fulani ya Jeshi ulikokuwa umetekwa?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji (Shahidi kamuita Jaji hapa ana jambo gani?)
Kibatala: Ndugu shahidi RELAX..
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mawakili Uliwakataza Kutoa Mawazo yao Bali Kuulizwa maswali
Kibatala: Shahidi hiyo Gari Ipo wapi
Shahidi: Kambini Kizuka
Kibatala: Umepeleka lini hiyo Gari
Shahidi: Ijumaa Wiki Iliyopita
Kibatala: Utaratibu gani Umetumika kupark hiyo gari
Shahidi: Park at Your Own Risk
Kibatala: Kwa hiyo wewe Kama afisa wa Jeshi unataka Kuniambia Kuwa Una park Gari at Owner's Risk Kambini, Upo serious kweli wewe?
Shahidi: Lipo Katika Parking ya Staff
Kibatala: Bado Kwamba Unaendelea Kusema Gari ipo Parking Owner's Risk?
Shahidi: Hapana Nimeliondoa jibu la Owner's Risk
Kibatala: Jibu lako la Kwanza kwamba Uli park Chini ya Owner's Risk Ulilitoa Chini ya Kiapo?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: haya, Turudi tena Kwamba Gari Umei' park Kwa Utaratibu gani
Shahidi: Pale Hakuna Ku'Register, Nilitoka Kwenye Oparation Nikaambiwa Nije kutoa Ushahidi
Kibatala: hapo Maana yake ni Owner's Risk
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: si Ndiyo umeliondoa hilo Jibu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Naiachia Mahakama Twende Eneo Lingine
Kibatala: Mwanzo Ulisema Ulikuwa unapanda Tax huna Gari
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Basi Ujue kwanini Nimekuuliza Kuhusu Gari
Kibatala: Shahidi Fungua Yohana Sura ya 8, Mstari wa 31 Mpaka 39
Shahidi anasoma biblia hapa..
Amemaliza..
Kibatala: Unafahamu Maan ya hilo Neno
Shahidi: Ndiyo Nafahamu
Kibatala: Maana yake ni nini
Shahidi: Tusiogope, Tuseme Kweli
Kibatala: Soma pia Waefeso Sura ya 4 Mstari Wa 25 Mpaka 32
Shahidi anasomeshwa Biblia tena
Kibatala: Je, unafahamu Maana ya hilo Neno
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Maana Yake ni nini
Shahidi: Tusiseme Uongo na tupendane
Kibatala: Kwa Hiyo Unafahamu Kwamba Maisha ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya yapo Mikononi Mwako
Shahidi: Ndiyo najua
Kibatala: na Ulisema Kwamba Mara Ya Kwanza Ulikutana na Mbowe Lini
Shahidi: JULY 2020
Kibatala: Tarehe Ngapi
Shahidi: Sikumbuki ni Tarehe za Kati kati
Kibatala: zipi hizo
Shahidi: Tarehe 10 Mpaka 15
Kibatala: Hizo ndiyo Tarehe za Katikati
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na wewe ni Luten wa Jeshi la Wananchi Tanzania tunalolipenda wote
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Elimu yako ni Form Four
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulipata Divisheni Ngapi
Shahidi: Three ya Point 25
Kibatala: unajua Division Four Inaanza point ngapi
Shahidi: Point 28 ila Sikumbuki Vizuri
Kibatala: Kwa hiyo Unakumbuka au hukumbuki
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Umesoma wapi.?
Shahidi: King'ori Sekondari
Kibatala: Headmaster Wako ni nani
Shahidi: Simkumbuki
Kibatala: Graduation Mlifanya lini
Shahidi: Hatukufanya Graduation
Kibatala: Ukimaliza Form Four lini
Shahidi: Mwaka 1999
Kibatala: Yule Mchungaji Wako anayefundisha Mzumbe Mara ya Mwisho Kuwasiliana naye ni Lini
Shahidi: Sina Mchungaji
Kibatala: Na Nabii Tito anayefundisha Mzumbe Umeacha Kusali Kwake lini
Shahidi: Simfahamu
Kibatala: Habari Nzito ya Mbowe Ulimshirikisha Paroko au Mchungaji
Shahidi: Sikumshirikisha Mtu
Kibatala: lakini Ulishindwa kulala
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: lakini Ukaenda Kumshirikisha nani
Shahidi: DCI na Kingai
Kibatala: Mwingine Je?
