Salaam Wakuu,
Leo tarehe 13/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.
Kufahamu ilipoishia, soma hapa:Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
UPDATES:
Jaji ameingia, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha
Pius Hilla Abdallah
Chavula Jenitreza
Kitali Nassoro
Katuga Esther
Martin Tulimanywa
Majige Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala, nipo pamoja na wakili:
Jeremiah Mtobesya
John Mallya Dickson
Matata Seleman
Matauka Faraji
Mangula Gaston
Garubindi Maria
Mushi Khadija Aaron
Jaji anaita washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika kuwa wapo Mahakamani
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja na sote tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea
Jaji: atakuwa ni Shahidi Wa Ngapi huyo?
Wakili wa Serikali: Robert Kidando atakuwa Shahidi Wa 09 Mheshimiwa Jaji Shahidi anaingia ni Mdada amevaa Miwani Mweupe na Mrefu Kidogo Kavaa Koti la blue
Jaji: Majina yako
Shahidi: Gladisi Fimbari
Jaji: Miaka
Shahidi: 36
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Jaji: Kazi yako
Shahidi: Mwanasheria kampuni ya Airtel_Tanzania
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakaotoa utakuwa ni Kweli, kweli tupu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ataongonzwa na Jenitreza Kitali
Wakili wa Serikali: unafanya Kazi wapi
Shahidi: Nafanya kazi Airtel Tanzania
Wakili wa Serikali: Unafanya Kazi kama nani
Shahidi: Nafanya kazi Airtel PLC
Wakili wa Serikali: Kama Nani
Shahidi: Awali niliajiriwa Kama Afisa wa Sheria. Baadae 2021 Mwezi March nilibadilishwa Cheo na Kuwa Meneja Kitengo cha Sheria
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kampuni ya AIRTEL PLC inajihusisha na nini
Shahidi: Inajihusisha Na Kupiga na Kupigiwa Simu, Huduma ya Miamala ya Fedha kupitia Airtel Money
Wakili wa Serikali: Sasa hiyo Kampuni ya AIRTEL PLC Inatoa hizo huduma kwa Watu gani
Shahidi: Ili Upate Huduma Kutoka Airtel TEL lazima uwe na Simu Handset na lazima uwe na Simcard ya AIRTEL\
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi tueleze huyo Mteja anapataje hiyo simcard ya AIRTEL?
Shahidi: Ili uweze Kuwa Mteja lazima ufike katika Ofisi za Airtel au Kwa Mawakala wa Airtel utanunua Sim Card lakini Baada ya Hapo lazima ufanyi we Usajili wa ile Line
Wakili wa Serikali: Sasa Mteja amemunua Sim Card ya AIRTEL Lazima afanye Usajili, Je Usajili unafanyikaje
Shahidi: Lazima Mteja awepo katika Usajili, atajitambulisha Majina yake yote, lazima awe na Kitambulisho Chake cha Taifa yani NIDA card, anaye Msajili atachukia hiyo namba na Kuingiza Katika Mifumo yetu, Kisha Atatakiwa aweke Dole Gumba na Kisha Msajili wetu atafanya Uhakiki (Verification) Kupitia Mifumo ya NIDA ambayo imeunganishwa na Mifumo yetu ya NIDA Baada ya Verification na Uhakiki atapata Namba ya NIDA Kuhusiana na Mifumo yetu, baada ya Kupata Uhakiki Kutoka NIDA, Taarifa Zote zitaifadhiwa Katika Mifumo yetu na Baada ya Hapo Usajili utakuwa Umekamilika..
Wakili wa Serikali: Ifafanulie Mahakama Vizuri, umesema Afisa Usajili Wa Airtel atafanya Uhakiki Kutoka NIDA, JE Afisa Wenu Usajili anapataje Taarifa Kutoka NIDA na Kuingiza Katika Mifumo yetu, Kisha Atatakiwa aweke Dole Gumba na Kisha Msajili wetu atafanya Uhakiki (Verification) Kupitia Mifumo ya NIDA ambayo imeunganishwa na Mifumo yetu ya NIDA Baada ya Verification na Uhakiki atapata Namba ya NIDA Kuhusiana na Mifumo yetu, baada ya Kupata Uhakiki Kutoka NIDA, Taarifa Zote zitaifadhiwa Katika Mifumo yetu na Baada ya Hapo Usajili utakuwa Umekamilika..
Wakili wa Sehemu: Ifafanulie Mahakama Vizuri, umesema Afisa Usajili Wa Airtel atafanya Uhakiki Kutoka NIDA, JE Afisa Wenu Usajili anapataje Taarifa Kutoka NIDA
Shahidi: Ok, Ni kwamba Mifumo Yetu imeunganishwa...........
Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Huyu shahidi ameingia akasema yeye ni Mwanasheria Hakuna Mahala yoyote ameongozwa Kusema Kama Ana utaalam wa Usajili..... Kwa Maoni yetu hiyo ni "HEAR SAY"
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ni mapema kwa Wakili kuibua Hiyo Hoja kama ni Hearsay au Lah
Jaji: Kwa nini Unasema ni Hearsay
Kibatala: kwa Sababu Yeye hajasema anafanya Jukumu la Usajili, Bali kasema Kuwa yeye ni Mwanasheria, Hakuna Mahala kasema ni Jukumu lake Kusajili
Jaji: Kwani Hearsay ni nini
Kibatala: Ni Jambo lolote ambalo halitoki Kwa Shahidi Bali kwa Third Party, Ndiyo Maana anasema Juu ya Afisa Msajili ambaye siyo yeye
Jaji: Mimi nafikiri ni Mapema Sana Kusema Ni Hearsay kwa sababu bado anaendelea Kutoa Ushahidi Wake
Wakili JEREMIAH MTOBESYA: Napata taabu Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Shahidi Msingi Wake unajengwa na Matukio, Hakuna Mahala kasema Kama alishawahi Kupata Training au Lah, anachotoa Ni opinion tu....
Jaji: Sasa Si mtamuuliza Maswali Baadae Katika Kumuuliza Maswali, Kwa sababu Hatuwezi Kusema Tuukatae Ushahidi Wa Namna hii, Ni Hatari Kama Kila Shahidi akija Tuukatae Ushahidi Kwa sababu Hana Knowledge Ya Kutosha
JEREMIAH MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji ni Hatari Sana Mbele Ya Sheria, Tufuate Sheria Inasemaje
Jaji: ninyi Mtapata Nafasi ya Kumfanyia Cross Examination, Tusubiri wakati huo
Wakili wa Serikali: Tuendelee Gladisi....
Shahidi: Majukumu yangu ni Kutoa Ushauri Juu ya Mambo Mbalimbali ya Kisheria, Lakini pia Kuandaa Tathimini Za Kisheria, Kuandaa Nyaraka Za Kisheria, Kufuatilia Kesi zinazohusu Kampuni ambazo zipo Mahakamani, Pia natoa Taarifa ninapoombwa, Juu ya Taarifa, za Kiuchunguzi Kwa Taasisi za Kiuchunguzi au Baada ya Kupokea Amri ya Mahakama Na hiyo Ndiyo Taarifa yangu Kwenye Maeneo hayo
Wakili wa Serikali: Sasa ieleze Mahakama Juu ya Mfumo wa MOBIQUIT Jinsi unavyofanya kazi katika Utunzaji Wa Kumbukumbu za Miamala
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Una Elimu gani ambayo inakuwezesha Kutekeleza Majukumu uliyo taja
Shahidi: Nina Shahada ya Sheria, Niliyopata Mwaka 2006 Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Nina Certificate ya Basic Skills za Computer ambayo nimepata Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UCC
NA pia nilipojiunga Airtel Mwaka 2004 nilipata Mafunzo ya Ziada ya Mifumo ninayotumia katika Majukumu yangu Nilipata Mafunzo ya Mfumo wa MOBIQUIT Kwa ajili ya Kuhifadhi Taarifa za Miamala Ya Fedha inayofanywa na Mteja Mafunzo hayo niliyapata Kwa muda Wa Wiki Mbili Airtel
