Yanayoendelea sasa CHADEMA ni mpango toka nje kuingiza nchi matatizoni. Serikali ina kazi ngumu huko mbele

Yanayoendelea sasa CHADEMA ni mpango toka nje kuingiza nchi matatizoni. Serikali ina kazi ngumu huko mbele

Mpuuzi kweli wewe ila siasa za DHULUMA NA MAUAJI ndiyo suluhisho siyo? Lini ulikemea mauaji ya kutisha nchini! Au hukuwahi kuyasikia?

Inasikitisha sana. CCM ni chama primitive, kinachoendesha siasa za kijambazi. Hakuna awamu ambayo CCM haijawahi kuwaua inaoamini ni wapinzani.

Siamini kama kuna jema wapinzani wanaweza kupata toka kwa CCM. Watanzania waendelee kudai haki kwa njia zote zijazoweza kukomesha udikteta wa CCM. Kwa kufanya hivyo, hakuna wanachokipoteza zaidi ya kongwa zao za kuobewa. Ni kitu gani kibaya ambacho CCM inaweza kufanya kwa sasa ambacho haikuwahi kufanya huko nyuma.

Kuua - wameua wakati wote

Kuteka - wamefanya hivyo wakati wa Kikwete na kuzidi wakati wa Magufuli

Kufunga - walifanya hivyo kipindi cha Mkapa, Kikwete, na zaidi wakati wa Magufuli

Kufilisi - walifanya hivyo wakati wa Mkapa, Kikwete, na zaidi wakati wa Magufuli
 
Sijaona elements za nchi za nje ila nilichokiona Kwa uzoefu wangu mdogo wa siasa zetu ni kuwa kwakua huu ni utawala mpya jamaa wanapima tu kina cha maji
 
Tanzania inatamaniwa sana na siku zote maadui wapo kazini kuhakikisha tunaondoka kwenye mstari.

Kilichowashangaza nai kwamba mambo yanaendelea kama kawaida.

Kama nchi inaingia kwenye vurugu kunakuwapo hakuna shughuli za kuchumi zinazoendelea kustawi maana watu watakaa ndani, jamii itadumazwa na hakuna shule wala shuguli za huru za kijamii.

Mitaani kutatokea uporaji na mauaji ya wale wanoandamana.

Nchi ikiwa na vurugu inageuka kuwa tegemezi.
Tupo kwenye mstari gani
 
Hivyo kwa maoni yangu napendekeza Chadema wajikite katika kujiandaa kuchukua majimbo ambayo yatawasaidia kuongeza idadi ya wabunge kule bungeni ambao wanaweza kuweka hoja yenye nguvu.
Chedema Wajiandae Kuchukua Majimbo Kwa Katiba Gani Au Umesahau Kilichotokea kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa Na Uchaguzi Mkuu Uliopita?

ACHA KUJITOA UFAHAMU.
 
Mimi ni mpenda mabadiliko na ni mwanaharakati.

Nilikuwa pamoja na akina BAK hapa enzi zetu.

Ningekuwa na uwezo wa kuanzisha chama ningefanya hivyo.

Ila siasa za Tanzania zilipofikia kwa sasa ni hatari sana.
Hamna hatari yoyote isipokuwa ccm iko siku zake za mwisho mwisho ndio maana inarusha mateke ili kukata roho.
 
Mstari wa kujitegemea kiuchumi.
Unaweza nisaidia initiative za kitakwimu ambazo for 60 years zimefanyika na zinaonyesha tunakwenda kujitegemea kiuchumi angalau 30 years to come??

Pili, ni secta gani ambayo ndio kipao mbele chetu kuelekea huko kwenye economic independence na mpaka sasa percentage zake zimefika ngapi kufikia hiyo status!
 
Waufufua kwa vurugu mchakato uloletwa na CCM na ukazimwa na CCM?

Mnajifanya hamnazo? Kwamba kuna wa nje? Thubutu!

Wananchi hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na uhuru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk.

Mwambie aliyekutuma matakwa hayo mzizi wa fitna ni katiba mpya!

Mtamlaumu sana dobi kaniki ni rangi yake.
 
Sina akili lakini siko kama ZWAZWA wewe kuja humu kuandika UZUSHI ili kutafuta teuzi nakuuliza maswali unayakimbia. Upumbavu wako mwisho lumumba siyo humu.
Naomba unielewe, mimi sijaandika uzushi nimeandika maoni ya ninachoikiona kwa kuangalia mwenendo wa Chadema.

Nimesikiliza na kupima kinachozungumzwa na Mbowe, Tundu Lissu, Mdude na John Mnyika.

Kisha niimetoa maoni.

Hivyo maoni ni tofauti na mtizamo yanaweza kuwa na chanya na hasi ndani yake.

Ila huwezi kuita maoni ya mtu upuuzi na kumshambulia binafsi kwa malengo unayoyafahamu weye.

