Watu tayari wameshaanza kufurika Uwanja wa Amani Zanzibar.
====
MWILI WA HAYATI DKT. MAGUFULI WAWASILI ZANZIBAR
Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli umewasili Visiwani Zanzibar ukitokea Makao Makuu ya Tanzania, Dodoma, ambapo shughuli ya kumuaga kitaifa ilifanyika jana Machi 22, 2021.
Mwili wa Dkt. Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 umepokelewa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa. Utapelekwa Uwanja wa Amaan ambapo utaagwa.
RAIS MWINYI: KIONGOZI KAMA DKT. MAGUFULI NI NADRA KUPATIKANA
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amesema Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa mstari wa mbele katika kuimarisha maisha ya Watanzania kwa misingi ya Haki na Usawa bila kujali Dini, Kabila, Rangi au Jinsia.
Amesema, "Tumempoteza Mwana Mapinduzi mahiri wa karne ya sasa. Alikuwa Kiongozi mwenye uwezo na kipaji cha aina yake. Kiongozi kama yeye ni nadra sana kupatikana"
Katika hotuba yake, amemuelezea Dkt. Magufuli kama Kiongozi aliyejipambanua kwa uzalendo wa kweli, mtetezi wa wanyonge, mwenye kujivunia na kujionea ufahari Utanzania na Uafrika wake.
Amesema kifo chake kimeleta simanzi kwa Watanzania na wapenda Maendeleo katika bara la Afrika.
Kwa jinsi "Hayati Mwenyekiti Wa CCM" alichowafanya wazanzibari kwenye uchaguzi mkuu 2020 miezi michache iliopita, "VIRUNGU/FIMBO/MAKOFI/MITAMA kolabo "MABOMU/RISASI", visiwani walichezea baikoko wakachezeka kweli kweli.
Sijui kama boat za bakhresa hazijajaa waombolezaji waliokatiwa ticket za bure tokea "MFUKO MAALUM WA MAAFA WA LUMUMBA".
Kuna watu huko kila wakisikia jina lake wanakumbuka sura za ndugu/watoto/marafiki waliokua wakiokotwa maiti zao mitaani waliopoteza maisha. Wenye matundu ya risasi vifuani/tumboni/vichwani.
Mungu awape subira wahanga, na maisha ya amani waliopoteza maisha yao kwenye uchaguzi mkuu 2020.
Acheni kejeli, ni JPM ni mpendwa wa wengi, acheni wamuoge ili wapate closure, kama mnaona wivu sana mwambieni Lissu na yeye afe aagwe na mashoga zake huko Belgium.