Nilijifunzwa Mafunzo kuhusiana na Bussiness Intelligence, Mfumo ambao unatunza Mawasiliano ya Mteja Nilipofika Mwaka 2018/2019 nilipata Mafunzo ya Mfumo Unaitwa AGILE huu ni Mfumo wa Kutunza Taarifa za Usajili Wa Mteja wa Ki BIOMETRIC
Katika Mifumo hiyo tunafundishwa Mambo Mbalimbali Ikiwamo Jinsi Taarifa inavyo chukuliwa na Kuhifadhi wa katika Mifumo hiyo Usalama wa Mifumo Endapo Kuna tolea tatizo la Kimtandao au tatizo la Kiteknolojia ni nini tunatakiwa kufanya na Utuzanji Wa zile Taarifa
Na hiyo Ndiyo Taarifa yangu Kwenye Maeneo hayo
Wakili wa Serikali: Sasa ieleze Mahakama Juu ya Mfumo wa MOBIQUIT Jinsi unavyofanya kazi katika Utunzaji Wa Kumbukumbu za Miamala
Shahidi: Kama Nilivyotaja Mfumo wa MOBIQUIT, Mfumo huu unatunza Taarifa za Miamala pale ambapo Mteja anatuma au Kupokea Pesa Automatic, Mfumo unachukua Zile Taarifa Na Kwenda Kuzihifadhi Kwenye Sever na Baada ya hapo, Ilikuweza Kuzifikia hizi Taarifa unatumia Mfumo
Wakili wa Serikali: VIpi kuhusiana na Mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE unafanyaje kazi
Shahidi: Pale ambapo Mteja anafanya Mawasiliano, Akiwa Karibu na Mnara, Automatically Mawasiliano Yake Yanachukuliwa Kupitia Mifumo na Kwenda Kutunza Kwenye Sever, Baada ya hapo Unapotoa Kuzifikia Hizi Taarifa Ndipo unatumia Mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama ni Mawasiliano ya Namna gani Mfumo huu ndiyo unafanya kazi
Shahidi: Anapopiga simu, anapotuma Ujumbe Mfupi, anapopokea Simu na anapotaka Huduma za Internet, inakuwa Captured kwenye Mfumo wetu
Wakili wa Serikali: Shahidi Umetaja Mfumo Mwingine Wa AGILE Ifahamishe Sasa Mahakama ni Kitu gani

Shahidi: Kama Nilivyoeleza Kuwa Mfumo wa AGILE unafanya kazi Mteja anapotaka Kwenda Kusajili Line yake, anapotaja Namba ya Utambulisho Wa NIDA Msajili anaingia namba za NIDA kwenye Mfumo, na Baada ya Taarifa hizi Mteja Kuweka Kidole Gumba zinakwenda Kuhakikiwa NIDA na Majibu Yatakurudi Kisha Taarifa Hizo zinaenda Kuhifadhi wa katika Mfumo wetu wa AGILE
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama, Ka wewe ni Mtumiaji wa hii Mifumo ni Kwa Muda gani Umetuma Hii Mifumo
Shahidi: Kwa Upande wa MOBIQUIT na BUSSINESS Intelligence Niliweza Kutumia Mifumo hii tangu Nipo Jiumga na Airtel Mwaka 2004 na Kwa Upande wa AGILE ni tangu Mwaka 2019 Mpaka Sasa
Wakili wa Serikali: Sasa Wakati wa Ushahidi Umeeleza Mahakama Majukumu yako, Na Moja ya Majukumu yako ni Kutoa Taarifa Chunguzi kwa Vyombo Vya Uchunguzi, Ifahamishe Mahakama Taarifa unazo toa ni Kwa vipi na zipi
Shahidi: Kwanza Nikianza, Tunatoa Kwa Jeshi la Polisi, Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB, Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya, Mamlaka ya Mawasiliano na Financial Intelligence, na pale Mteja anapohitaji Kupewa Taarifa zake anaruhusiwa Kupewa
Wakili wa Serikali: taarifa ya namna gani?