Pia, mimi sina haja ya uteuzi kutoka kokote, nafasi yangu nje ya JF ni ya kudumu na ni nzuri kuliko hata huyo Mbowe na wengine chini ya mama yetu hivyo sina shida.
 
Pia nimewahi kusema kuwa Chadema imekosa wanamkakati au "strategists" ambao wataisaidia kuogelea kwenye bahari ambayo imejaa maji mengi ya CCM na vifaa vyake vyote bunge, mahakama, polisi, jeshi na mamlaka zingine.
Mahakama ni kifaa cha CCM....

Am kweli tunahitaji katiba mpya sasa.
 
Chadema ni chama cha siasa chenye wanasiasa ambao si makini.

Ni chama kilichokusanya watu wanojiita wanasiasa lakini hawana mbinu za kuishi kwenye siasa.

Miaka mitano ilopita Chadema walipata shida na hawakuweza kujinafasi na serikali ambayo iliongozwa na raisi ambae hakuwa tayari kuvumilia vurugu iwe maneno au vitendo.

Sasa yupo raisi Samia Hassan huu ndo ulikuwa wakati wa Chadema kuketi chini na kupanga mikakati mipya ambayo itaendana na mwendo wa serikali ya sasa.

Nimewahi kusema mara nyingi kuwa Chadema haina wanasiasa makini ambao wanaweza kutofautisha siasa za vurugu na siasa makini za majibizano ya hoja kwa ustaarabu.

Pia nimewahi kusema kuwa Chadema imekosa wanamkakati au "strategists" ambao wataisaidia kuogelea kwenye bahari ambayo imejaa maji mengi ya CCM na vifaa vyake vyote bunge, mahakama, polisi, jeshi na mamlaka zingine.

Mwanamkakati kazi yake kubwa ni kutumia kampeni ambazo zitahakikisha wapiga kura wanabadili mawaqzo yao juu ya chama kingine na kuwa tayari kuwapa kura.

Kazi zingine ni kufanya kura za maoni kuona kama chama kinakubalika kwa wapiga kura na kwa asilimia ngapi, kutumia teknolojia na mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe halisi wa kisiasa na pia kuendesha harambaee za kuchangisha mifumo ya chama ili kupata fedha za kujiendesha.

Ni hili suala namba tatu ndilo lingeiwezesha Chadema kujenga ofisi yake maalum ya makao makuu ambayo ingekuwa inatambulika rasmi badala ya kajumba ka pale Ufipa Street.

Siasa ambazo Chadema inaendesha sasa hivi za kudai katiba mpya haziwezi kuiyumbisha CCM hata kwa dawa.

Sanasana ni kwa wanasiasa wa Chadema na wafuasi wao kuketi chini na kupanga mbinu mpya badala ya maandamano ambayo ni dhahiri yatapata taabu kuruhusiwa na polisi.

Katiba ndo msingi wa sheria na hutoa mwongozo namna serikali inavyotenda shughuli zake za kila siku.

Hivyo katiba ya nchi ni muhimu na pia utaratibu mzima wa kutaka kuibadili pia ni muhimu.

Bado Chadema haiweki wazi kuwa yataka katiba mpya au mabadiliko ya katiba tulio nayo.

Lakini Chadema ingeweza kuketi na kushawishi ili kupata washirika kutoka CCM kwa maslahi ya taifa na kutaka katiba ifanyiwe marekebisho kuwa wabunge wasijiongeze mishahara kiholela.

Serikali ya awamu ya sita yapaswa kusikiliza dai la tume huru. hili dai ndo msingi wa vurugu zinazoweza kujitokeza hapa nchi ama leo au siku za usoni.

Kuna dalili zote zionyeshazo kuwa nguvu kubwa kutoka nje ya nchi ipo nyuma ya hizi kelele za katiba mpya au tume huru.

Suala ni je ni kelele za msingi au ni nguvu tu ya kutaka kuhakikisha CCM inaondolewa madarakani?

Kabla ya uchaguzi wa 2015 CCM ilikuwa imefikiriwa katika majukwaa ya kimataiofa kuwa ni chama kilichohitaji kuondoka kupisha chama kingine ambacho kingekuja na mawazo mapya.

Ni pale CCM ilipompata hayato John Magufuli na baada ya miezi sita ya kwanza ndipo majukwaa hayo yalipobaini kuwa CCM huenda imejigawa ila ni ileile.

Kelele za Katiba mpya au tume huru ya uchaguzi hazitaisha leo.

Ila katiba mpya si rahisi kuipata bila kuwepo kura ya maoni ambayo ndo itatoa mwanga kuwa wananchi wanataka nini.

Hivyo kwa maoni yangu naona Chadema na wanaharakati wote wanapaswa kupigania kuwepo kura ya maoni.

Pia kuhusu tume huru ni kwamba ni lazima wabunge wa upinzani bungeni wawe na ushawishi wa kuweza kuleta bungeni wazo la kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo ndo itasimamia zoezi la uchaguzi nchini na kuhakiksha vyama vyote vya siasa vinahakikiwa vyanzo vya0o vya fedha.

Ili zoezi la uchaguzi lipate heshima ni lazima kuwepo tume huru ya uchaguzi ambayo pia itasimamiwa na Bunge kupitia kamati ya siasa.

Katika hali ya sasa ni vigumu sana kupata tume huru ya uchaguzi endapo wabunge wa upinzani hawazidi theluthi mbili ya wabunge.

Idadi kadhaa ya wabunge wakija na hoja na wakazidi theluthiu mbili hiyo huwa ni shida tayari na ni lazima wazo lao lisikilizwe.

Ndo maana mwaka 1993 Marehemu Njelu Kasaka ambae alikuwa mbunge wa jimbo la Lupa huko Chunya akiongoza kundi la wabunge 55 kudai serikali tatu na serikali ya Tanganyika alizimwa na hayati Mwalimu Nyerere kwa kuwa tu ndie alikuwa mlezi wa chama na hoja yake ya kupinga hoja ya serikali tatu ilikuwabaliwa tu kwa kilichoonekana ushawishi wa kisiasa badala ya hali halisi.

Hivyo kwa maoni yangu napendekeza Chadema wajikite katika kujiandaa kuchukua majimbo ambayo yatawasaidia kuongeza idadi ya wabunge kule bungeni ambao wanaweza kuweka hoja yenye nguvu.

Hivi ndivyo chama cha MCP cha Malawi kilivyojipanga kukitoa madarakani chama cha DPP na ikawa hivyo. MCP walihakikisha wanapata wabunge wengi zaidi ili kuweza kuunda serikali na bunge.

Serikali isipuuzie hizi harakati za Chadema maani hii ni mikakati ya muda mrefu katika kuhakikisha nchi inaingia kwenye matatizo endapo matakwa yao hayatatimizwa.

Watanzania tunasifika kwa woga na upole kiasi cha kushindwa kuhioji hata uhandisi jamii unoendelea hivi sasa wa kuhakikisha miradi ya maendeleo inadhurika na isiendelee.

Katika duru za usalama, uhandisi jamii waweza kutafsiriwa kuwa ni kitendo cha kumshawishi mtu kufanya kitendo ambacho kitanufaisha au kutonufaisha maslahi yake.

Mtu au watu hao ni pamoja na matarishi, makatibu muhtasi au mamesenja na maafisa masijala.

Nina imani serikali yetu itakuwa makini na itatumia busara katika kujadiliana na Chadema ambao sasa hivi wamekuja kwa kasi.

Pia sina shaka na mazee na mkuu wao Mabeyo na wanakamati wengi ambao bado wanatatizwa na kinachoendelea.

Mungu ibariki Tanzania.
Ccm maslahi , kindakindaki, limbukeni mna matatizo Sana, Yani CHADEMA kuanzisha vuguvugu la katiba mpya mmechanganyikiwa, why,

Nyie ndo mnaua chama chenu KWA umbea na mapambio yasiyokua na sababu,

Sikia Chadema tunampenda SSH rais, na tumemunga mkono tangu ameingia madarakani Mpaka mkawa mwaona gere nyie

Sasa sie CHADEMA ukitenda haki tutakunga mkono ila sio vinginevyo

CCM mmekua chama Cha kualibu vipaji, mfano SSH rais alingia madarakani na kuanza fanya Mambo KWA ustadi mkubwa , Sasa mmezingira mawazo yake anayaweka pembeni na kuwasikiliza Wana ccm wanataka nini na mbaya zaidi hawasikilizi wanaccm huru, wabomoaji wa nchi hii ni ccm Wala sio mtu Alie juu,

Hata mie nikiingia ccm leo lazima akili Yangu itabadilika , CCM MUNGU ANAWAONA NAWAMBIENI ACHENI HARIBU VIPAJI VYA WATU,mfano tu

Prof kabudi, wasasa na wa kipindi kile wakikutana lazima watoane dam,
Polepole, BASHIRU, only , Mzee Warioba amebaki Kama WARIOBA, Sasa njoo KWA Malchela, Msekwa, n.k mpaka unashangaa
 
Mdude Nyagali na Joshua Nassari ni watu wawili tofauti.

Yes, lakini sio tofauti hiyo unayoisema ww. Kwa hapo ccm ilipofikia inachukua yoyote toka upinzani ili mradi awe maarufu ili kuvutia umma kwao. Ukishakuwa nje ya wakati unafanya lolote kubaki madarakani. Tazama kilichofanyika uchaguzi uliopita, halafu ingia kwenye tovuti ya tume uchaguzi kama kuna matokeo ya uchaguzi ule. Hiyo ndio maana ya chama kupitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom