#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

Inabid ufanye checkup ya malaria ujitibie kama ipo ili homa ya chanjo isiamshe homa ya malaria ya MUNGU utayaona
 
Mimu nilibadilika kuwa zombie ndanu ya masaa 24 baada ya hapo nikawa normal
 
Kumbe hata nikitumia diclopar haina shida maana maumivu bado ninayo. Tena nahisi jioni hali inaweza nibadilikia
Yes. Pigaa diclipar. Kwangu imesaidia. Kwani hukiambiwa utumie pain killer? Panadol nilimeza ile saa nane usiku haikusaidia. Kulipokucha ndo nikaoiga diclopar
 
Mimi na mke wangu tulichoma siku moja.Mimi nilipata homa kali usiku, lakini mke wangu hakupata shida yoyote.
Baada ya siku moja nikawa fresh.
Mabadiliko niliyoona ni kwamba sasa hivi sisumbuliwi na mafua tena. Kawaida mke wangu akipata mafua huwa ananiambukiza na yananisumbua,lakini juzi alipata mafua lakini mimi ninadunda tu.
Asante sana Johnson& Johnson [emoji16]
Halaf watu wanachukuliaga poa sana johnson and johnson. Wangejua kwanza ubora wa hizi bidhaa na gharama zake wasingekua wanachonga hivi. Nilifanya kazi kampuni kubwa inadeal na products za johnson m johnson (jnj) za kudeal operation hasa mifupa, screws, nyuzi etc. Hizo bei mtu akikuambia unaweza sema anajibrag. Yaan ni ghali mno
 
Ha ha ha.. eti unakuta mtu na akili zake timamu anawaza dunian watu watabadilika kuwa mazombie, amakweli kazi ipo.
Nachekaga hapa tu[emoji28][emoji23][emoji23]

Nimewaambia after hiyo 2 to 5 years wahamie ulaya na america maana hakutakua na watu tena kumebaki mazombie tu
 
Ila Bongo kweli ni ushenzini. Kumbe watu wanapokwenda kuchomwa hawaulizwi maswali yoyote na kuambiwa side effects za kawaida zinazoandamana na chanjo na pia zile za hatari ambazo wanatakiwa kwenda hospital wakizipata? Karatasi siyo gharama kubwa, yaani serikali imeshindwa kuchapisha vipeperushi ambavyo watu watapewa baada ya kuchoma chanjo? Ona mleta mada anashangaa alipoambiwa asubiri kidogo, hata hajui ni kwa nini! Very lazy and incompent people indeed.
 
Sisi wenzenu tuna maamuzi magumu. Tumekiangalia kifo usoni na kusema mi nachanja njoo niue basi.

Baada ya kuchanja hamna kitu.
Kuna waliochanja mbele yetu bado kidogo kumaliza mwaka wako fresh tu na Mungu atajalia.

Sasa nyie wenzetu ukiona tu husikii ladha na mbavu zinabana basi aandika wosia.
Ile hofu tu ya Lohh kumbe, itakuua.
Issue ya kutosikia harufu zishawatokea sana watu tena kuna uzi humu watu wanaelezea watu washakutana na hizo hali za kushindwa kunusa,kutopata radha na kubanwa pumzi.
 
Ila Bongo kweli ni ushenzini. Kumbe watu wanapokwenda kuchomwa hawaulizwi maswali yoyote na kuambiwa side effects za kawaida zinazoandamana na chanjo na pia zile za hatari ambazo wanatakiwa kwenda hospital wakizipata? Karatasi siyo gharama kubwa, yaani serikali imeshindwa kuchapisha vipeperushi ambavyo watu watapewa baada ya kuchoma chanjo? Ona mleta mada anashangaa alipoambiwa asubiri kidogo, hata hajui ni kwa nini! Very lazy and incompent people indeed.
Hivi na si kuna makundi ya watu ambao hawatakiwi kuchanjwa?
 
Mi tangu nimechoma silewi kabisa pombe, kiwango cha unywaji kipo juu sana hadi naogopa. Na siku niliyochoma nilipiga sana tungi
 
Habari zenu wana JF

Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu (anaishi na aunty Dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
Subiri kuwa zombie baada ya miaka miwili mkuu!! Pole sana.
 
Katika wenzetu watatu wa kazini waliochoma ni mmoja tu ndio amepata side effect mpk kwenda hospital. Nae alisumbuliwa na kichwa na homa na baridi.

Mie bado najishauri [emoji848]
 
Nenda kachanjwe, me saiv naendelea fresh. Naamin kesho nitakuwa mzima kabisa maana saiv napiga gkass za maji tu
 
Waliochanja wakigeuka mazombi hii dunia haitakalika,na itokee waliochanja wakazaa mavampaya sijui itakuwaje.
IMG-20210519-WA0015.jpg
 
Habari zenu wana JF

Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu (anaishi na aunty Dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
Mie siku ya 8/8 nilienda kumjulia hali mgonjwa mmoja hospitali, pale mapokezi nikakuta kuna benchi la chanjo ya Covid.Bila ajizi nikachanjwa, sasa kesho yake trh 9/8 nilikumbana na hali kama hiyo, kichwa na homa. Kuwauliza waganga wakanishauri nitumie dawa za kutuliza maumivu tu!.Nashukuru Mungu ilipofika trh 10/8 asubuhi ile hali ya kuumwa kichwa na homa iliisha kabisaa!!! mpaka sasa nipo mzima wa afya tele.Wana JF twendeni tukapate chanjo!!!!
 
Ila Bongo kweli ni ushenzini. Kumbe watu wanapokwenda kuchomwa hawaulizwi maswali yoyote na kuambiwa side effects za kawaida zinazoandamana na chanjo na pia zile za hatari ambazo wanatakiwa kwenda hospital wakizipata? Karatasi siyo gharama kubwa, yaani serikali imeshindwa kuchapisha vipeperushi ambavyo watu watapewa baada ya kuchoma chanjo? Ona mleta mada anashangaa alipoambiwa asubiri kidogo, hata hajui ni kwa nini! Very lazy and incompent people indeed.
Mbongo wanakuchoma,Kama kundondoka kadondookee kwenu!!
 
Back
Top Bottom