Shahidi: Kila Taasisi Zinaomba Taarifa za Mawasiliano Kwa Ujumla nikimaanisha Kupiga na Kupokea Simu, Miamala ya Fedha na Pia Usajili wa line
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Utaratibu Wa Maombi huwa Unafanyikaje
Shahidi: Taratibu Kubwa ni Chombo Chunguzi Kuleta Barua ya Maombi ya Taarifa, Na Maombi haya Yana Wasilishwa Airtel Kupitia Upande wetu wa Mapokezi Ya kisha pokelewa yanaratibiwa Katika Register Yetu na Kupelekwa kwenye Kitengo Cha Sheria Kufanyiwa kazi na Baada ya Hapo Mkuu wa Kitengo Cha Sheria anatoa Ruhusa Kwa Muhusika Juu ya Kufanyia Kazi Maombi hayo
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Barua ya Maombi Imeshafika na Mkuu wa Idara ameshasaini, Sasa Huyu aliye na Barua anafanya nini kazi
Shahidi: Lazima afanye Kazi Barua Kwa Kujiridhisha Kwanza, Juu ya anuani ya Taasisi Kama Barua hiyo Imeelekezwa kwa Airtel? , Je Barua hiyo Ina Nembo ya Taaaisi husika? , Taarifa hizo ni za Kiuchunguzi? Na Kama siyo Za Kiuchunguzi haiwezi Kufanyia Kazi, lakini Pia iwe na Sahihi na Muhuri Wa Taaaisi Husika
Wakili wa Serikali: Umesema Afisa Anahakiki Vitu Vyote ikiwemo Taarifa ya Kiuchunguzi, Nini Unaangalia Kujua Kama Kiuchunguzi au siyo
Shahidi: Barua zote za Kiuchunguzi zinataja Kosa. Kuna ambazo zinataja Jalada namba Ili Kuonyesha Kwamba Kuna Kesi inaendelea
Wakili wa Serikali: Ni watu gani hasa sasa wanao fanyia kazi Maombi
Shahidi: Ni watu wa Kitengo Cha Sheria
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Kitengo cha Sheria ni watu Wangapi Wanashughulikia hizo kazi
Shahidi: Ni watu Wawili ambapo ni Mimi na Mwenzangu
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Assignment Imefika Mezani Kwako na Maombi yote Umepangwa yamefuata Utaratibu
Shahidi: Ofisini Kwangu Kumeanganishwa na Mifumo Niliyotaja Kupitia Computer Yangu yangu MOBIQUIT, BUSSINESS INTELLIGENCE NA AGILE. Na Kila Mfumo ni Credentials zangu za Kuniruhusu Kuingia Kwa Kila Ninapo ingia
Wakili wa Serikali: USER name Unapata wapi?
Shahidi: Kitengo Cha IT ambapo ni Mimi Mwenyewe na Kitengo Cha IT Hakuna Mwingine anayefahamu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuingiza hizo Credentials Kitu gani kinafuata
Shahidi: Mfumo wenyewe Unakuletea Sasa sehemu Ya Kuingiza Namba ya Simu ya Mteja lakini pia Muda ambao Unataka zile Taarifa Na automatically Mfumo wenyewe Unachakata zile Taarifa na Kuleta Katika Computer Yako
Wakili wa Serikali: Taarifa zinachakatwa na Zinakuja Kwenye Page yako (Computer Yako) Je Zinakuwa zimehifadhiwa wapi
Shahidi: Zinakuwa zimehifadhiwa Katika saver, zinahifadhiwa na Mfumo
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Taarifa Ku Display katika Page yako nini Kinafuata
Shahidi: Baada ya Hapo Ni Uhakika Wa Taarifa ukitoka Katika Mfumo na Taarifa Husika Kama Ni Namba husika, Je ni sahihi na Kama Vile Unavyotaka, Kisha Nina Print Taarifa
Wakili wa Serikali: Sasa Ukiisha Print Kitu gani kinafuata
Shahidi: Nilisha Print Inafanya tena Uhakiki
Wakili wa Serikali: Uhakiki wa Namna gani
Shahidi: Kwa Kulinganisha na Barua ya Maombi, Nagomga Muhuri na Kusaini pamoja na Kuweka Tarehe, Kisha naandaa Cover Later Kwa ajili ya Kuambatanisha Taarifa hizo
Shahidi: Ni naweka Vizuri na Kuiwasilisha Kwenye Mamlaka husika Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Umesema Hapa Mahakamani Kwamba Wewe huwa Unapewa Credentials na Watu wengine Kuwezesha Kuingia Katika Mifumo, Je ni watu Gani Wengine Katika Taasisi yenu
Shahidi: Kuna Watu wa aina Mbili, Watu wa Call Centers, Watu Wa Customer Care hawa Ndiyo wenye Uwezo wa Kuona, Kama Nilivyosema Kwa Ajili ya Kuhudumia Wateja Kwa ajili ya Kuona Miamala Kama Imekosewa au lah. Na Watu wengine ni Watu wa Ku Extract Zile Taarifa, Huyu ni Mtu pekee Kutoka Kitengo Cha Sheria
Wakili wa Serikali: Sasa huyu Mtu aliyepewa Uwezo Wa Kuingia na Kuona zile Taarifa, Ni Kitu gani Kingine anaweza Kufanya katika Taarifa
Shahidi: Huyu aliyepewa Access ya Kuona hana Uwezo wa Kufanya lolote zaidi ya Kuona, Kwani Taarifa hizo Zinakuwa katika Mfumo wa READ ONLY (kuweza Kusoma tuh)
Wakili wa Serikali: Hawa watu wenye Uwezo wa Kuona tuh ni watu wa Idara zipo.?
