Yametimia: TANESCO yakiri uhaba wa umeme. Kutoa 'Taarifa' watu wapange kazi zao


 
Mkuu hapa issue ni kuanza kupanga kazi zetu Kama Tanesco walivyotushauri
 
Duh!, Haya maji yalisubiri Magufuri kutoweka ndio yameanza kupungua?.

Kwa nini tangu tupate uhuru hadi karne hii bado tunategemea mito tu, kwanini tusianze kufikiria uzalishaji wa umeme wa upepo kule kwenye Mkoa kama Singida?, Au sehemu zenye Milima?.. Halafu ile gesi toka Mtwara imeishia wapi?.

Nawashauri mnapoanza kukata umeme kila Mkoa msisahau kufanya biashara zenu za kuuza Majenereta maana kwa sasa ni kama vile ufisadi umeanza kurudi.

JPM alikuwa na mapungufu yake mengi, ila kuna mahali alifanya vizuri.
 
Huyu Waziri anayevaa mashati ya mikono mirefu kisha anayakunja mpaka kwenye viwiko kama Obama, si ndiye aliyetudanganya kuwa wako kwenye "maintenance", kumbe maji hakuna, kulikuwa na sababu gani watu wazima kudanganyana hovyo?

Kuna watu tangu awamu ya 4 utendaji kazi wao ni wa kisanii sanii, uongo uongo, wizi wizi, uswahili swahili tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…