Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

Kutoka kwa Kibatala,tusome;

Waefeso 4

25 Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.

26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

27 wala msimpe Ibilisi nafasi.

28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

31 Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;

32 tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
 
Yohana 8

31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?

34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.

38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.

39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.
 
sijawahi ona watu wanapenda picha kama cdm. sasa mnyika kaenda hapo ili aonekane tu kwenye picha. akitoka hapo nje anaweka mkutano anawatukana majaji ati majaji wa michongo. hata heshima kwa mahakama hana, na bado anaenda hapo kila siku. kavimbisha mashavu tu kwa hela za wanachadema, na hawasaidii lolote. siku mkija kuwafahamu undani hawa viumbe, mtajua mlipoteza muda sana.
Duh yaani we dada uliemuona kwenye hizo picha ni Mnyika tu, kweli unajua kupenda.
 
Yaani hadi kufikia leo hakuna sehemu hata moja inayojaribu kuonesha palikuwa na njama za kupanga vitendo vya kigaidi.

Halafu kamanda zero aliuhakikishia umma kwamba wanao ushahidi mzito na wa kutosha juu ya vitendo vya njama za ugaidi...
Ndugu usi-conclude mapema hivyo, bado kuna mashahidi zaidi ya kumi hatujui watakuja na lipi. Ila kwa yaliyosemwa mpaka sasa mmmmnh! sijui mie si mwanasheria ila nafuatilia kinachojiri.
 
Ndugu usi-conclude mapema hivyo, bado kuna mashahidi zaidi ya kumi hatujui watakuja na lipi. Ila kwa yaliyosemwa mpaka sasa mmmmnh! sijui mie si mwanasheria ila nafuatilia kinachojiri.
So far mm nafikiri ushahidi wa msingi at least ungekua ni kutoka kwa kina Adamoo, Lijenje, Mohammed na Bwire kama wangetumika kama undercover na wakawa upande wa jamuhuri, ila hadi so far ukiangalia msingi wa kesi na mashahidi walioletwa unaona kabsa hapa hakuna jipya tena hata akiletwa huyo Lijenje Bado haoneshi kama kuwa na ushahidi wenye mashiko
 
Huwezi kujua pengine hao wengine ndiyo wana vithibitisho kuwa mipango ilipangwa na ikapangika, ngoja tusubiri.
 
Back
Top Bottom