Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Mkuu, umefuatilia kesi hii toka jana? Wakili wa serikali alimuuliza, kwa cheo chake Urio, anaongoza askari wangapi, alijibu 30. Pia, koplo anaongoza 9.Haya maswali ya wakili wa utetezi, yana tofauti gani na hayo aliyoulizwa jana?
Kuna tofauti kubwa kati ya maswali yanayoulizwa wakati wa EXAMINATION IN CHIEF na CROSS EXAMINATION
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall



KAZI IPO

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Aisee, inamaana kagomea Hukumu ya Jaji.
Hapo kizimbani yupo chini ya kiapo cha Mahakama na yeye anajitetea kuwa yupo chini ya kiapo cha mwajiri wake. Noma

Sasa ikifika zamu ya Kibatala si itakuwa balaa!.
 
sina chuki binafsi bali nina hasira sana na mtu yeyote anaye chezea amani ya nchi hii.
huyu mboe dhamira yake ilikuwa ni kuichezea amani ya nchi huku akiwa amejificha kwenye kivuli cha uenyekiti wa chama!!
hata hivyo ashukuru sana Mungu Tanznia kuna utawala wa sheria, ingekuwa nchi zingine zisizo fuata utawala wa sheria.....hiiiiiiiiieeeee!!
Sasa unakuwaje na hasira na mtu ambaye hajathibitishwa kuwa na hatia?Mtuhumiwa yoyote ni innocent until proven guilty!
Acha hizo,sio afya kabisa!
 
Ninachoona hapa shahidi anaogopa swali la kesho kutwa na kusema yeye kuwa yupo chini ya kiapo kujibu level ya mafunzo yake ni uwongo mkubwa. Court Marshal gani anayoisingizia yeye? Ajibu swali ili mambo mengine ya endelee, na jaji pia kama kuna mchezo anaujua na anaufumbia macho. Kama hivyo shahidi hata uliswa maswali kwa kigezo cha kiapo cha jeshi. Kwani yy hadi kufika hapo kavunja viapo vingapi?
Hapo awali shahidi huyu alisema anayo ruhusa toka kwa wakuu wake wa kazi kuja kutoa ushahidi, ingawa movement order hakuja nayo mahakamani ameiacha hotelini. Sasa Hiyo Court Martial inakuja vipi hapa?
 
Huwezi kukataa kusema elimu yako ya kijeshi. Yani hajui lipi haruhusiwi kusema na lipi anatakiwa kusema. Hiyo anasubiri aruhusiwe baada ya kuuliza kwa watu walio nyuma yake.

Naona kabisa Kama Denis kapangwa au katishwa kabla ya kuanza kutoa ushahidi. Na kidogo nataka niamini kuwa nayeye aliminywa Kama walivyosema akina Adamo. Na wakijua ndio shaidi muhimu Sana kwa Jamuhuli na uwenda akasema tofauti.
 
kipigo, kina kingai washamuharibu huyu jamaa - dhambi sana hii. hayupo sawa kichwani maskini.
Ni dhambi sana huyu Urio amewafanyia hawa jamaa ...... Kama anaweza kuwadanganya watu anaodai walikuwa marafiki zake pia kuwa kuna kazi kumbe anawachomekea. Kwa nini tusiamini pia kuwa amemchomekea Homeboy wake ....!!
 
Mkuu weka chuki zako binafsi pembeni na angalia uhalisia!Hayo mambo ukiyaweka sana moyoni unaweza jisababishia matatizo ya kiafya!
Subiri kesi ifike mwisho utajua mbivu na mbichi,usihukumu kwani hiyo sio nafasi Yako!
Ukizingatia hayo basi Hukumu yoyote itayotoka haitakutesa nafsi Yako!
Duniani tunapita tu!
Mwambiye unajuwa watu wengine ukada umekuwa ukichaa unaondoa akili ya mtu heti atafungwa kwa ushahidi UPI
 
Kama elimu yake ni form four failure aliwezaje kufanya senior course?
Zamani nilikuwa nikisikia Komando nilikuwa nafikiri ni Maafisa fulani ambao wamekuwa trained kwenye kiwango cha juu .... Kumbe ni design tu ya from four failures nao wanaweza kuwa Makomando.
 
Hapo awali shahidi huyu alisema anayo ruhusa toka kwa wakuu wake wa kazi kuja kutoa ushahidi, ingawa movement order hakuja nayo mahakamani ameiacha hotelini. Sasa Hiyo Court Martial inakuja vipi hapa?
Nashon kamuuliza uliwezaje kuwa Luteni? Kumbuka elimu yake ni 4m4 hivyo alipaswa kuishia kuwa korokoro mwenye logo ya bibi na bwana tu. Mara nasimamamia askari 30 kwa platoon, kweli huyu hajafanya senior course. Cheo chake huyo ni coplo tu na sio luten
 
Kwa hiyo platoon inakuwa na askari 30? Huyu mwanajeshi wa wawapi,mpakani au fire? Kama section 1 inakuwa na askari 9 na kila platoon inakuwa na section 3 hiyo idadi ya askari 30 ametoa wapi?

Kama nyota 2 hajui vipi kwa staff sajent wake atakuwa anajua nn? Huyu hajatoka kikosini tokea akamatwe na madoso aliyokula ndio hizo zimemwongezea mtero(hofu)mahakamani
Usikariri Bro. Kwenye Organization ni kweli kuna idadi tajwa lakini haimlazimishi mtu kuifuata. Ndio maana kuna - or +. Unaweza kutengeneza Organization itakayo fit hitajio lako.
 
Zamani nilikuwa nikisikia Komando nilikuwa nafikiri ni Maafisa fulani ambao wamekuwa trained kwenye kiwango cha juu .... Kumbe ni design tu ya from four failures nao wanaweza kuwa Makomando.
Ukomando ni wanajeshi wa kawaida tu na wengi wao ni private yaani askari mtendaji na ndio maana maofisa wachache sana wanakuwa. Komando ni mtu wa kutumwa na ndio maana unaona hata wanavyofanyiwa hao akina Adamoo na hawaheshimiki kabisa ndani ya jeshi, kupewa privilege ya kupanda ndege bure ndicho kitu pekee kinawatia kiburi
 
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall



KAZI IPO

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Nashangaa Jana alijibu maswali ya wakili Wa serikali yeye nani anaongoza watu wangapi akajibu na dafouu walikuwa wanakaa nani ajibu viongozi mpaka asema alikuwa anawalinda viongozi Leo anakataakujibu aibu tupu kwanza ana dhambi huyu Urio wachomeka watu aliodai ni Rafiki zake watoto na family zinateseka
 
Back
Top Bottom