Yametimia: TANESCO yakiri uhaba wa umeme. Kutoa 'Taarifa' watu wapange kazi zao

Yametimia: TANESCO yakiri uhaba wa umeme. Kutoa 'Taarifa' watu wapange kazi zao

Hata kigwendu anatosha kuliko CCM.

BBA9528A-07A7-43ED-B5C6-FE7C00923B3F.jpeg
 
Waswahili wanasema usiku wa deni haukawii, leo Tanesco wametoa statement ya kuonyesha uhaba wa uzalishaji umeme kutokana na kina cha maji kupungua.
Hivyo watatoa ratiba ya umeme, watu wajipange
Waziri alisema sababu ni maintenance, lakini kumbe sio. Kazi iendelee
Eti watu waanze kupanga kazi zao

View attachment 2015253

F0BA39F7-6AFA-4311-9167-78987DD3D978.jpeg
 
Nadhani hatimae watu ndo wataelewa...

It's just last week nimehoji mara kadhaa hapa, kama sio 57% ya umeme unaotokana na gesi, nchi ingekuwa katika hali gani wakati umeme wa maji ni ONLY around 36%?!

Kiukame kidogo tu, tushaanza kutafutana...

Huku Misukule ikikazana kwamba, kwavile kuna Bwawa la Nyerere linajengwa basi ku-explore vyanzo vingine vya umeme ni kutaka kumhujumu JPM ili ionekane Mradi wa Bwawa la Nyerere haufai!!

Tuna taifa lenye viumbe wa ajabu sana...
Mkuu hapa issue ni kuanza kupanga kazi zetu Kama Tanesco walivyotushauri
 
Duh!, Haya maji yalisubiri Magufuri kutoweka ndio yameanza kupungua?.

Kwa nini tangu tupate uhuru hadi karne hii bado tunategemea mito tu, kwanini tusianze kufikiria uzalishaji wa umeme wa upepo kule kwenye Mkoa kama Singida?, Au sehemu zenye Milima?.. Halafu ile gesi toka Mtwara imeishia wapi?.

Nawashauri mnapoanza kukata umeme kila Mkoa msisahau kufanya biashara zenu za kuuza Majenereta maana kwa sasa ni kama vile ufisadi umeanza kurudi.

JPM alikuwa na mapungufu yake mengi, ila kuna mahali alifanya vizuri.
 
Waswahili wanasema usiku wa deni haukawii, leo Tanesco wametoa statement ya kuonyesha uhaba wa uzalishaji umeme kutokana na kina cha maji kupungua.
Hivyo watatoa ratiba ya umeme, watu wajipange
Waziri alisema sababu ni maintenance, lakini kumbe sio. Kazi iendelee
Eti watu waanze kupanga kazi zao

View attachment 2015253
Huyu Waziri anayevaa mashati ya mikono mirefu kisha anayakunja mpaka kwenye viwiko kama Obama, si ndiye aliyetudanganya kuwa wako kwenye "maintenance", kumbe maji hakuna, kulikuwa na sababu gani watu wazima kudanganyana hovyo?

Kuna watu tangu awamu ya 4 utendaji kazi wao ni wa kisanii sanii, uongo uongo, wizi wizi, uswahili swahili tu.
 
Back
Top Bottom