#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

Habari zenu wana JF

Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu (anaishi na aunty Dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
Watu mna moyo aisee
 
Mi nilichomwa Astrazenica,siku ya kwanza nilikuwa poa,ya pili nilihis homa kidogo na kichwa lakini nilikuwa sinywi dawa,baadae nikaamua ninywe paracetamol nikawa poa tu.Wife kapata Moderna ye yupo poa,ivo inategemea na mwili wa mtu sababu kitu kipya kinaingia mwilini.lakin nashkuru nimejikinga,mengine tutaomba Mungu, we have done our part.
Kongole
 
Yani mimi walinicheleweshea hii chanjo. Since jamaa hajadead nilikuwa naitamani sana ije nichome. Maana nilipomsikia tu anasema tumeishinda corona kwa maombi ya siku tatu nikaona chenga tu hapa bongo
 
Kesha iingiza ubovu mwilini mwake, muda ndiyo utaongea,kwa Sasa bado mapema mno kuona madhara yajayo!! Lakini asanteni sana kwa kujitolia na kukubali kufanywa kua majaribio ya Chanjo bila malipo, huo ndiyo uzalendo hasa,mmewapita hata Wanajeshi wanaoenda vitani, mmeamua kujivisha mabomu ya Chanjo!!
Hii sio chanjo ya bure serikali imenunua kupitia mkopo ambao tutalipa kama taifa,wasiwasi wangu ni mmoja tumekopeshwa mapesa mengi tununue chanjo watu wasipoenda kuchoma tutapeleka wapi hizo chanjo?
Attendance ni ndogo kwenye vituo
 
Hasira za nini sasa? Wewe ni ndondocha ni ndondocha tu. Utafanya nini sasa? Ujua hata hayo matusi ni madhara ya chanjo? Poleni sana. Ageni kabisa famlia zenu maaana hamfahanu kama mtaweza kukumbuka kitu au kuandika wosia.
Ngoja yaje yakupate mateso ya kuugulia covid 19 utakuja tusimulia hapa au hao ndugu zako unaowadanganya
 
Me cheti nilipewa jana jioni kupitia email, kama ulifanya booking online watakutumia kwa email. Kama ulifanya manually nadhani inabidi ukafatilie ulipochomea
Ok shukrani sana ni kule maneromango, kisarawe itabidi niende.
 
Nilichoma toka 6/8 na haikuisumbua kwa lolote zaidi ya maumivu ya sindano yenyewe for some days...
 
Hiyo kitu ipishe mbali
Sihitaji hats kuiona
Bado nahitaji kuishi na kuzaa
Sihitaji kuwa zombi Mimi
Sisi wenzenu tuna maamuzi magumu. Tumekiangalia kifo usoni na kusema mi nachanja njoo niue basi.

Baada ya kuchanja hamna kitu.
Kuna waliochanja mbele yetu bado kidogo kumaliza mwaka wako fresh tu na Mungu atajalia.

Sasa nyie wenzetu ukiona tu husikii ladha na mbavu zinabana basi aandika wosia.
Ile hofu tu ya Lohh kumbe, itakuua.
 
Ambao mnaogopa kuchanja mna kihoro kikubwa cha kuogopa kifo.
Sawa death is a subject which makes most people uncomfortable to talk about,
but then you must appreciate that against all odds there are some chaps like us (me) who dared to face death one on one by taking the jab not knowing what will happen afterwards.
So far am in good health thank God the Almighty i don't expect to kick the bucket anytime soon.
 
Mara nyingi chanjo zina reaction fulani mwilini. Mimi hii sijachanja bado lakini nitafanya hivyo soon.
Nilichanja yellow fever ukubwani nikapata homa kali baada ya siku kama mbili hivi. Hata pain killer sikutumia, nilipumzika tu na kunywa maji mengi ikaisha. Hii yellow fever nilichanja japo nilikua na cheti tayari 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom