Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Upande wa Utetezi waanza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka 26 Novemba, 2021

Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Upande wa Utetezi waanza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka 26 Novemba, 2021

wamfunge chap huyu gaidi..haya makelele ya ubw## koko yaishie.ushahidi umeenyoka kabisa kesi inatakiwa iwe imeisha muda mrefu sana...hawa mawakili kazi yao imekuwa nikuweka mapingamizi tu ili kuisumbua mahakama ila hakimu kwa wanavyokuchosha..mfunge gaidi na viboko juu
Inzi wa kijani mna bongo ndogo na nyepesi sana! Kuna ushahidi gani ulionyooka pale zaidi ya mbege ya Rau Madukani, na vitabu vya kuandikishwa mahabusu?
 
tangu kesi ianze sijaona popote kwenye Ushahidi wa Ugaidi zaidi ya mbege ya pale Rau madukani kwa mama P.
Bado wapo kwenye kesi ndogo hawajaanza hata hiyo kesi kubwa kibatala wanapotezea muda tu wakili uchwala
 
Si chadema walisema mahakama ya mafisadi na majizi haipo?

Inakuweja tena Mungu wao anahudhuria hapo.
Daaaah! Ili mradi tu na wewe umeandika, bila kujali fahali ya kuwa ni sehemu ya wana JF, itambulikayo kuwa ni nyumbani kwa ma G/Thinkers!
 
wamfunge chap huyu gaidi..haya makelele ya ubw## koko yaishie.ushahidi umeenyoka kabisa kesi inatakiwa iwe imeisha muda mrefu sana...hawa mawakili kazi yao imekuwa nikuweka mapingamizi tu ili kuisumbua mahakama ila hakimu kwa wanavyokuchosha..mfunge gaidi na viboko juu

Halafu kuna wapuuzi wanabeza nyeto! Nyeto moja tu ingeliepusha Taifa na hii takataka.
 
Si chadema walisema mahakama ya mafisadi na majizi haipo?

Inakuweja tena Mungu wao anahudhuria hapo.
CCM Haikuweza kuwashitaki wahujumu wote Hadi Akina Singh na IPTL yake wooote walionekana sio wahujumu wanaostahili kufikishwa ndani ya jengo hilo!
Ila CCM ikaona Mbowe anastahili kuhukumiwa ndani ya jengo hilo Kama mhijumu na gaidi anaefadhiri Ugaidi kwa sh 600,000 kwa watu watatu
1. Wakafyeke miti Moro - Iringa
2, wakachome vituo vya mafuta Dom - Dar
3. Waitishe maandamano nchi mzima.
4. Wahakikishe nchi haitawaliki.
Kumbuka hayo yote kwa 600k.
Ukitoa hela ya kununulia panga na mashoka na chainsaw moja hela inaisha.
Huo Ni Ugaidi au ujinga tuambieni ninyi mnao imba hizo pambio!
 
Kesi ya ugaidi ( kesi ndogo katika kesi kubwa) inayoendeshwa divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa inaendelea leo ambapo upande wa Jamhuri utaleta shahidi mwingine.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe -Inspector Lugawa ISSA Maulid atoa Ushahidi, Kesi yaahirishwa hadi Novemba 25, 2021

========

UPDATES:
Mpaka_sasa__Saa_5%3A07_Asubuhi%2C_Mawakili_Wa_Serikali_hawajafika_Mahakamani.jpg
 
Halafu kuna wapuuzi wanabeza nyeto! Nyeto moja tu ingeliepusha Taifa na hii takataka.
Kwa hoja yako..nikiashiria yakwamba haunatofauti na toilet paper ya chooni..ila bora ile toilet paper kuliko wewe kwasababu inarangi nyeupe.
 
Kwani hukumu sibado mkuu, jaji sasaivi kaziyake nikusikiliza tu. Ingawa mbakasasa mimi kama mimi sioni ushahidi wenye nguvu .
Kwani hujafatilia hukumu za kesi ndogo ndani ya kesi kubwa pamoja na hukum za mapingamizi ukaona hii ni fedhea?
 
Update siku izi zinachelewa sana
Sana
Kesi ya ugaidi ( kesi ndogo katika kesi kubwa) inayoendeshwa divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa inaendelea leo ambapo upande wa Jamhuri utaleta shahidi mwingine.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe -Inspector Lugawa ISSA Maulid atoa Ushahidi, Kesi yaahirishwa hadi Novemba 25, 2021

========

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16/2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

WS Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Idd Msawanga
Seleman Matauka
Maria Mushi
Khadija Aron
Evaresta Kisanga
Hawa Manasheria wa Serikali wanaipa hasara Serikali,
 
Mashahidi wote ukiangalia wanazungumzia Sana ukamataji zaidi na wote asilimia kubwa ni askari kwa uwingi wao itachukua muda mrefu huku watuhumiwa wakiwa wanatabika gerezani kwa kesi isiyo na kichwa Wala miguu.
 
