#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

Nenda kachanjwe, me saiv naendelea fresh. Naamin kesho nitakuwa mzima kabisa maana saiv napiga gkass za maji tu
Kisa wwe umechanjwa, basi unataka kila mtu achanjwe!? Nakukumbusha tena, Chanjo ni hiyari!!
 
Ila Bongo kweli ni ushenzini. Kumbe watu wanapokwenda kuchomwa hawaulizwi maswali yoyote na kuambiwa side effects za kawaida zinazoandamana na chanjo na pia zile za hatari ambazo wanatakiwa kwenda hospital wakizipata? Karatasi siyo gharama kubwa, yaani serikali imeshindwa kuchapisha vipeperushi ambavyo watu watapewa baada ya kuchoma chanjo? Ona mleta mada anashangaa alipoambiwa asubiri kidogo, hata hajui ni kwa nini! Very lazy and incompent people indeed.
Hata mimi nashangaa hawakupewa semina kiaje. Maana kabla niende choma magroup ya familia vile vipeperushi vilikua vinawekwa tunasoma tu. Na tulipofika pia tulielezwa juu ya side effects. Hata nilipoumwa kichwa sikusema lolote. Na sikuogopa. Ila nilikausha maana mamangu muoga angeanza nilaumu na kujutia mpk yeye alipoanza sema anaumwa kichwa japo si sana[emoji28] na hakua anaogopa wakat ni mwoga wa kupitiliza.
 
Issue ya kutosikia harufu zishawatokea sana watu tena kuna uzi humu watu wanaelezea watu washakutana na hizo hali za kushindwa kunusa,kutopata radha na kubanwa pumzi.
Kuna ile ya 1st variant ilinipata nikiwa kituo cha mwendokasi. Nikawa nataka anguka kbs. Nilikimbia kufa na nikafanya kutrotri kbs. Sikwenda tena safari yangu. Nikapanda boda faster nikarudi home. Niliogopa ningeanguka kituoni ningekimbiwa halaf nipelekwe mloganzila ama amana
 
Chanjo ni hiari na anayechanja au anayekataa wote wana haki

Mungu atusaidie
 
Mi tangu nimechoma silewi kabisa pombe, kiwango cha unywaji kipo juu sana hadi naogopa. Na siku niliyochoma nilipiga sana tungi
Kwetu rombo kunae kijana alichoma leo kesho akaenda kunywa amefariki juzi. Sidhan kama hata ameshazikwa. Amemwogopesha hata bibi yangu kuchoma[emoji28] maana na yeye anapiga tusker sana.. hoping amepiga aisee. Lzm kesho nimchek
 
Kwani hao viongozi unataka nao mkuu wakiumwa homa na kutetemeka usiku kwenye maduveti yao pia wakwambie?

Chanjo zote duniani huwa hivi. Ni lazima mwili u react ukichoma chanjo. Umewahi kuchoma chanjo gani ingine ukiwa mkubwa? Umewahi choma ya hepatitis? Yellow fever? Ya mafua? Na zote tu huwa hivyo. Na ungekuwa mzazi utakumbuka kuwa watoto wachanga wakichomaga chanjo za aina mbali mbali huwa zinawaletea homa siku chache za kufuatia na huwa wanalia sana tu

chanjo ya Ini hainaga shida

hii chanjo ya COVID19 Jansen; wengi waliochoma reaction wanayokutana nayo ni baridi kali na homa hasa nyakati za usiku lakini baadaye inatulia na maisha yanaendelea.
 
Kuna mtu kakulazimisha mkuu?
Sasa Mtu kasema amenyuti kwanza,anasikilizia, wwe unamwambie nenda kachanje eti mbona wwe uko fresh! Unajitambuwaji wakati umeshainhiza kitu kigeni kwenye Kinga zako za asili!? Muombe Mungu akuvushe salamaa, maana nyinyi mliokimbilia kuchoma ndiyo tumewafanya panya wa maabara tunawasikilizia nyinyi hali zenu zitakuwaje,hadi na Watoto mtakao zaa watafananaje! Kuna mengi kwenye hiyo Chanjo!!
 
Sasa Mtu kasema amenyuti kwanza,anasikilizia, wwe unamwambie nenda kachanje eti mbona wwe uko fresh! Unajitambuwaji wakati umeshainhiza kitu kigeni kwenye Kinga zako za asili!? Muombe Mungu akuvushe salamaa, maana nyinyi mliokimbilia kuchoma ndiyo tumewafanya panya wa maabara tunawasikilizia nyinyi hali zenu zitakuwaje,hadi na Watoto mtakao zaa watafananaje! Kuna mengi kwenye hiyo Chanjo!!
Sawa, ngoja tusubiri hayo mengi yatokee maana hii sio chanjo ya kwanza kuchoma. Kwahiyo napenda sana hayo unayoyadhania wewe yatatokea yatokee ili ujifunze kitu. Vinginevyo utasubiri sana bila mafanikio ya unachokisubiri kukiona
 
Mimi nilichoma mchana wa saa sita nikawa vizuri tu, baadaye jioni naona mkono niliochoma kama unaishiwa nguvu kufika saa moja usiku naona na mwingine unaishiwa nguvu usiku saa nne kiuno,Shingo na kichwa vinauma sana usiku natamani kukuche mapema hali iliendelea hadi kesho yake mwili hauna nguvu nikawasiliana na Dr. Akanishauri ninywe panadol nikaanza kujisikia vizuri.!
NB; Wataalamu inabidi watueleze ukweli maana wanasema tu haina madhara kumbe shida ipo.!
 
Na Kuna kuchoma sindano ya pili... Hii moja haitoshi...

Keep in mind...
 
Antibodies wamejisalimisha kwa Corona. Chanjo inachukua nafasi ya Antibodies
 
Habari zenu wana JF

Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu (anaishi na aunty Dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
Pole sana kwa kuingia chama usichokijua.
 
Mapimbi na misukule ya Gwaji boy bado mpoo kumbe?
Usijifariji kwa kumchukia Gwajima wakati dunia nzima wenye akili wanahoji. Wewe ndiye sukule hasa. Unaujasiri gani wa kumpinga gwajima wakati hata elimu huna. Unasubiri jembe na nyundo wakuambie nenda kulika unaenda kushoto hakufai, unaenda, kesho wanakuambia nenda kulia, ukisema kushoto wewe ni haini, unakwenda. Halafu unaanza kuimba, WAIOKUSHOTO NI MAHAINI bila hata kujiuliza nini kimetokea!!. KUNA USUKULE NA UPUMBAVU ZAIDI YA HUO? HEE!. HUJIONI?

HUYU NI GWAJIMA?

 
Shughuli take utaipata mwakani. Huyo mzee janja janja anaekaa ndani ya boxer katikati ya miguu atakua amestaafu. Litakua bomba tu.
 
Duh!
Mbona Mimi nimechoma tarehe 13 August na sijahisi chochote Cha ajabu zaodi ya kaganzi flani kwa mbaali kwenye bega pale nilipochomea sindano ambayo ilidumu kama siku tatu au nne tu ikapotea na mpaka sasahivi Niko fiti na hata siku niliyochoma hiyo chanjo kazi nzito za kutumia nguvu nilikuwa nafanya Kama kawaida.
Anyway Kama ni kweli Basi pole Sana na hongera kwa uamuzi wa kupata chanjo.
Kuna tatizo la ELIMU kwenye vichwa vya watu, hapo umeandika utumbo gani?.
 
Back
Top Bottom