Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Umesema vizuri kila utawala ulifanya madudu yake sasa mbona haya ya mh Jiwe yakitajwa mnaumia sana?

Wewe unasema alikuwa mwanadamu wa kawaida anayefanya makosa lakini mwenyewe hakujiona kama mtu anayeweza kukosea. Na zaidi alijifanya mtaalam wa kila kitu hata hakusikia la mtu.
Hakuna anaeumia. Tunachouliza ni kwann atajwe na kusakamwa kwa mabaya tu na sio kwa yale mazuri mengi uliyoyafanya!!
 
Habari zenu ndugu zang watanzania mliopo humu. Ndugu zang nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana yanayoendelea nchini, hasa kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoelekezwa kwa aliyekuwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John P Magufuli.

Najua na inajulikana wazi tu kwamba tokea tulipopata uhuru mpaka leo hakuna awamu ambayo haikufanya madudu iwe madogo madogo au makubwa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilifanya mazuri na mabaya pia kwahiyo hili ni jambo la kawaida kwa tawala zote zilizopita kuanzia mwaka 1961 mpk 2020.

Kinachosikitisha ni kuona kila ufisadi au kila jambo baya lililofanyika, au lililofanywa na kiongozi au mtu yoyote aliekuwa katika serikali ya awamu ya tano lawama zote anabebeshwa hayati Magufuli.

Tunafaham kwamb kuna mamb mengi ya kimaendeleo na mazuri lkn watu kadhaa sijui kwa maslahi au faida ya nani wameamua kumchafua.

Na kwa vile mtu akishafariki hawezi kujitetea kwa shutuma zote zinazoelekezwa kwake iwe za kweli au za uongo, sasa sisi tulio hai tutaendelea kumtetea ili kufuta kbs uchafu unaotengenezwa kwa ajili yake.

Najua hata na yeye alikuwa binadamu kwa hiyo kukosea ni jambo la kawaida lkn asibebeshwe makosa na matatizo mengine ambayo hakuyafanya kwa masilahi ya kundi la watu fulani.

Najua kwa sasa wanaomchafua ambao baadhi yao wapo ndani ya CCM na wanaona fahari sana hayati Magufuli kuchafuliwa ili ionekane kwamba yeye na Serikali yake hawajafanya chochote lkn wakumbuke kuwa huyo wanaemsema ameshakwenda zake, sasa kazi kubwa imebaki kwao walio hai.

Mwaka 2025 unakuja wamejipangaje kupangua hoja za wapinzani wa CCM na serikali kwa ujumla kuhusu ufisadi huo unaoongelewa sasa hivi?
Napiga tuuuu.…….
 
Ohoooo !!!
Mungu huwa hadhihakiwi,
Mungu huwa hapendi unafiki,
Mungu anona
Mungu anasikia,
Mungu Ana WIVU,usiabudu Mungu mwingine ila yeye tu.kuna watu walishaanza kuabudu kijimungu mtu.

Mtanzania mmoja anaitwa Kikwete alisema acha KUJIMWAMBAFAI.
Pamoja na kwamba JK Ni walewale na alikua dhaifu dhidi ya wanamtandao, hasa wale mapapa alioshindwa kuwatumbua Rostam,Lowasa na Change,lakini hakua KATILI kama Marehemu Mungu wetu.
 
Back
Top Bottom