Yaliyonikuta jana!!

Yaliyonikuta jana!!

  • Thread starter Thread starter Deleted member 485868
  • Start date Start date
Mm nakumbuka tulienda Bahari beach kuogelea maeneo ya Tegeta katikati ya kibaoni na kwa ndevu ndio unakutana na Bahari beach basi tulivyotoka kwenye maji tukaenda kucheza mchezo wa kujichimbia kwenye michanga pembeni yetu ghafla tukaona mkaka mzuri amevaa nguo nyeupe t-shirt mpaka suruali yuko peku hana kitu chochote amesimama anatuangalia sisi tuakendelea kucheza baada kama ya dkk 1 akawa haonekani na maeneo ya beach kama mtu anatembea lazima utamuona umbali mrefu tukaanza kuogopa ghafla tunaona wakaka wengine wanakimbia wameshika nguo mkononi ikabid na sisi tutoke nduki kuelekea maeneo ya nyumba na vipensi vyetu tukafika mbele tukavaa nguo tukaenda mpaka kwenye kituo cha pikipiki tukamuuliza mmojawapo akasema nasikia watu wanasemaga huwa kuna jini la kiume toka siku hiyo sijaenda bahari beach tukahamia Mahaba beach ya BOKO.
Kwenye ubora wako sasa namsubiri na Mbalizi1 [emoji23][emoji23]
 
Nikageuka kwa mara ya mwisho sikumuona tena yule dada

Si alikuwa keshapotelea ki kawaida tuu maana kwa maeneo km yale huwez muona muda wote
 
Nikageuka kwa mara ya mwisho sikumuona tena yule dada

Si alikuwa keshapotelea ki kawaida tuu maana kwa maeneo km yale huwez muona muda wote
Najua alikua keshapotea ila bado nilikua na shauku ya kumuangalia
 
Habari zenu wana Jf

Nianze na mkasa ulionikuta jana..mida flani hivi nilienda kariakoo na Dada yangu..katika mizunguko yetu yeye alikua mbele mimi nyuma

Sasa si mwajua kariakoo ilivyo na watu wengi..nikiwa katika mshangao wa kushangashangaa nguo ghafla nikapigana kikumbo na mdada amevaa baibui ameziba macho kama avatar ya madame s

Yani nikaganda ghafla uku nikimuangalia tu..akafika mbele akageuka..lahaullah!! Macho ya yule dada sikuyaelewa hata kidogo alafu yalikua hayatulii kile kiini cheusi kinafanana na kiini cha paka

Nikasema hapana sikuamini nilichokiona nikageuka kuangalia mbele huku nikijiuliza kama yule ni mtu

Nikageuka tena nyuma alikua amefika mbali lakini bado aliponiangalia macho yalikua vilevile...ghafla Dada akaniita jina langu nikaitikia "aliniuliza vipi mbona umesimama tu hapo" sikumjibu kitu

Nikageuka kwa mara ya mwisho sikumuona tena yule dada

Yani nilinyon'gonyea hadi tunatoka kariakoo bado najiuliza..hivi nilikutana na jini ama kuna binadamu wenye macho ya vile!!!

Hayo ndio yaliyonikuta siku ya jana mwenzenu
Usishituke mkuu, majini au hawa ndugu zangu wapo na always tupo nao katika maisha yetu ya kawaida tu.
 
Back
Top Bottom