Yanayoendelea ndani ya uongozi wa CCM na serikali yanatafakarisha

Samia huyo huyo aliwahi kusema kwa kejeli jukwaani kwamba wapige kura wasipige CCM itashinda tu. Haya tunayaongea tukiwa watu wa nje tunaotazama ndani. Ukikaribia uchaguzi wanakaa pamoja na kuja na suluhisho la shida zao wakitambua ukubwa wa madaraka waliyonayo mbele ya mamilioni ya watanzania.

Wanaweza kukwaruzana lakini linapokuja suala la kulinda mkate wao haraka sana wanakuwa kitu kimoja. Samia ameshawanunua wanasiasa wengi hata wale wenye kuheshimika mbele ya jamii, kwa kufanya hivyo keshapunguza idadi ya maadui wa kweli wenye kuweza kuudhuru uongozi wake.
 
Hivyo tusiegemee kwenye hoja ya uanamke wa Samia, waliopendekeza jina lake ni binadamu kama mimi na wewe na hawakuona kwa namna yoyote ile kuwa mwisho wa JPM ungekuwa ni March 17 2021.
1. Hoja ya jinsia ya mwanamke na uanamke wa Samia Suluhu Hassan ina - matter and it's so powerful kuliko unavyowaza ndugu Steven Joel Ntamusano.

2. I agree that, Rais Samia Suluhu Hassan binadamu tu kama ulivyo wewe. Lakini yeye ni MWANAMKE na wengine ni WANAUME. Hiyo ndiyo tofauti kuu.

Na kumbuka ulimwengu huu uko kwenye taabu na mahangaiko kwa sababu mwanamke ndiye aliyedanganywa na shetani (nyoka) na kusababisha watu tuangukie ktk mikono ya adhabu ya Mungu..
Huyo huyo mwanamke amekuwa na bahati mbaya ya kuletwa huku bara na kupewa cheo na JK, kwake JK ni sawa na kiongozi anayeendelea kuwa hai miaka na miaka, hawezi kuusahau mchango wa JK katika uongozi wake hata akija kustaafu.
Na hilo👆👆👆ndilo tatizo na unathibitisha mwenyewe hoja yangu.

Mwanamke hajawahi kuwa na hataweza kuwa independent hata siku moja. Siku zote atamtegemea mwanaume tu maana yaye ndiye kichwa chake.!!
Tatizo ni mipango ya Mungu namna inavyofanya kazi, alitaka mpaka muda huu wastaafu wote isipokuwa JK wawe wameshatangulia mbele ya haki, tatizo lipo kwa hiyo JK namna asivyoonekana kujali wala kuguswa na vilio vya watu huku mtaani.
Ndugu Steven Joel Ntamusano tatizo sio JK kuwa hai. Tatizo ni kuwa tuna "Rais mwanamke". Huelewi nini hapo? Wakati wa Hayati John P. Magufuli huyu JK si alikuwepo? Unadhani ni kwanini hakukuwa na ujinga huu unaoendelea sasa? Jibu ni kwa sababu tuna "Rais mwanamke.."

Na nikuhakikishie hili kuwa, hata kama huyu JK akiondoka leo, atakuwepo mwanaume mwingine ku - take control juu ya huyu "Rais mwanamke". Hii ni asili (nature). Ndivyo ilivyoumbwa na ndivyo ilivyo..

By the way, unadhani ni JK tu yupo nyuma ya huyu mwanamke? Wako kibao tena wengine wateule wake na wote wanampiga kamba kila siku na ndio maana hii nchi inajiendea tu. Lakini kwa sababu ya uvumilivu na neema ya Mungu, tupo tunaishi..
 
Tafuta takwimu za Samia utazame mambo ambayo ameshayafanya kwa miaka hii mitatu, labda itakusaidia kuondokana na hii kasumba ya mfumo dume iliyokujaa kichwani mwako.

Anafanya mengi sana tena makubwa hata huyo JPM watu walimlaani kwa maamuzi yake baadhi yaliyojaa ukatili usiosemeka hadharani.

Kwa kuwa alikuwa mtoto wa kiume watu waliyasamehe yote mabaya aliyolaumiwa kuyafanya akiwa Ikulu. Makonda akiwa mkuu wa mkoa wa Dar alipigwa stop ya kwenda USA, tafuta katika historia ni RC gani aliyewahi kuzuiwa kuingia ndani ya nchi nyingine, hakuna!.

Huyo Makonda alizuiwa akiwa na bosi wake mwanaume pale Ikulu!, unyama mwingi tu kaufanya lakini anapigiwa makofi kwa sababu ya jinsia aliyokuwa nayo. Tubadilike.

Laumu CCM kwa kumpitisha akiwa mgombea mwenza, usimlaumu yeye kama yeye unapoteza muda tu.
 