Shahidi: Ni watu wa Customer service pamoja na Call Center, na Wale ambao Wapo Kwenye Kitengo Cha IT
Shahidi: Kundi la 2 Ni Kitengo Cha Sheria, Sisi tumepewa Uwezo Wa Kuona na Ku print lakini pia hatuna Uwezo Wa Kufanya chochote Katika ile Taarifa, na sisi Pia inakuja kwa mfumo wa READ ONLY
Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeeleza Mahakama Juu ya Mifumo, Je umadhubuti wa Hiyo Mifumo Ikoje
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Taarifa zetu ni Automatic generator Designated, Hakuna Mtu Anayeweza Kuzalisha Taarifa za hiyo Mifumo, Mifumo hiyo pia inalindwa kwa kuwekwa software za Usalama (Firewalls) kwa Kulinda Usalama wa Mifumo na Taarifa Endapo Imetokea Muingilio wa aina yoyote
Mifumo hiyo pia inafanyiwa SYSTEM AUDIT Mara kwa mara Kuangalia Uimara wake, Lakini si Kila Mtu ana access ya hii Mifumo, Ni baadhi ya Watu ambao Wamepewa Credentials ambazo Zinawaruhusu Kuingia katika Mifumo.
Lakini Mifumo hii Imeunganishwa na AIRTEL Kwa Maana Hauwezi kuwa Mahala Popote Kuingia katika Mifumo hii, Lakini pia Uwezi Kutumia Kifaa Chochote Kuingia Katika Mifumo yetu
Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Sababu ya Kutoingia Ukiwa popote
Shahidi: Katika Mifumo yetu Mtu hawezi Kuingia pasipo Kuwa na Kifaa Ambacho Kinatambulika na Airtel Kuweza Kuingia Katika Mifumo yetu
Wakili wa Serikali: Unaposema Kifaaa/Vifaa ni Vya Namna gani
Shahidi: Namaanisha Computer yaani Desktop au Laptop
Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaelezea Umadhubuti wa Hiyo Mifumo, Je ni Kitu gani Kingine
Shahidi: Kwenye Mifumo Hii lazima Uwe na Hivyo Vifaa ambavyo vimeunganishwa na Airtel na siyo Kila Mtu anaweza Kuingia katika mifumo
Wakili wa Serikali: hiyo Mifumo inausalama gani Kuhakikisha nyie watumiaji na Mliyotumia ni Salama
Shahidi: Kwanza Kuna software ambazo ni Firewall ambazo zitatambua endapo Kuna Mtu anajaribu Kutaka Kuingia, Na Lakini pia Endapo Patakuwa na Tatizo la kimtandao zile Taarifa haziathiriwi Kwa Namna yoyote
Wakili wa Serikali: Unaposema Kifaaa/Vifaa ni Vya Namna gani
Shahidi: Namaanisha Computer yaani Desktop au Laptop
Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaelezea Umadhubuti wa Hiyo Mifumo, Je ni Kitu gani Kingine
Shahidi: Kwenye Mifumo Hii lazima Uwe na Hivyo Vifaa ambavyo vimeunganishwa na Airtel na siyo Kila Mtu anaweza Kuingia katika mifumo
Wakili wa Serikali: hiyo Mifumo inausalama gani Kuhakikisha nyie watumiaji na Mliyotumia ni Salama
Shahidi: Kwanza Kuna software ambazo ni Firewall ambazo zitatambua a endapo Kuna Mtu anajaribu Kutaka Kuingia, Na Lakini pia Endapo Patakuwa na Tatizo la kimtandao zile Taarifa haziathiriwi Kwa Namna yoyote
Wakili wa Serikali: Na Je Utendaji Kazi wa Huu Mfumo Ukoje
Shahidi: Mfumo wetu ni Madhubuti na hauna hitilafu yoyote, na Inapotokea pale unapoingiza Credentials, kuwa Kuna tatizo na huwezi Kuzifikia Taarifa za Mteja
Wakili wa Serikali: Nini Kinatoa Endapo network inakuwa Chini kwa Taarifa mnazotunza
Shahidi: Network Inapokuwa Down Haiathiri Vile Vilivyomo Ndani, Pale ambapo imerekebishika unaweza Kupata Taarifa
Wakili wa Serikali: Na Kurudisha Nyuma, Ulisema wakati wa Usajili Mteja anaweka Dole Gumba katika Kifaa Je Hilo Kifaa Kinaitwaje
Shahidi: Msajili anakuwa na Vifaa Viwili, Handset na Kifaa cha Dole Gumba ambapo Airtel tunatumia Kifaa Kinaitwa FALOPO
