Nawakumbusha, haya siyo matokeo rasmi. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itaanza kutangaza matokeo baada ya kupokea fomu 34A kutoka vituo vyote.
Lengo ni kuhakiki matokeo kwa kulinganisha fomu halisi na ile iliyotumwa kupitia mtandao.
Hata hivyo, mtu yeyote mwenye internet anaweza kupakua fomu hizo na kujumlisha matokeo kutoka kwenye website ya IEBC.
Matokeo yanatofautiana kwenye vituo vya Tv kwasababu ya uwezo wa nyenzo za kupakua na kujumlisha matokeo katika vyombo vya habari.
Ukiyachukulia kama matokeo rasmi utaumia.
Tunywe mtori kwanza nyama tutazikuta chini.
Watanzania wataishia kuona na kufundinshwa maana ya uchaguzi na Kenya hadi pale watakapoacha uwoga.
Huu uwazi na utulivu tunaoushuhudia haujaja kirahisi, kumbukeni. Haki haiombwi, haki inapiganiwa. Wakenya walizichapa 2007/08 matokeo yake wakapata serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoleta Katiba mpya.
Katiba mpya imetibu magonjwa mengi sana Kenya, huku Watanzania wanawabeza kwamba wana ukabila, wao waligundua hilo na wameamua kushughulikia ukabila kimfumo kwa kuanza na Katiba.
Mtanzania anasubiri Mbowe na Lissu ndo aje apigane kwa niaba yake huku yeye akijisemea, ‘basi Sawa’.