Kesi ya ugaidi ( kesi ndogo katika kesi kubwa) inayoendeshwa divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa inaendelea leo ambapo upande wa Jamhuri utaleta shahidi mwingine.
Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe -Inspector Lugawa ISSA Maulid atoa Ushahidi, Kesi yaahirishwa hadi Novemba 25, 2021
========
UPDATES:
Jaji ameingia
Kesi namba 16/2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu
WS Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Idd Msawanga
Seleman Matauka
Maria Mushi
Khadija Aron
Evaresta Kisanga
Jaji anaita washtakiwa wote 4 na wanaitika wapo
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa, upande wetu baada ya kupitia Sheria ya ushahidi, baada ya Shahidi wa 4, tumeamua Kufunga ushahidi wetu katika kesi hii ndogo katika kesi kubwa.
Wakili wa Serikali: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..
Jaji: anaandika Kidogo
Jaji: Mna lolote la kusema upande wa Utetezi
Wakili Peter Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji
Jaji: anaandika Kidogo.
Jaji: baada ya Maombi ya Upande wa Mashtaka ambayo yamewasilishwa Muda siyo Mrefu, Mahakama Inafunga Ushahidi wa Upande wa Utetezi na Kwa Sababu hiyo nawakaribisha Upande wa Utetezi.
Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa Niaba ya Mshitakiwa Wa Tatu tupo tayari Kujitetea na Sababu hiyo basi ataanza Wakili Dickson Matata kumuongoza Shahidi
Jaji: Mshitakiwa namba 3
Mshitakiwa namba 03 anaenda Kizimbani Kama shahidi Upande wa Utetezi.
J
aji: Majina yako
Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya
Jaji: Umri
Shahidi: 35yrs
Jaji: Kabila
Shahidi: Mmakonde
Jaji: Dini yako
Shahidi: Muislamu
Shahidi: Wallah wabillah watallah Nathibitisha Mbele ya Mahakama hii, Kuwa Ushahidi nitakao toa Utakuwa ni kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu nisaidie
Jaji: Karibu Mr. MATATA
Wakili Dickson Matata: Asante Mheshimiwa Jaji
Matata: Shahidi Ieleze Mahakama Unaitwa nani Unatokea Wapi
Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya, Naishi Kimara, King'ong'o
Matata: Shahidi Ulikuwa unafanya Kazi Gani?
Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi, na Baada Ya Kuacha kazi nikawa napambana Kupata Kazi kwa Freeman Mbowe
Matata: Kazi ya Jeshi Umeacha lini?
Shahidi: Mwaka 2017
Matata: Baada Ya Kuacha kazi Mwaka 2007 ukawa unaishi wapi?
Shahidi: Nilikuwa naishi Shinyanga
Matata: Baada ya Kuishi Shinyanga Ukaishi Wapi
Shahidi: Nikaipata Kazi Mtwara
Matata: Ulikuwa umepata kazi gani?
Shahidi: Kampuni ya Muhindi Ya kusaga Kokoto, DOT
Matata: Kwanini Uliacha kazi?
Shahidi: Nakumbuka Nilipigiwa simu na Denis Urio Kwamba Kuna kazi Ya VIP protection
Matata: ilikuwa ni Kipindi gani ambapo Denis Urio alikwambia Mbowe alikuwa anahitaji VIP Protection
WS ROBERT Kidando: OBJECTION
Matata: Ngoja Nibadili Swali
Matata: Unakumbuka Tarehe 05 August 2020 ulipokea kuwa wapi
Shahidi: Nakumbuka nilikuwa Moshi, Rau Madukani, nikavamiwa na Polisi na Kupelekwa Central Polisi
Matata: Unasema Central Polisi, ya wapi.?
Shahidi: Moshi
Matata: Unasema Kwamba Ulivamiwa na Polisi Walikuwa wangapi
Shahidi: Walikuwa zaidi ya Nane, Hatukujua ni Polisi Kwa sababu Hawakujitambulisha, Baada Ya kutukamata na kutoa Amri tupelekwe Polisi ndiyo tukajua hawa ni Polisi
Matata: Baada Kufikisha Central Polisi Moshi
Shahidi: Moja kwa Moja nipelekwa mahabusu, Chumba ambacho Kina Watu wengi
Matata: chumba ambacho Ulipelekwa Kilikuwa eneo gani
Shahidi: palepale Central
Matata: Unaweza Kuwatambua Baadhi ya watu Waliokuwa katika hicho Chumba