Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.

Ulikunywa ngapi?

Vp umewahi kazini leo au hang over imechyua nafasi yake umeshindwa kuamka.
Chezeya mahaba na simb
a
We acha tu nimelala kaunta kufika kazini ni usingizi wa hangover ila nimeomba ruhusa kwa boss kwa kisingizio naumwa
 
Watu (back four yote ya Yanga) wapigwe bench hadi waaanze kupigania namba upya. That was schoolboy defending from Yanga defence!

Wakati wenzetu Simba sasa wana timu na wanacheza kitimu, sisi tumebakiwa na club ya wachezaji waliolewa umaarufu wa magazetini na kutukuzwa kusikostahili!


Yanga wenzangu, niliyoyaona na kuyaandika hapo juu ndiyo ambayo mwalimu Brandts pia aliyaona na anayafanyia kazi. Kama mwalimu atafanya maamuzi magumu kama haya walau nitapata hope ya taji letu kurudi mahala pake Jangwani. Angalia hapa chini...


Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam KIPA Ally Mustafa ‘Barthez' anaweza kupumzishwa katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina a timu yake na Rhino Rangers ya Tabora, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mechi tisa alizodaka Barthez hadi sasa, amefungwa mabao 11 na inaonekana kudaka mfululizo tangu msimu uliopita kunamchosha na bila shaka Deo Munishi ‘Dida' atasimama langoni kwa mara ya kwanza kesho katika Ligi Kuu tangu asajiliwe na Yanga msimu huu kutoka Azam.
Kwa ujumla, kocha Mholanzi Ernstus ‘Ernie' Wilhelmus Johannes Brandts anatarajiwa kufanya marekebisho makubwa katika safu yake ya ulinzi kesho baada ya matokeo ya sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi Simba SC Jumapili, Uwanja wa Taifa, wakitoka kuongoza 3-0 hadi mapumziko.

Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro' anaweza kuanzia benchi, wakati Juma Abdul ataenda beki ya kulia kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite, atakayehamia katikati kucheza na Kevin Yondan.
Kuna uwezekano pia wakongwe Athumani Iddi ‘Chuji' na Haruna Niyonzima nao wakapumzishwa ili ‘kuweka akili sawa' baada ya sare isiyotarajiwa mwishoni mwa wiki na Frank Domayo akatengeneza safu ya kiungo kwa pamoja na Salum Telela au Hamisi Thabiti.
 
Unaelewa maana ya kupoteza mechi?....Ama matokeo ya 3-3 kwa Simba dhidi ya Yanga siku hizi yana tafsiri mpya?.....

Simba hampaswi kushangilia 'ushindi' huu dhidi ya Yanga.....Mlipaswa kujiuliza kwa nini mmeshindwa kuifunga Yanga na kurudi kileleni mwa ligi....Matokeo ya leo hayana faida yoyote kwenu zaidi ya kuwabakisha nafasi ya 3 ambayo mlishushwa jana na Azam na Mbeya City.....Haya ni matokeo mabaya kwenu kutokana na mechi mbili zinazofuata dhidi ya Coastal Union( Itachezwa Tanga Jumatano hii) na Azam(Itachezwa Chamazi Jumamosi)....Yanga wao wana mechi na vibonde Rhino Rangers na Mgambo JKT ambazo zote zinachezwa Uwanja wa Taifa.....

Baada ya mechi hizi ndio mtakumbuka umuhimu wa mechi ya leo ambayo nyinyi ndio mlikuwa wenyeji....Yanga walikuwa ugenini leo.....

Ni shabiki maandazi pekee wa Simba ndio atashangilia sare ya leo.....

Mkuu Bala, mimi sina nia ya kuleta utani wa SImba na Yanga ktk hili, nimesema Yanga walipoteza mechi dhidi ya Simba kwa kuangalia haya;
1. Baada ya mechi, upande gani ulikuwa na furaha?
2. Baada ya mechi kuisha, upande gani ulikuwa na huzuni?

Ukiweza kuyajibu haya utagundua kwa nini Yanga walipoteza mechi dhidi ya SImba. Sijasema Yanga wamefungwa na SImba, bali Yanga wamepoteza mechi dhidi ya Simba!
 
Nadhani wewe umeanza kushabikia juzi.....Una habari Yanga wamewahi kuchomoa mechi na Simba Sheikh Amri Abeid Arusha matokeo yakawa 4-4......

Simba bana, badala ya kujiuliza ni kwa nini mliruhusu ba0 3-0 1st Half mnaanza kuiponda Yanga kwa kuruhusu magoli matatu......Ulitaka Yanga ishinde???/

Bala, haikuwa kama matokeo ya juzi! Haijawahi kutokea (tafuta kumbukumbu) walipocheza Simba dhidi ya Yanga huko nyuma, na timu mojawapo ikiwa nyuma ya mabao matatu bila halafu mpinzani wake akafanikiwa kuyarudisha yote, Tafuta! Hiyo ya 4-4 ilikuwa 'funga-nikufunge' na sio kama hii ya juzi.
 
Sitaki kuchelewa hata kidogo nimeshaanza safari ya kuelekea Taifa.halafu Jamaa wa JF walikuwa wameficha naona walikuwa na ukarabati, hongera sana Maxence Melo.

kATUNI(1).jpg


UPDATES:

Mapumziko: Yanga 3 - 0 Simba

Dakika 54: Yanga 3 - 1 Simba (Goli la Simba limefungwa na Mwombeki)

Dakika 57: Yanga 3 - 2 Simba (Goli la Pili la Simba kafunga Owino)

Dakika 82:
Yanga 3 - 3 Simba (Goli la Simba limefungwa na Kaze)

Full Time: Yanga 3 - 3 Simba
Hii kwangu ilikiwa mechi bora kabisa zilizowahi kuwakutanisha Simba Vs Yanga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom