Siku zote chama kinatakiwa kuwa na wananchi ili wakiunge mkono. Kwa kuwashawishi wananchi, chama chaweza kubadilisha team yake serikalini kutokana na hoja za wananchi.Mtakuja kutuambia. Hii Secretariat ya Nchimbi ni mbovu kuwahi kutokea. Ni zaidi ya ile ya Wilson Mkama. Picha linaanza wanafanya kazi na kutoa hotuba kama vile ni watumishi wa umma(civil servants). Wamegeuka wasemaji wa maafisa masuhuli na Mawaziri katika maeneo tofauti tofauti. Nadhani hili limechangiwa pia name ukweli kwamba wengi wao wamezoea kuwa watendaji katika maeneo kadha waliopita.
Makonda ndiye anajua na alijua kutafsiri maana halisi ya chama cha siasa, chama tawala na maana ya chama kuunda serikali.
Chama tawala hakipaswi kujiunga katika mlolongo wa Government Bureaucratic system but it should commands the system. Nchimbi and Co. ndio kwanza wameanza ziara ya kwanza lkn kwa jicho la tatu, wanafanya kazi kama bureaucrats wa serikali.
Wanashindwa kutafsiri majukumu yao kwa niaba ya chama. Wanashindwa kutafsiri supremacy ya chama over the govt system. Wanashindwa kukaa upande wa Wananchi ama kuvaa viatu vya wananchi. Wasipobadilika, itakuja kuwa Secretariat Mbovu kuwahi kutokea ndani ya chama cha mapinduzi.
Hata hivyo, kwa sababu ya siasa za uchawa wa kutafuta teuzi, chama tawala, watumishi wa serikali na vyombo vya dola huimba mapambio ya kusifu na kuabudu.
Utamaduni huu utabadilika pole pole kama wakiwepo viongozi wanaoona mbali (kwa vyama vyote).
Siasa lazima zijengwe kwa hoja zenye mantiki badala ya uchawa (wawepo watu wafuasi wa viongozi, siyo chawa, ambao wanaweza kujenga hoja).