hawa jamaa wa Azam Tv wangekuwa waungwana iyo chanel ya Azam HD wangeuza na kwenye vingamuzi vingine ili watu wengi wapate fursa ya kuangalia mechi hizo.
Au wapunguze bei ya kununua vingamuzi vyao ili watu wengi wapate fursa ya kujiunga nao.
Watanzania wengi wamenunua Startimes kutokana na wachina wanajua sana biashara.
Wanauza vingamuzi vyao kwa bei chee ili kuwavutia wateja na kweli wamevuna watu wengi sana.
Hivyo nahawa jamaa wa lamba lamba wanatakiwa wajitathimini ikiwa wanahitaji kupata wateja wengi zaidi, biashara ni ubunifu na kuvutia wateja.