Tafuta takwimu za Samia utazame mambo ambayo ameshayafanya kwa miaka hii mitatu, labda itakusaidia kuondokana na hii kasumba ya mfumo dume iliyokujaa kichwani mwako.
Ishu hapa sio takwimu. Unaweza kufanya hili au lile lakini overall haikufanywi wewe uwe mwanamme. Elewa kuwa Samia Suluhu Hassan ni mwanamke...
Anafanya mengi sana tena makubwa hata huyo JPM watu walimlaani kwa maamuzi yake baadhi yaliyojaa ukatili usiosemeka hadharani.
Afanye hili au lile, hiyo haindoi ukweli kuwa yeye ni mwanamke. Jinsia yake tu ya "kike" inam - disqualify kuwa kiongozi wa juu (Rais) wa nchi hii. This is nature. Huo ndio uumbaji. Ndivyo tulivyoumbwa..
Huelewi nini mpaka hapo ndugu Steven Joel Ntamusano? Ni kwa sababu huyu ni mwanamke. Hatutaki nafasi hiyo kushikiliwa na mwanamke. Period..!!

Familia yenye mwanaume, mwanamke literally hawezi kuwa kichwa cha familia bila kujali mwanaume huyo ana udhaifu au mapungufu gani. Hiyo ni principle ya nature inavyotaka..!
Huyo Makonda alizuiwa akiwa na bosi wake mwanaume pale Ikulu!, unyama mwingi tu kaufanya lakini anapigiwa makofi kwa sababu ya jinsia aliyokuwa nayo. Tubadilike.
Nisome hapo juu 👆👆👆
Laumu CCM kwa kumpitisha akiwa mgombea mwenza, usimlaumu yeye kama yeye unapoteza muda tu.
Yes, CCM inalaumiwa big time. Hata wao bila shaka hawakuwahi kujua kuwa hatimaye taifa hili lingeweza kufiwa na Rais wake mwanaume na eti mwanamke awe Rais badala yake..

It's a lesson. Wote tumejifunza. Sasa tunajua na tumeona wote jinsi jambo hili lisivyofaa.!
 
Pole sana mkuu, waliompa huo umakamu na baadae urais ni wanaume kama wewe, hapo ndio kichekesho kinapoanza. Huwezi kusema hutaki awe rais hutaki kuongozwa na mwanamke wakati ndio yupo ikulu akiongoza nch!.

Hizi ni akili fulani za kitoto sana. Hutaki vipi wakati anapigiwa mizinga kila anapokwenda?.

Hutaki vipi rais mwanamke wakati keshafanikisha safari ya kwanza ya SGR ya Dar mpaka Dodoma?.

Huoni kwamba unajipa tu mateso ya moyo yasiyo na kichwa wala miguu!?.

Kuwa kichwa au shingo ya familia hayo ni masuala yake huko nyumbani na mume wake hayatuhusu sisi huku majumbani mwetu na maofisini.

Narudia tena kukwambia kwamba lawama zako peleka kwa kamati kuu na halmashauri kuu za CCM zilizopitisha jina lake huku zikitambua kuwa kwa mujibu wa katiba akiaga dunia rais anayechukua mikoba ni makamu wake. Peleka lawama zako huko vinginevyo ni sawa na kupiga ngumi ukuta, unapoteza tu nguvu na muda wako kulalamika.

Kwa taarifa yako miradi yote aliyoiacha JPM inamalizwa mmoja baada ya mwingine, mnabakia kulalamika tu huku mitaani hamna uwezo wowote wa kubadilisha hii hali na inaendelea kuwepo mpaka tunapoaga dunia.

Pia uwe na adabu Mama aliyekuweka tumboni miezi tisa na kuja kukuzaa, kukunyonyesha, kukulea mpaka umekua ni mwanamke pia.

Usijisahau na kiburi kikakujaa mpaka kukupofusha macho.
 
Vizuri na hii minyukano ni kwa afya ya Taifa.

Mungu akipitisha fimbo yake, kama haujirudi na kujisahihisha, kinachofuata ni kama jiwe linavyoelea kwenye sakafu za vilindi vya maji
 
Kwa akili yako siasa hai athiri uchumi??
 
Umechanganya, Makonda, Nchimbi, Magufuli, Kikwete, Samia na "vijana wengine", mpaka nimeshindwa ku6elewa ujumbe uliotaka juufikisha.

Wewe.ni CCM au Chadomo?
 
Pole sana mkuu, waliompa huo umakamu na baadae urais ni wanaume kama wewe, hapo ndio kichekesho kinapoanza. Huwezi kusema hutaki awe rais hutaki kuongozwa na mwanamke wakati ndio yupo ikulu akiongoza nch!.
Ndugu Steven Joel Ntamusano, mwanaume akiwa kwenye nafasi yake sahihi (in his right position) akikosea, kamwe hiyo haiwezi kuwa ishu ya kujadili, huwa inaeleweka na huwa tunasonga mbele.

