Samson Kwayu
Member
- Jun 9, 2022
- 19
- 94
Imefahamika kuwa Tulia Akson Mwansasu Spika wa bunge, anaendesha genge haramu ndani na nje ya bunge la kuhakikisha wanamkata miguu mapema Mwigulu Nchemba wakimhofia kuwa anaweza kuwa tishio kubwa katika kipute cha ugombea Urais ndani ya CCM mwaka 2030, baada ya Dkt Samia kumaliza muda wake.
Imefahamika kuwa Spika Tulia na baadhi ya wanasiasa wanaopiga hesabu ya urais wa 2030 wameunda genge haramu ambalo wamekuwa wakilituma bungeni kumshambulia Mwigulu Nchemba ili kumchafua, kumbomoa na kumkosesha imani kwa wananchi mapema kabla ya 2030, imefahamika pia mikakati yao hiyo inapangwa nje ya bunge na kuja kutekelezwa ndani ya bunge chini ya usimamizi wa Spika Tulia Akson ambae anashiriki vikao hivyo vya gizani, na huwa anaingia Bungeni akiwa anayajua mabomu yote waliyoyaanda kwa siku husika na namna gani atakavyogeuka kuwa jaji wa kurahisha michezo yao.
Mtandao huo mkubwa umeundwa kwa lengo kuu la kumweka Mwigulu kwenye Kona kali kila anapoongea bungeni, lakini cha kustaajabisha hivi karibuni baadhi ya wanamtandao huo wametambua yote yanayopikwa kwajili ya kumhusisha Mwigulu wala hauhusika nayo bali huwa anatetea serikali kwa ujumla wake, na kuna siku Mwigulu alitetea reli ya mwendokasi wakadhani yeye ndie amesaini mkataba na pengine amepata ten percent but baadae wakatambua mikataba hiyo imesainiwa na watu wa Wizara ya Uchukuzi wakaishia kukunja nyuso kwa hasira kali, next time wakakomaa nae tena kwenye na EPC+F wakidhani Mwigulu ndio amesaini Fedha hizo kumbe iliyokuwepo ni EPC pekee iliyosainiwa na Wizara ya Ujenzi wakaishia kufyonza na kung’ata meno kwa uchungu.
Sote tunatambua Bungeni kila Wizara huwa zinafanya masemina na maonesho kwa wabunge wote, na Wizara zote zimefanya lakini cha kustajaabisha Spika na genge lake wamezuia Semina ya Mwigulu kwasababu wanahisi Mwigulu akifanya atapata umaarufu na kuungwa Mkono na wabunge wote na hiyo itakuwa hatari kwenye harakati za Spika Tulia za kuutaka Urais 2030.
Mimi binafsi nikiri nilishaanza kumchukia Mwigulu, lakini nimegundua ulikuwa ni mchezo mchafu wa kumkwamisha, lakini kumbe huyu ni mtu makini anayefanya kazi ya umma kwa uzalendo mkubwa, weledi na uadilifu wa hali ya juu sana. Sasahivi nimeelewa kwanini hata kajambo kadogo tu ka Mwigulu lazima Spika Tulia atakashikia sana bango na anajigeuza kuwa Jaji alafu kina Halima, Mpina na wengine wanakuwa waendesha Mashtaka, shame on them all na kwa taarifa yenu wote wananchi tumewagundua mapema sana.