Mbowe sio kiazi kiasi hicho, yaani akurupuke aende kuongea na luteni wa jeshi kuhusu kuleta taharuki?
Hivi kwa cheo Mbowe alichonacho, namna anaijua serikali kuliko hata mimi ambae nisingekubali, inakuwaje aongee na luteni wa jeshi jambo classified kama hilo eti kisa ni homeboy?
Na Mbowe alipoletewa hao vijana hakutafakari kama kati yao kuna mmoja au wawili ambao ni wapelelezi na wataripoti kila analifanya jambo ambalo ni hatari kwake.
Kwa muda Mbowe amekaa kwenye siasa na anajua michezo yote michafu, anajua mwansheria wao Lissu alichofanywa how comes awe kiazi kiasi hiki?
Haiingii akilini kabisa, mtaani tu kwenye kahawa watu hawaropoki mambo kuhusiana na suala zima la usalama wa taifa, sote tujiulize Mbowe ni kiazi kiasi hicho?
Kuna watu kwenye mambo fulani unakuta hata mkewe hamuamini, nirudie tena Mbowe ni mjinga kiasi gani ajimwagie petroli na kujiwashia kibiriti?
Hawa vijana wameuzwa tu ili kumkamata Mbowe, masuala haya ya kijasusi kuuzana ni swala la kawaida, kugeukana ni suala la kawaida, yawezekana kwa asilimia kubwa Moses Lijenje yule aliopotea ndio alikuwa mchora ramani mkubwa kuwauza wenzie au alikuwa na taarifa nyeti hivyo kuwa tishio either akawa executed, how comes apotee ghafla? Yeye alijuaje polisi wanakuja asiwatonye wenzie? Maswali ni mengi sana..
Hawa kina Adamoo mpaka sasa wapo surprised na hawaamini kinachowatokea ndio ile unasikia unapigwa mshangao at the same time hujui nini kinaendelea.
Kuna wale askari walimuua Imrani Kombe former mkuu wa idara ya usalama kwa kumpiga risasi, simple logic , walifuata maagizo lakini mwisho wa siku walikutwa na hatia, which means nao waliuzwa au walitolewa sadaka kama mbuzi ya kafara ili mambo mengine yaendelee.
Huyu Urio ukimsikiliza anaonekana anajua ukweli wa mambo yote.