Kesi ya ugaidi ( kesi ndogo katika kesi kubwa) inayoendeshwa divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa inaendelea leo ambapo upande wa Jamhuri utaleta shahidi mwingine.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe -Inspector Lugawa ISSA Maulid atoa Ushahidi, Kesi yaahirishwa hadi Novemba 25, 2021

========

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16/2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

WS Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Idd Msawanga
Seleman Matauka
Maria Mushi
Khadija Aron
Evaresta Kisanga

Jaji anaita washtakiwa wote 4 na wanaitika wapo

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa, upande wetu baada ya kupitia Sheria ya ushahidi, baada ya Shahidi wa 4, tumeamua Kufunga ushahidi wetu katika kesi hii ndogo katika kesi kubwa.

Wakili wa Serikali: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..

Jaji: anaandika Kidogo

Jaji: Mna lolote la kusema upande wa Utetezi

Wakili Peter Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji

Jaji: anaandika Kidogo.

Jaji: baada ya Maombi ya Upande wa Mashtaka ambayo yamewasilishwa Muda siyo Mrefu, Mahakama Inafunga Ushahidi wa Upande wa Utetezi na Kwa Sababu hiyo nawakaribisha Upande wa Utetezi.

Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa Niaba ya Mshitakiwa Wa Tatu tupo tayari Kujitetea na Sababu hiyo basi ataanza Wakili Dickson Matata kumuongoza Shahidi

Jaji: Mshitakiwa namba 3

Mshitakiwa namba 03 anaenda Kizimbani Kama shahidi Upande wa Utetezi.

Jaji: Majina yako

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya

Jaji: Umri

Shahidi: 35yrs

Jaji: Kabila

Shahidi: Mmakonde

Jaji: Dini yako

Shahidi: Muislamu

Shahidi: Wallah wabillah watallah Nathibitisha Mbele ya Mahakama hii, Kuwa Ushahidi nitakao toa Utakuwa ni kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu nisaidie

Jaji: Karibu Mr. MATATA

Wakili Dickson Matata: Asante Mheshimiwa Jaji

Matata: Shahidi Ieleze Mahakama Unaitwa nani Unatokea Wapi

Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya, Naishi Kimara, King'ong'o

Matata: Shahidi Ulikuwa unafanya Kazi Gani?

Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi, na Baada Ya Kuacha kazi nikawa napambana Kupata Kazi kwa Freeman Mbowe

Matata: Kazi ya Jeshi Umeacha lini?

Shahidi: Mwaka 2017

Matata: Baada Ya Kuacha kazi Mwaka 2007 ukawa unaishi wapi?

Shahidi: Nilikuwa naishi Shinyanga

Matata: Baada ya Kuishi Shinyanga Ukaishi Wapi

Shahidi: Nikaipata Kazi Mtwara

Matata: Ulikuwa umepata kazi gani?

Shahidi: Kampuni ya Muhindi Ya kusaga Kokoto, DOT

Matata: Kwanini Uliacha kazi?

Shahidi: Nakumbuka Nilipigiwa simu na Denis Urio Kwamba Kuna kazi Ya VIP protection

Matata: ilikuwa ni Kipindi gani ambapo Denis Urio alikwambia Mbowe alikuwa anahitaji VIP Protection

WS ROBERT Kidando: OBJECTION

Matata: Ngoja Nibadili Swali

Matata: Unakumbuka Tarehe 05 August 2020 ulipokea kuwa wapi

Shahidi: Nakumbuka nilikuwa Moshi, Rau Madukani, nikavamiwa na Polisi na Kupelekwa Central Polisi

Matata: Unasema Central Polisi, ya wapi.?

Shahidi: Moshi

Matata: Unasema Kwamba Ulivamiwa na Polisi Walikuwa wangapi

Shahidi: Walikuwa zaidi ya Nane, Hatukujua ni Polisi Kwa sababu Hawakujitambulisha, Baada Ya kutukamata na kutoa Amri tupelekwe Polisi ndiyo tukajua hawa ni Polisi

Matata: Baada Kufikisha Central Polisi Moshi

Shahidi: Moja kwa Moja nipelekwa mahabusu, Chumba ambacho Kina Watu wengi

Matata: chumba ambacho Ulipelekwa Kilikuwa eneo gani

Shahidi: palepale Central

Matata: Unaweza Kuwatambua Baadhi ya watu Waliokuwa katika hicho Chumba
Kazi nzuri
 
Back
Top Bottom