Yanayoendelea CCM yamenikumbusha kisa cha Rais Ben Ali wa Tunisia mwezi January, 2011


View: https://www.threads.com/@leonardsoza/post/DMR5P_utIB0?xmt=AQF0p1ElZGEEAT5jwSOE1rdehbsXgxH3Opr3SPlfIN3Aqg
 
Mwishowe ikawaje mkuu alirejea tena?
 
Ikulu ya Dodoma mtego ule.

Kila kitu kiko wazi. Ni dakika tu watu wanarudisha mpira kati.
Rais akimbie kisa chama hakitaki kumpitisha kugombea?
Chama hiki hiki ambacho kajiteua mwenyewe na wameufyata.

Ni mwanachama gani au mtu gani ndani ya CCM mwenye uwezo wa kumtoa Rais ikulu kwa sababu za chama? Ni organ gani ya CCM inaweza muondoa Rais?
 
Rais Samia amefanya kadiri alivyoweza kuifikisha nchi Toka mwaka 2021 alipotuacha rais JPM mpaka sasa.Kwa Hali ilivyo Bora angewaachia wanaccm wengine kusonga mbele kwenye nafasi hiyo
Urais siyo kufanya ''kadiri unavyoweza'' bali ni kufanya ''kadiri inavyotakiwa''. Ukisema ''kadiri anavyoweza'' inawezakana akawa mtu mwenye uwezo mdogo kabisa, huoni ni hatari? Suala la urais siyo kwa kila mtu ndiyo maana unaapishwa na kuwekewa malengo ya kufikia.
 
Mwishowe ikawaje mkuu alirejea tena?
Aliamua kutorudi baada ya kutohakikishiwa usalama. Maana ndugu zake na binamu zake aliokuwa amepachika kwenye nafasi mbalimbali walikuwa wameanza kuzuiliwa kuondoka nchini Tunisia.

Aliomba uhamisho nchini Saudi Arabia na akakubaliwa kwa sharti la kutowahi kujiingiza kwenye siasa tena.
 
Kwa nini kakimbia?
 
Kwa nini kakimbia?
Bado hujajibu swali.

Nikija kwenye kujibu swali lako, Rais hajakimbia. Hana wa kumkimbia.

Turudi kwenye swali langu. Pale CCM ni nani au ni chombo gani cha chama kinaweza mtoa Rais na Mwenyekiti wao madarakani?
 
Bado hujajibu swali.

Nikija kwenye kujibu swali lako, Rais hajakimbia. Hana wa kumkimbia.

Turudi kwenye swali langu. Pale CCM ni nani au ni chombo gani cha chama kinaweza mtoa Rais na Mwenyekiti wao madarakani?
Mbona hatumuoni hapa Ikulu?
 
Mbona hatumuoni hapa Ikulu?
Hakuna sheria inayosema Rais anapaswa kukaa ikulu siku zote.

Magufuli alikuwa anaenda Chato hadi anakutana na delegates wa kimataifa uko, hadi anakutana na mawaziri wanamfuata uko kina Mwigulu Nchemba. Alikuwa anakaa kule hadi analala juu ya mawe.
Kikwete alikuwa anaenda Msoga anakaa siku kadhaa.

Nyinyi huyu kutoonekana ikulu siku mbili tatu mnasema amekimbia. Mtu yeyote ambaye amewahi kanyaga ikulu, achana na kufanya kazi uko hawezi andika eti Rais amepakimbia kisa sijui nani wa CCM. Rais anaweza muweka house arrest kenge yeyote ndani ya CCM na msifanye kitu. Rais hata fomu ya kugombea hajachukua, kajiteua akiwa anaongoza kikao na hao unaosema watamfukuza ikulu wakiwepo wote, na aliyempinga kakatwa jina ubunge jimboni.

Mnaota nyie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…