Yaliyonikuta jana!!

Yaliyonikuta jana!!

  • Thread starter Thread starter Deleted member 485868
  • Start date Start date
Mwanamke anaweza kujipamba akabadilisha kila kitu kwenye uso wake..nyusi..kope..lenzi..poda..wanja wa kuchora au masinzi.

Mwisho wa siku ukajiuliza umekutana na jini au binadamu.

Pole mkuu
Inawezekana pia ikawa ivyo
 
Habari zenu wana Jf

Nianze na mkasa ulionikuta jana..mida flani hivi nilienda kariakoo na Dada yangu..katika mizunguko yetu yeye alikua mbele mimi nyuma

Sasa si mwajua kariakoo ilivyo na watu wengi..nikiwa katika mshangao wa kushangashangaa nguo ghafla nikapigana kikumbo na mdada amevaa baibui ameziba macho kama avatar ya madame s

Yani nikaganda ghafla uku nikimuangalia tu..akafika mbele akageuka..lahaullah!! Macho ya yule dada sikuyaelewa hata kidogo alafu yalikua hayatulii kile kiini cheusi kinafanana na kiini cha paka

Nikasema hapana sikuamini nilichokiona nikageuka kuangalia mbele huku nikijiuliza kama yule ni mtu

Nikageuka tena nyuma alikua amefika mbali lakini bado aliponiangalia macho yalikua vilevile...ghafla Dada akaniita jina langu nikaitikia "aliniuliza vipi mbona umesimama tu hapo" sikumjibu kitu

Nikageuka kwa mara ya mwisho sikumuona tena yule dada

Yani nilinyon'gonyea hadi tunatoka kariakoo bado najiuliza..hivi nilikutana na jini ama kuna binadamu wenye macho ya vile!!!

Hayo ndio yaliyonikuta siku ya jana mwenzenu
pole sana mkuu hilo ni jini na lilikupenda leo lazima ule mzigo
 
Back
Top Bottom