Sina mlengo na siasa, ila nimejaribu kutoa tetesi, plz acha kuhemkwa.Hakika nyie waongo na mnatafta Kiki huu umati wote unang'aa kwa nguo Safi za kijani et unatuambia wameropoka hawamtaki. Walai nawaambia watanzania wamemchagua Dr John P Magufuli na wamemchagua CCM.
Na wale waliokuwa wanatumia Kiki ya tetemeko povu leo limewatoka baada ya kuona umati Mkubwa ukimshangilia jemedari wao na Rais wao anayesubilia kuapishwa
Check umati huu
View attachment 1571640
Hizo ni Kiki zilizotengenezwa baada ya waliyotegemea kutotokea. Wakaamua kutengeneza pumba Kama hiiSasa ndo ikawa hivyo kadri ya taarifa kutoka huko.
Yaani ccm wacheni vichekesho mnawakusanya wanafunzi kibao ndiyo mnajisifu mafuriko? Shame on you guysChadema waliishiwa zamani saaana
Magufuli ana upeo mdogo sana. Kwake kila kitu anakiangalia kwa jicho la ujenzi hadi anachosha. Hajui kuwa maisha ya watanzania yana mambo mengi zaidi ya hayo mataa yake anayowaza kujenga. Bure kabisa huyu MhutuAisee bado sana ,yaani taa za barabarani ati ni agenda ya kuombea kura ....dah
Hayo ni maendeleo maana watu wanapita sehemu yenye mwanga ambapo hawawezi kutana na wahuni wowote barabaraniAisee bado sana ,yaani taa za barabarani ati ni agenda ya kuombea kura ....dah
Hizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????Yaani ccm wacheni vichekesho mnawakusanya wanafunzi kibao ndiyo mnajisifu mafuriko? Shame on you guysView attachment 1571667
Kwanin unateseka kiasi hicho?Angalia usijeanguka kwa pressure!Mpaka tar 28 bado mbali sana,huu moto wa kampeni angalieni usijewaacha na maradhi ya moyo!Watu wanampenda Magufuli Hadi basi na tarehe 28 utashuhudia Kama upinzani mtapata hata Jimbo moja Kagera
Ccm mmekwisha jiandaeni kisaikolojia maana Lissu ndiye rais wako ajayeHizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????
Jana Lissu alituma picha za sehemu alipokwenda na kuambiwa katika kata ile hajawahi kumwona Mgombea urais so hata Jana watu hata Kama ni wanafunzi wanaenda kumwona Rais anayewasomesha bure
Duh....chizi...pumba....huna maneno mengine kujenga hoja yako zaidi ya maneno haya....chizi...pumba?? Unaelewa maana ya neno chizi?! Unaelewa maana ya kumwambia mtu kuwa 'maneno yako ni pumba' ? Hebu Kwanza kamwambie Kwanza baba yako aliyekuzaa na mama yako kwamba 'baba wewe ni chizi....mama wewe ni chizi na maneno yako ni pumba' tu..'. Majibu utakayopata kutoka kwa wazazi wako uje utujulishe humu JF...Mimi silalamiki ila nakushangaa kujifanya Chizi wa kutokuwa unaangalia matukio ambayo yanakushika na unaangalia tu matukio unayotolea pumba zako za kutuletea hapa
Upepo wa JPM ni wa kuotea mbaliMagufuli ana upeo mdogo sana. Kwake kila kitu anakiangalia kwa jicho la ujenzi hadi anachosha. Hajui kuwa maisha ya watanzania yana mambo mengi zaidi ya hayo mataa yake anayowaza kujenga. Bure kabisa huyu Mhutu
Mwambie awe makini betri isije gusa tank la mafutaKwanin unateseka kiasi hicho?Angalia usijeanguka kwa pressure!Mpaka tar 28 bado mbali sana,huu moto wa kampeni angalieni usijewaacha na maradhi ya moyo!
Hatuna pressure maana ushindi wa Magufuli Mwaka huu ni wa kihistoria. Mwenye shida ni Lissu maana juzi kaanza kuanguka na pressure mufindiKwanin unateseka kiasi hicho?Angalia usijeanguka kwa pressure!Mpaka tar 28 bado mbali sana,huu moto wa kampeni angalieni usijewaacha na maradhi ya moyo!
Nakuona unateseka kwenye nyuzi humu JF,angalizo ni kuwa angalia usijepata maradhi ya moyo!Hatuna pressure maana ushindi wa Magufuli Mwaka huu ni wa kihistoria. Mwenye shida ni Lissu maana juzi kaanza kuanguka na pressure mufindi
Wanakagera hatujasahu ujue ewe john.https://www.facebook.com/
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.
MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.
"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.
Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.
Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."
Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.
Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.
"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.
----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Watoto wa shule 🤣🤣🤣🤣Upepo wa JPM ni wa kuotea mbali
CheckView attachment 1571681
https://www.facebook.com/