Wakili wa Serikali: Kuna Suala la Intergrity ya Mfumo (uadilifu wa Huo Mfumo) ukoje
Shahidi: Mfumo Wetu sisi ni Automatic generated, Hakuna Taarifa ya Ziada ya Kuongeza, Mifumo yetu Inafanya kazi Vizuri, Tuna Vifaa (software) ili Kusaidia Usalama wa Hiyo Mifumo
Wakili wa Serikali: Intergrity ya Vifaa Mnavyotumia Ofisini Ukoje
Shahidi: Tunatumia Desktop au Laptop, Ambapo Vifaa Hivi vimeunganishwa na Mifumo ya AIRTEL Na uwezi Kufanya lolote, Vifaa hivi vimeunganishwa na Mifumo ambayo inatoa ALERT pale ambapo unafanya Kinyume
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa hiyo Mifumo NI Mifumo ipi
Shahidi: Mifumo ya Kuweza Kupata Taarifa za Mihamala ni MOBIQUIT kama Nilivyo eleza Ni Mfumo wa Kuchukua Taarifa na Kuhifadhi Miamala
Shahidi: Mfumo Mwingine ni AGILE ambapo Mteja anapofika Dukani na Kufanya Usajili, Basi Uhakiki wa Taarifa Hizo, Zile Taarifa zinaenda Kuhifadhi wa Kwenye Mfumo wa AGILE, Na Kupitia Mfumo huo unaweza Kuzipitia Taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Ieleze Mahakama Mnamo Tarehe 02 July 2021 ulikuwa wapi
Shahidi: Mnamo tarehe 02 July 2021 nikiwa Ofisi za Airtel Morocco Nikiwa nafanya Majukumu yangu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Morocco ipo Maeneo gani
Shahidi: Ofisi za Airtel Zipo Morocco hapa hapa Dar es Salaam ambapo Ndipo Kitengo Cha Sheria Kilipo
Wakili wa Serikali: Sasa Wakati Upo Ofisini Kwako Kilitokea Kitu gani
Shahidi: Wakati naendelea na Majukumu yangu ya Sheria, Mkuu wetu wa Idara alini assign Kushughulikia Maombi ya Taarifa
Wakili wa Serikali: Maombi hayo yalitaka nini
Shahidi: Kushughulika na Maombi ya Miamala Ya Fedha ya Namba 0782237913, 0787555200, 0784789944 pamoja na Taarifa za Miamala Iliomba Pia na Taarifa za Usajili

Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Maombi hayo Ulifanya Kitu gani
Shahidi: Nilihakiki Barua kama Imetoka Kwenye Taasisi Husika, ya Uchunguzi Wa Kisayansi, Barua ilikuwa inaongelea Taarifa ya Kiuchunguzi na niliangalia Taarifa Gani inayoombwa, Nilihakiki kama Imegongwa Muhuri Wa Taaaisi Husika
Shahidi: Baada ya Kujiridhisha nili ingia Kwenye Kifaa Changu cha Kazi ambacho ni Computer, Kisha Nikaingia Kwenye Mfumo wa AGILE, Na Mfumo huo Ulifanya kazi Vizuri nikaingiza namba Moja ya Simu ambayo imeombewa Taarifa, na Kisha ikanitolea Taarifa Husika Baada ya Kuchakata
Wakili wa Serikali: Taarifa Inayohusiana na Nini?
Shahidi: Taarifa ambayo Nimeomba Kuhusiana na Zile namba tatu nilizo zitaja awali
Wakili wa Serikali: Kwenye Barua Iliombwa Taarifa za Miamala Ya Fedha na Usajili, Hapa Unaomgelea Kuingia Kwenye Mfumo wa AGILE Je Ulipata Taarifa Ipi
Shahidi: Nilipata Taarifa za Usajili Wa Namba
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu namba zingine
Shahidi: Hiyo ilikuwa Kwa namba 0784789944 ni kafanya kwa namba ya Pili 0782237913 na Ni kafanya Vilevile Kwa namba ya tatu 0787555200 ambapo Zote nilipata Usajili wa Namba hizo Nika Print
Wakili wa Serikali: Kitu gani Ulifanya Baada ya Kupata hizi Nyaraka
Shahidi: Niliingia Tena Katika Mfumo Wa MOBIQUIT ambapo ni lazima Uinhize Namba na Muda, Tofauti na Ule Mfumo wa AGILE
Wakili wa Serikali: Sasa Kwa Namba hiyo Uliyotaja Unasema iingiza namba na Muda, endelea
Shahidi: Nilipo ingia Namba na Muda, Window Yangu ya Computer Ikaniletea Zile Taarifa,.
Wakili wa Serikali: Baada ya Taarifa hizo Kuja Nini Ulifanya
Shahidi: Nilihakiki tena, Ile namba ambayo imeombewa Taarifa, na baada ya Kujiridhisha nili print na Nikaendelea Kwa Namba Nyingine
Wakili wa Serikali: Nini Kilifanyika Baada ya Zoezi hilo
Shahidi: Baada ya Ku print Kwanza Niligonga Muhuri Wa Airtel Katika Nyaraka zote, Kisha Nikaweka Sahihi Pamoja na Tarehe Lakini Pia Niliandaa Barua (Cover Later) ambayo niliambatanishia Taarifa
Wakili wa Serikali: SASA ieleze Mahakama Hali ya Hiyo Mifumo Uliyotumia Siku hiyo Kama ilikuwa Inafanya kazi Vizuri
Shahidi: Mifumo Hiyo ilikuwa Inafanya Kazi Vizuri, Hapakuwa na Tatizo la Kimtandao na Hakukuwa na Changamoto yoyote Wakati na Print hizo Taarifa
Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusiana na Kile Kifaa Kazi ambacho Ulikuwa unakitumia
Shahidi: Kifaa Kilikuwa katika Hali Nzuri na Hakikuwa na Tatizo lolote wala Changamoto Yoyote na Endapo Kingekuwa na Tatizo lolote Basi Pale ambapo Unaingiza Credentials zingakukatalia na Kukutaarifu Kuna tatizo, lakini Katika Kifaa Changu Hapakuwa na Tatizo hilo Siku hiyo
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuandaa hizo Taarifa na Kuweka Cover Later nini Kilifuata
Shahidi: Baada ya Hapo Ni Wasilisha Taarifa hizo Ofisi ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Hizo Nyaraka Ukiziona Hapa Mahakamani Unaweza Kuzikumbuka
Shahidi: ndiyo
Wakili Wa Serikali: Eleza Utajuaje
Shahidi: Niliandaa na Cover later Niliyo andaa Ilikuwa na Logo ya Airtel, Zile Taarifa, Katika Cover Later hiyo Kuna Jina Langu, Sahihi Yangu na Muhuri Wa Airtel
Katika Cover Later hiyo niliambatanishia Barua ya Maombi Kutoka Ofisi Ya Uchunguzi ya Tarehe ya 01 July 2021 ambayo Inaonyesha Jalada namba ilikuwa ni CD/IR/2097/ 2020 lakini pia Ina namba 3 ambazo ziliombewa Taarifa ambazo 0787555200, 0782237913, 0784779944
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Zile Taarifa Za Usajili Wa Namba za Simu. Kitu gani Kitakufanya Ukiziona Uzikumbuke
Shahidi: Taarifa hizo Zina namba ya Simu, Majina yangu na Signature Yangu na nimegonga Muhuri Kwa Barua zote pamoja na Tarehe

Wakili wa Serikali: Taarifa ya Kwanza Ambayo utaweza Kuitambua ni ya namba Ipi
Shahidi: Taarifa ya Kwanza ni 0787 555200 Ya Pili ni 0782 237913 Namba ya Mwisho ni 0784789944
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu Taarifa za Miamala
Shahidi: Kuna Taarifa Ya Miamala Ina Jina Langu, Sahihi Yangu, Muhuri Wa Kampuni na Tarehe
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Wetu Nyaraka hizo
Wakili wa Serikali: Angalia hiyo Nyaraka na Uniambie ni Kitu gani
Shahidi: Nyaraka Mkononi Mwangu ni Cover letter ambapo Inaonyesha Anuani
Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka Hizo Unazitambua au huzitambui
Shahidi: Cover letter Hii naweza Kuitambua Kwa Sababu Zifuatazo Kwa Sababu ina anuani ya Kampuni ya AIRTEL, Ina namba Ambazo zimeombewa Taarifa, Ina Jina Langu, na Muhuri Wa Airtel
Shahidi: Nyaraka Inayofuata ni Barua KUTOKA Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi, na Nimeitambua Sababu, ina Namba ya Jalada Niliyo taja, Ina Muhuri Wa Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi.
Shahidi: Lakini pia akuna Taarifa za Usajili Ambazo Zina namba Iliyo ombewa Taarifa, Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe
Wakili wa Serikali: Unasema Kuna namba ambayo Umetaja Mwanzoni, Ni ipi
Shahidi: Ni 0784789944, Kuna Taarifa Ya Usajili Pia wa Namba 0782237913
Wakili wa Serikali: Umeitambuaje
Shahidi: Kutokana na hiyo Namba lakini Pia Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Shahidi: Ni 0784789944, Kuna Taarifa Ya Usajili Pia wa Namba 0782237913 Wakili wa Serikali: Umeitambuaje Shahidi: Kutokana na hiyo Namba lakini Pia Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Unaiomba Nini Mahakama Kuhusiana na Nyaraka Zote Hizo hapa Mahakamani
Shahidi: Naiomba Ipokee Kama Vielelezo NYARAKA ZINA PELEKWA UPANDE WA UTETEZI Jopo la Mawakili Wa Utetezi Wanazizunguka na Kuanza Kuzichambua
Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Kwanza Hatuna Pingamizi Kwa Kuzingatia Haki ya Kufanya Cross Examination
Wakili John Mallya: Kwa Upande wangu sina OBJECTION
Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande Wangu sina Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Nne hatuna Pingamizi NYARAKA ZINATOKA UPANDE WA UTETEZI ZINAENDA JUU KWA MHESHIMIWA JAJI KUPITIA WASAIDIZI WAKE Jaji anazitizama Mahakama Bado ipo Kimyaaaa
Jaji: tuliishia Kielelezo Namba 14, Si Ndiyo..? Wnaitika NDIYOO!
Bado Mahakama ipo kimya, nyaraka zote kutoka airtel Tanzania kama Ushahidi katika kesi hii ya Jamhuri Vs. FREEMAN Mbowe na wenzake watatu, zipo pale Juu kwa Jaji anazipitia na kuandika masuala yake...
Jaji: Kwa Maana Riport za Transactions ni Namba Mbili Siyo tatu, Si Ndiyo..?
Kibatala: kwa Maana Print Out au Barua Kutoka Airtel.?
Wakili Peter Kibatala: Na sisi tumeona Mbili Jaji Kwa Hiyo Kwenye Registration ni Namba 3 ila Kwenye Transactions ni Namba 2
Jaji: Basi Mahakama Inapokea Vielelezo Kama Ifuiatavyo Barua ya Kwenda Ofisi ya Uchunguzi no Kielelezo namba 15 Barua ya Kuomba Taarifa ni Kielelezo 16 Taarifa Usajili ya 0784789944 ni Kielelezo namba 17 Taarifa ya Usajili ya namba 0782237913 ni Kielelezo namba 18
Taarifa ya Usajili ya namba 0797555200 ni Kielelezo namba 19 Taarifa ya Miamala ya Namba 0787555200 ni Kielelezo namba 20 Taarifa ya Miamala ya Namba 0784789944 ni Kielelezo namba 21 Mawakili wa pande zote 2 wanakubaliana na Uamuzi Jaji na Kusimama. Na Kuinama
Jaji: Sasa taarifa zote zinatakiwa kusomwa na Shahidi kama ulivyo utaratibu
Shahidi ameanza kusoma barua ya Airtel Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi Wa Kisayansi Shahidi anasoma sasa barua kutoka Ofisi ya uchunguzi wa kisayansi maombi ya taarifa
Shahidi: anasoma Taarifa ya Usajili wa namba ya Usajili wa Namba 0784789944 Shahidi sasa anasoma taarifa ya usajili wa Namba 0782237913
Shahidi anasoma taarifa ya Usajili wa Namba 0787555200 namba ya Luten Denis Urio
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kielelezo kinachofuata cha Mihamala ya Namba 0787 555200, Tusomee Miamala ya Tarehe 20 July 2020
Shahidi: Muamala wa Kwanza wa Tarehe 20 July 2020 Namba ya muamala, namba Iliyotuma ni 0784789944, Receiver ni 0787555200 kiasi Kilichotumwa ni TSh 500,000
Wakili wa Serikali: Naomba Utusomee Muamala Wa 22 July 2020
Shahidi: Kuna Miamala mitatu
Wakili wa Serikali: Naomba Utusomee Muamala Wa Pili wa 22 July 2020
Shahidi: Transactions, Muamala Umetoka 0780900244 ametumiwa TSh 199,000 akawa na Jumla ya Tsh 300,000. Kwenda 0787555200
Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kielelezo kinachofuata cha Mihamala ya Namba 0787 555200, Tusomee Miamala ya Tarehe 20 July 2020