Hapo mwisho kwenye hujawahi kufanyiwa sherehe nimecheka sana.
Nikirudi kwenye mada,binafsi nimepitia hali kama yako,mzee wangu hajawahi kunipa senti kumi yake licha ya kuwa alikuwa mwalimu mwenye mshahara.
Alipostaafu 2006 akaniambia anataka anipe 5m nifanyie mtaji kwasababu hajawahi kunisadia.Hakunipa chochote ni porojo.
Nilipambana biashara hapa na pale nikanunua daladala route ya Mwenge _Bagamoyo mwaka 2008.
Hapo ndoto yangu ya kusoma ikarudi,nikajisomesha QT namshukuru Mungu nilitoboa kote,2012 nikaingia chuo kikuu na mkopo nikapata (BAED)
Baada ya kumaliza chuo nikapata kazi ,nikafundisha miaka 3 nikaacha kwasababu sikuona kama ndoto zangu zitatimia kwenye kada ya ualimu,hivyo nikarejea kwenye biashara.
Wakati wote huo mzee wangu amejiweka mbali na mimi hata nikimpigia simu anaongea ile kimachale haraka haraka ili nisimuombe kitu kumbe hajui niko vizuri wakati huo.
Point ambayo ndio tuliagana rasmi na sidhani kama nitapiga u turn, ni wakati nataka kuoa,nikamtaarifu kwa heshima tu akasema ni jambo jema tuko pamoja atanipa ushirikiano nk.Kinyume chake hakufanya chochote hata kwenda ukweni alipiga chenga akidhani kwamba nitamuambia atoe mahari (kama ilivyo desturi ya kwetu )
Kutoka hapo hatuwasiliani kabisa zaidi ya miaka 3 sasa.Habari zangu anasikia kwa ndg zangu,kijana kajenga ghorofa pale,kijana kanunua gari ya mbunge 😂 nk.Roho inamuuma lakini hawezi kuniambia nimsaidie amepigika mbaya.
Nimetoa huo ushuhuda mrefu kuwatia moyo wale wote wanaopitia hali ya kukataliwa na wazazi hasa baba zao, wapambane kana kwamba mzazi alishafariki.Hiyo hasira ya kukataliwa igeuze kichocheo cha kuchapa kazi kwa bidii na ubunifu ili siku moja uwaoneshe kwamba walibet vibaya