Yanayoendelea CCM yamenikumbusha kisa cha Rais Ben Ali wa Tunisia mwezi January, 2011

Yanayoendelea CCM yamenikumbusha kisa cha Rais Ben Ali wa Tunisia mwezi January, 2011

Wakati wa Maandamano ya kumtaka aliyekuwa Rais wa Tunisia kujiuzuru na kuondoka Madarakani, Rais huyo Marehemu Ben Ali alimtegemea sana Mkuu wake wa majeshi na Waziri wake wa Ulinzi kutuliza hali ili aendelee kuwa Rais.

Maandamano yaliposhika kasi, Ben Ali alipanda ndege na kukimbilia Saudi Arabia.

Mawasiliano ya mwisho yaliyonaswa na shirika la habari la Uingereza BBC yalionesha akiwa kwenye ndege Ben Ali alikuwa akiwasiliana na Mkuu wa Majeshi na kuuliza kama hali imetulia ili arejee.

Simu za mwisho za Ben Ali zilionesha how frustrated He was. Alikuwa anauliza kama mtoto mdogo vipi huko hali ikoje Mkuu wangu wa Majeshi nirudi? Mkuu wa Majeshi mwisho akampasukia Ni ushauri wangu usirejee, siwezi kukuhakishia usalama wako endapo utarejea.

Tukio hili lililotokea mwaka 2011 limenikumbusha kisa kilichotokea hapa Dodoma baada ya mtu kupanda ndege kwenda Kizimkazi hadi kufanya Vikao vya Kamati Kuu kuahirishwa.

Maswali ninayojiuliza ni Je wajuba wamepata akili? Wataweza kumwambia baki huko huko kwanza ili waiponye nchi na kuipatia Reforms ili itoke mikononi mwa Wanasiasa wezi/ wahuni na iendeshwe na mifumo chini ya Katiba Bora?

No Reforms No Election ✊️ ✌️

View: https://www.threads.com/@leonardsoza/post/DMR5P_utIB0?xmt=AQF0p1ElZGEEAT5jwSOE1rdehbsXgxH3Opr3SPlfIN3Aqg
 
Zine El Abidine Ben Ali alikimbia nchi baada ya waandamanaji kuzidi nguvu vyombo na ulinzi na usalama. Walikuwa wanaua waandamanaji kila siku na bado wanaendelea kuongezeka zaidi ya jana.
Na kadri siku zinavyoenda wanakuwa na fujo, wanavamia ofisi za serikali, ikawa ni vita baina ya waandamanaji na vyombo vya ulinzi.

Maafisa wakaanza kujiuliza sasa cha kufia nini maana kama wameua na kujeruhi ila hali hairudi nyuma sasa wataishia wapi. Ndipo jeshi likazingira makazi yake ila Ben Ali na familia yake wakaenda Airport na jeshi likawaruhusu waondoke kisha likafunga anga.
Alivyokuwa kwenye ndege ndivyo aliongea na huyo mkuu wake wa majeshi ambaye kwa lugha ya mazungumzo inaonekana alikuwa anamheshimu sana, hakusema asirudi ila alisema hawezi kumuhakikishia usalama endapo atarudi.

Hiyo situation ni kubwa sana, hii ya kwetu hamna kitu. Sisi hatuna politics ngumu hata, cheo cha Naibu Rais wa Kenya kina changamoto kuliko cheo cha Rais wa Tanzania.
Mwishowe ikawaje mkuu alirejea tena?
 
Ikulu ya Dodoma mtego ule.

Kila kitu kiko wazi. Ni dakika tu watu wanarudisha mpira kati.
Rais akimbie kisa chama hakitaki kumpitisha kugombea?
Chama hiki hiki ambacho kajiteua mwenyewe na wameufyata.

Ni mwanachama gani au mtu gani ndani ya CCM mwenye uwezo wa kumtoa Rais ikulu kwa sababu za chama? Ni organ gani ya CCM inaweza muondoa Rais?
 
Rais Samia amefanya kadiri alivyoweza kuifikisha nchi Toka mwaka 2021 alipotuacha rais JPM mpaka sasa.Kwa Hali ilivyo Bora angewaachia wanaccm wengine kusonga mbele kwenye nafasi hiyo
Urais siyo kufanya ''kadiri unavyoweza'' bali ni kufanya ''kadiri inavyotakiwa''. Ukisema ''kadiri anavyoweza'' inawezakana akawa mtu mwenye uwezo mdogo kabisa, huoni ni hatari? Suala la urais siyo kwa kila mtu ndiyo maana unaapishwa na kuwekewa malengo ya kufikia.
 
Mwishowe ikawaje mkuu alirejea tena?
Aliamua kutorudi baada ya kutohakikishiwa usalama. Maana ndugu zake na binamu zake aliokuwa amepachika kwenye nafasi mbalimbali walikuwa wameanza kuzuiliwa kuondoka nchini Tunisia.

Aliomba uhamisho nchini Saudi Arabia na akakubaliwa kwa sharti la kutowahi kujiingiza kwenye siasa tena.
 
Rais akimbie kisa chama hakitaki kumpitisha kugombea?
Chama hiki hiki ambacho kajiteua mwenyewe na wameufyata.

Ni mwanachama gani au mtu gani ndani ya CCM mwenye uwezo wa kumtoa Rais ikulu kwa sababu za chama? Ni organ gani ya CCM inaweza muondoa Rais?
Kwa nini kakimbia?
 
Kwa nini kakimbia?
Bado hujajibu swali.

Nikija kwenye kujibu swali lako, Rais hajakimbia. Hana wa kumkimbia.

Turudi kwenye swali langu. Pale CCM ni nani au ni chombo gani cha chama kinaweza mtoa Rais na Mwenyekiti wao madarakani?
 
Bado hujajibu swali.

Nikija kwenye kujibu swali lako, Rais hajakimbia. Hana wa kumkimbia.

Turudi kwenye swali langu. Pale CCM ni nani au ni chombo gani cha chama kinaweza mtoa Rais na Mwenyekiti wao madarakani?
Mbona hatumuoni hapa Ikulu?
 
Mbona hatumuoni hapa Ikulu?
Hakuna sheria inayosema Rais anapaswa kukaa ikulu siku zote.

Magufuli alikuwa anaenda Chato hadi anakutana na delegates wa kimataifa uko, hadi anakutana na mawaziri wanamfuata uko kina Mwigulu Nchemba. Alikuwa anakaa kule hadi analala juu ya mawe.
Kikwete alikuwa anaenda Msoga anakaa siku kadhaa.

Nyinyi huyu kutoonekana ikulu siku mbili tatu mnasema amekimbia. Mtu yeyote ambaye amewahi kanyaga ikulu, achana na kufanya kazi uko hawezi andika eti Rais amepakimbia kisa sijui nani wa CCM. Rais anaweza muweka house arrest kenge yeyote ndani ya CCM na msifanye kitu. Rais hata fomu ya kugombea hajachukua, kajiteua akiwa anaongoza kikao na hao unaosema watamfukuza ikulu wakiwepo wote, na aliyempinga kakatwa jina ubunge jimboni.

Mnaota nyie.
 
Back
Top Bottom