Simuoni JK akiwa amepunguza mahaba yake kwa kina Makamba zaidi zaidi namuona akiwa huru ndani ya Chama.
Wastaafu waliomtangulia wameshaaga dunia hivyo yeye ndiye mkongwe wa CCM tofauti na siku za nyuma walipokuwepo kina RIP Mkapa, Mwinyi wakongwe waliomtangulia na kuwa na uwezo wa kumkosoa hadharani muda wowote.
Samia anapowavuta hao kina Sabaya, Biteko na Makonda anatengeneza kambi yake mwenyewe kwa ajili ya 2025, hivyo unapoona Nchimbi anamkosoa hadharani Makonda anakuwa akifikisha ujumbe kwa Samia kwamba mambo sio rahisi kihivyo kama anavyodhania.
Lakini Mungu anaipenda sana Tanzania, hii ni nchi iliyowekwa chini ya usimamizi wa nguvu za Mungu siku ya tarehe 8 Desemba 1961 kina Makamba na wengine wenye sifa za upigaji wasahau kabisa kuja kuwa warithi wa Samia atakapostaafu.