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Msemo wa Kwamba Askari hawezi Kuwa Raia ila Raia anaweza Kuwa Askari Maana yake nini
Shahidi: Kwamba Ukishakuwa Askari huwezi kuwa Raia, Ila Raia anaweza Kwenda kujifunza Kuwa Askari
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Mnafundishwa Kuwa Jeshi la Polisi ni Jeshi Kweli au si Kweli
Shahidi: Kweli
Kibatala: Raia Akiona Uhalifu unatendeka anaweza Kuzuia Uhalifu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwamba Mwajeshi Akiona Uhalifu Unatendeka anaweza Kuzuia au anaacha utokee alafu ana report Taarifa Polisi
Shahidi: Anazuia Uhalifu
Kibatala: ila wewe Ulikuwa na Mbowe anakwambia Mambo ya Kigaidi ukamuacha
Shahidi: Ndiyo Maana Nilienda Ku report Polisi
Kibatala: Kwani Jeshini si Kuna sehemu ya kwenda Kutoa Taarifa za Kihalifu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Kuna Kitengo Kina shughulika na Ugaidi
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kuna Jeshi la Navy ambalo kazi yao Ni Kushughulika na Ugaidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: na bado wewe ni Luteni wa Jeshi kabisa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwani kwa ufahamu wako wewe Jeshi halishirikiani na Jeshi la Polisi
Shahidi: Kama ikihitajika
Kibatala: Kwani Shahidi Kwa Mfano Mbowe angelipua Kituo cha Mafuta Puma pale Mwenge, Jeshi Pale Jirani Wangedhurika au Wasingedhurika
Shahidi: Wangedhurika
Kibatala: Bado Ukaona Usiwaambie Jeshi
Shahidi: (Kimya)
Kibatala: unasema Kwamba Mbowe alikwambia Kukata Miti wapi
Shahidi: Kukata Miti Kwenye Barabara zote zinazo ingia Mjini
Kibatala: pale Kambi ya Jeshi Lugalo Kuna Barabara ya Kuingia Mjini au Hakuna
Shahidi: Ipo
Kibatala: Kama Wangekata Miti pale Barabara ya Lugalo Jeshi lingedhurika au lisingedhurika
Shahidi: Lingedhurika
Kibatala: Lakini Bado wewe Ukaona Usiwaambie Jeshi
Shahidi: Nilipeleka Taarifa Polisi Kwa sababu wao Wana husika na Uchunguzi
Kibatala: Kati ya Wewe Ulipo pale Mgulani Kambini na Ofisi za DCI, Wapi Ilikuwa Rahisi Kwako Ku report?
Shahidi: Kambini Mgulani
Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa Logic na Common sense
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: haya pale kwa DCI umesema Kwamba Kuna Scanner, Umejitambulisha Kuwa wewe ni Luteni na ukafanyeje
Shahidi: Nikatoa Kitambulisho
Kibatala: Baada ya Pale Ulimwambia Jaji Kwamba Jina lako liliingizwa Kwenye Register
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba sisi tumefika Kwa DCI Mara ngapi
Shahidi: Hapana, Sijui
Kibatala: Nikikukwambia Kwamba pale kwa DCI Nilifika Kumsindikiza Edward Lowassa Mwaka 2017
Shahidi: Ndiyo nitakubali
Kibatala: Unafahamu Kuwa DCI ni Mwanajeshi
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Kuna Mtu alipiga Simu Kwanza Kuhakiki appointment Yako
Shahidi: Hapana Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba Wanajeshi hasa DCI ambaye ndiye Kama WAZIRI Mkuu wa Jeshi la Polisi ni watu wa tahadhari kwa sababu ni Watu wana deal na Uhalifu Nchi Nzima?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je, Umemwambia Jaji Kwamba Kuna Kitambulisho Ulipewa cha Kuvaa
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwa DCI Kuna Askari Kwa ajili ya Kimsindikiza Wanaenda Kwa DCI
Shahidi: Sikumwambia Jaji
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Askari Wa Kukusindikiza Mpaka Kwa PS wa DCI
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Waiting Area ya Ofisi za DCI Makochi ni Rangi gani
Shahidi: Ya Brown
Kibatala: Unauhakika Kwamba Siyo Mekundu
Shahidi: (Kimya)
Kibatala: Ukifika kwenye Ofisi za DCI PS anakuwa Upande Upi
Shahidi: Upande huu, (anaonyesha Kushoto)
Kibatala: Umebadilsha Sasa hivi eeh?
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba niilipokuwa Ulipokuwa wait Area Kwa DCI iwapo Body Guard Wake Ukiwa Una subiri Kuingia
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Jana wakati wa Ushahidi Ulizungumzia Meza na Viti, Je Ulizungumzia DCI kuwa Ni Mnene, Mfupi, Mwembamba au Lah
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ukaona ni Muhimu tufahamu Viti na Meza na siyo DCI ambaye Ulimfuata
Shahidi: DCI SI anajulikana
Kibatala: anajulikana na nani
Shahidi: Watanzania wote
Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Utaratibu gani Ulitumia Kutoka
Shahidi: Sijamwambia