Ni makosa makubwa kuruhusu mwanamke kuwa kwenye nafasi isiyo yake.

Halafu anaharibu then watu wanaanza ku - justify uharibifu wake ya kuwa "naye ni binadamu..."

Yes, ni binadamu. Lakini ni binadamu wa jinsia ya ya kike. Hii jinsia ya kike naturally ina position yake inayostahili kuwepo ktk jamii.

Unajua ni nini kilitokea pale bustanini Eden hata kosa kufanyika na kumwingiza mwanadamu ktk taabu na mahangaiko?

Nitakusaidia kujibu.

Kilichotokea ni mwanamke (Eva au Hawa( kuwa kwenye nafasi (position) ambayo hakupaswa kuwa, nafasi ya mwanaume ambayo ni nafasi ya maamuzi na utawala.

Kilichotokea ni mwanamke huyu kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kuuleta ulimwengu wote ktk hukumu ya dhambi.!

Tanzania Tunataka haya?.........NO WAY....!!

Turudi kwenye hoja yako kule juu👆👆👆

Kwamba, aliwekwa na wanaume? Nakubali kwa kusema, Yes.

Lakini wanaume hawa walikosea. Wanapaswa kurekebisha kosa hili once and for all.

This is going to be done!
 
Aseee umemlilia mungu sana hadi nimeigopa
 
Umeandika pumbu tupu mkuu The Palm Beach.

Ujerumani imeongozwa na mwanamke kwa miaka 15 {2006 - 2021}, Tanzania inapewa misaada na Ujerumani kila kukicha.

Na uchumi wa Ujerumani ndio unaoongoza barani Ulaya, wao na wewe nani wenye hekima zaidi katika kuwafahamu wanawake na udhaifu wao?.

New Zealand imeongozwa na mwanamke katika kipindi cha COVID 19 na ni mojawapo ya nchi zenye vifo vichache vya ugonjwa huo hatari ulioua mamilioni ya watu.

Wewe ni mhanga wa MFUMO DUME na pole za dhati ziufikie moyo wako.

Narudia tena kukueleza kama unazo akili timamu hutamlaumu Samia kwa makosa yaliyofanywa na CCM wenyewe, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

Na ni kasumba za kipuuzi kuamini kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu, angekuwa dhaifu asingekubeba wewe miezi tisa tumboni na akahangaika na mimba yako mpaka ukazaliwa.

Unapoteza muda wako kuumia moyoni kisa Tanzania inaongozwa na Mwanamke. Anaweza kuiongoza mpaka 2030 wakati huo pengine mimi na wewe tumeshatangulia mbele za haki.

Kwa sababu aliwekwa na wanaume na wao walikosea unamshauri aachane na urais ili ampishe mwanaume aongoze?. That is a stupid opinion.
 
Ukiwa na akili hasi utakuwa unatafuta mabaya tu ya SSH kwa sababu ya jinsia yake lakini ukiwa mtu mwenye upeo na mwenye kujielewa hutapoteza muda wako katika kumhukumu kwa mujibu wa jinsia aliyopewa na Mungu.

Hizi ni akili ambazo wajinga tu wanaziona ni za kisasa. SSH anamalizia kujenga daraja la Busisi kule Mwanza.

Treni ndio hiyo imeshafanya safari ya kwanza kutoka Dar mpaka Dodoma.

Na miradi mingi mingi sana iliyoachwa na marehemu JPM inakwenda kufikia ukingoni muda huu, haya yote yatazamwe katika utendaji wa Rais Samia.

Ni upuuzi kuanza kutenganisha jinsia yake na namna anavyozimaliza ahadi zote alizoahidi siku alipokabidhwa kijiti baada ya kuaga dunia hayati Magufuli.
 
Umeandika pumbu tupu mkuu The Palm Beach.
Kwa ufahamu na akili yako ni pumba. Lakini unaweza kupingana na nature?
Ujerumani imeongozwa na mwanamke kwa miaka 15 {2006 - 2021}, Tanzania inapewa misaada na Ujerumani kila kukicha.
Unafikiri shetani naye hafanyi miujiza? Unadhani shetani hatendi na kuleta matokeo? Je, kwa kuwa analeta matokeo unadhani anaweza kuchukua nafasi ya Mungu?

And remember this. Two wrongs can't make right..!

Forget about Germany, New Zealand, India, Liberia and other nations. Makosa ya wengine hayawezi kutupa uhalali sisi nasi kufanya makosa kama hayo!
 
Kwani Rais angewaweka pembeni hao Vijana wa Mwendazake Kuna shida gani?
Kwa hivyo unataka kumpangia Mh.Samia watu wa kufanya nao kazi?

Yeye hafuati hisia zako wala zangu Bali anapokea ushauri toka kwa watu wake anao waamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…