Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

hivi kwa kukadilia sherehe kama hizi hugharimu kiasi gani..?
Sijui. Cheki kile Magufuli alichokisema mwaka jana juu ya kubana matumizi na kuokoa fedha za sherehe za uhuru.
 
Basi sawa. Ila number utaisoma tu
Sisomi namba mimi , mwaka huu nimeuza korosho zangu huku kijijini kwa sh 3750 kwa kilo na nilivuna tani 15, we na wapiga dili wako mnaong'ang'ania mjini mkidai ajira ndio mnaisoma namba kudadadeki!
 
.., wale wale wananchi ambao mwaka jana (2015) mwezi kama huu (desemba) walishangilia kweli sherehe za uhuru zilopohairishwa kwa kisingizio cha 'kubana matumizi' na fedha zile kuelekezwa kwenye matumizi mengine., tukielezwa tufanye usafi nchi nzima..,

..., mwaka huu (2016) ndiyo wananchi hao-hao leo wanasherekea na kushangilia tena wakati maadhimisho yale ambayo mwaka jana yalikataliwa kwa kisingizio cha kubana matumizi, leo wakati yanafanyika.., tena wananchi wale-wale wakishangilia kwa vifijo na nderemo wakisema Hapa Kazi Tu..,

[emoji1485] wananchi hawa siyo watu wa mchezo-Mchezo, wanakwenda na namna unavyovuma.
[emoji1485] wananchi hawa wanacheza kila wimbo, hata wimbo reggae wao wanakata Viuno.
[emoji1485] wananchi hawa, ni rasmi wamekuwa wepesi kusahau, sasa wameruhusu watawala waone udhaifu wao, na bado!
[emoji1485] ni rahisi sana Kuwaongoza watu wa aina hii.., leo wakisikia hivi OYEE, kesho wakisikia hivi OYEE!
[emoji1485]Wale wananchi ambao mwaka jana walisema ahsante kwa kuondoa sherehe za maadhimisho haya.., leo ndiyo wameingia katika uwanja wa uhuru (shamba la Bibi) tangu alfajiri.., ajabu sana!
[emoji1485] hata mwaka mmoja haujapita, tumesahau kabisa tuliambiwa nini 2015 (Desemba) , na sasa 2016 (Desemba) tunashangilia kile ambacho tulisema kwa pamoja ni gharama na hasara kuadhimisha sherehe hizi.., WADANGANYIKA!

T U S A M E H E,
Wale wananchi waliosema:-
1.Lowasa dhaifu na ni fisadi hana sifa ,
2.Ni heshima kubwa kwa Mungu kumzomea Lowasa fisadi,
3.Vibaka wanachomwa moto wakati fisadi anaachwa uraiani akizurura na fomu
4.Atakayemuunga mkono Lowasa akapimwe Akili,
5.Top ten ya mafisadi wa kwanza ni Lowasa,
Ndio wananchi hao hao wanaozunguka naye mikutanoni na walimpa nafasi ya pekee ya kugombea uraisi na ni wananchi wale wale wanaotuaminisha kwamba yule baba sasa sio fisadi tena, na ni wale wale wanaopita naye mitaani na kumbebea begi huku wengine wana PhD zao! Ha ha ha ha ama kweli mnafiki hana aibu!
 
Raisi Magufuli amesema leo kuwa sikukuu ya uhuru ya leo ni ya mwisho kufanyikia Dar es salaam na kwamba ijayo itafanyikia Dodoma. Miundo mbinu ya kuwezesha kufanyika kwa sikukuu hizo ipo? Dodoma kuna uwanja wa Kitaifa?
 
Tatizo ninaloliona hapo ni gharama za kuwasafirisha viongozi wakuu na waalikwa kwenda Dodoma na kurudi.Tutaingia gharama ambazo zingeweza kuepukika.
 
Dodoma kila kitu kipo kwa shughuli zote za serikali.ni bahari tu hakuna.
Ngoja wafanyie huko huko kuondoa foleni na misafara kama ilivyokuwa leo watu wamepata shida kusubiria magari yao yapite,wakienda Dodoma jiji la Dsm litapumua kwa mengi na maendeleo yataongezeka kwa kasi kubwa zaidi maana miji yote ya biashara Duniani hukaa mbali na Ofisi kuu za serikali.
 
Back
Top Bottom