Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Shahidi: alikuwa ananiambia nitaje tena Majina ya wale Vijana na Namba zao za simu na kazi wanazozifanya kwa Sabaya

Wakili wa Serikali: Wewe baada ya kukutaka Ufanye hivyo Ulichukua hatua gani

Shahidi: Kabla ya kuanza kuwataja nikamtaka Mlinzi wake akachukue kalamu na Karatasi ilituweze kuandika
Ha ha ha, eti nilimtaka mlinzi wake achukue kalamu na karatasi ili waandike duh aisee
 
Naona mwenye chair ushahidi unamkaanga..sion possibility ya yeye kuchomoka asee...
 
Hii kesi haina ukweli wowote
Shahidi: Mbowe, Halfani Bwire, Mohamed Ling'wenya na Adamu Kasekwa kwa sasa wako hapa mahakamani. Wakili wa Serikali Chavula anamtaka shahidi awaoneshe kwa majina na Shahidi anawasogelea na kuwataja kwa majina.

Shahidi: Akianza na Halfan Bwire, Adamu Kasekwa, Mohamed Ling'wenya na Mbowe. Kisha anarejea kizimbani.
 
Mbowe sio gaidi
Mbowe siyo gaidi lakini ni mkaidi, ikiwa tumefiwa na raisi aliyekuwa madarakani, je itashindikana kwa kiongozi wa chama cha upinzani?

Wapinzani watumie busara katika kudai katiba mpya, tume huru na ya haki ya uchaguzi, mikutano ya hadhara ya kisiasa, bunge na mahakama zisizoingiliwa katika utendaji wake n.k.

Tubadilike ifike mahala tufanye siasa za kistaarabu zisizokuwa na chuki wala kudhuruiana.
 
Joyce mukya daah mwamba alimpenda sana kimada
 
Kwa hiyo Mbowe alikuwa anapanga ugaidi na kumdhuru Sabaya kwa kuongea moja kwa moja na huyo mbeba chai ambaye hata nauli hana? waliopewa jukumu la kubambika hii kesi wamefanya kazi ya ovyo sana wafukuzwe tuu
 
Eti huyo Kaaya aliambiwa akae upande wa kulia wa barabara, na gari ya Mbowe ilipofika, kioo cha upande wa abiria kikashuka ndipo akamuona Mbowe. Kama gari ni tinted, kioo cha abiria kikishushwa halafu wewe upo upande wa kulia utaweza vipi kuona ndani?

Halafu eti alichukuliwa kama mpiga picha na baadaye akaishia kuwa house boy wa Sabaya! Yani alipenda kazi yake ya kupiga picha akamuhamishia nyumbani kwake kabisa.

Duh! Haya mazingaombwe matupu.
Sabaya alikuwa anamtafuna huyu kilaza wa Kimeru
 
Mbowe siyo gaidi lakini ni mkaidi, ikiwa tumefiwa na raisi aliyekuwa madarakani, je itashindikana kwa kiongozi wa chama cha upinzani?
Wapinzani watumie busara katika kudai katiba mpya, tume huru na ya haki ya uchaguzi, mikutano ya hadhara ya kisiasa, bunge na mahakama zisizoingiliwa katika utendaji wake n.k.
Tubadilike ifike mahala tufanye siasa za kistaarabu zisizokuwa na chuki wala kudhuruiana.
Unaongelea siasa za kistaarabu za kupiga risasi,kufunga na kubambikia kesi wapinzani kama kina Sugu, Lisu, Mbowe, lema etc na kuiba uchaguzi nchi nzima, kuweni na aibu kidogo
 
Huyu Mbowe mzembe sana, Yaani uzoefu wote alionao kwenye siasa za bongo bado anapiga masimu na kutuma hela kwenye simu kindezindezi hivi?

Anamuamini mtu hata hamjui vizuri na anamkaribisha hadi ndani ya gari lake la KUB tena akiwa na "Mukya"? Alishindwa nini kuwatuma hao akina Bwire kudili na huyo houseboy wa Sabaya?

And ukimkuta majukwaani anapayuka tu oh mtupe nchi tuiongoze, kwa uzembe na upuuzi kama huu hata huo ubunge hauwafai...
 
Huyu Mbowe mzembe sana, Yaani uzoefu wote alionao kwenye siasa za bongo bado anapiga masimu na kutuma hela kwenye simu kindezindezi hivi? Anamuamini mtu hata hamjui vizuri na anamkaribisha hadi ndani ya gari lake la KUB tena akiwa na "Mukya"? Alishindwa nini kuwatuma hao akina Bwire kudili na huyo houseboy wa Sabaya? And ukimkuta majukwaani anapayuka tu oh mtupe nchi tuiongoze, kwa uzembe na upuuzi kama huu hata huo ubunge hauwafai...
Tutakuchagua wewe unda chama chako tu
 
Watu wameanza kupaniki mapema sana, mbona ngoma bado mbichi sana hii.....
FCtHNKnX0AkERN2
 
Kama kummaliza Saa mbaya na mwendazake ni ugaidi..bora iwe hivyo kiroho safi tu
 
Back
Top Bottom