Naungana na mtoa hoja kwamba hawa wajinga wachache wanaotia doa uislam kwa vitendo vilivyo nje ya mafundisho ya uislam serikali ni lazima iwaangalie na kuwadhibiti kwani wanakotupeleka ni kwenye vilio na kusaga meno.hali ya chuki za kidini na kisasi ikishamiri ktk jamii yetu ya kitanzania kitachofuata ni mauaji ya kimbari.lakini waislam lazima tujifunze kuishi kwa kuvumiliana na siyo kujifanya mahakimu wa kila jambo ktk hii dunia.tukihukumu sisi mungu atafanya kazi gani?tuache kuwa wa kwanza kuanzisha machafuko ambayo baadae yana-back fire upande wetu tunabaki kulalama kama ilivyotokea huko jamhuri ya afrika ya kati.
Kuhusu kufunga wako watu ambao hawana sifa ya kufunga kama vile wagonjwa,wasafiri,watoto nk,hawa wote lazima wale chakula.lakini pia kufunga saumu pamoja na maana zingine ni kujizuia kula na sio kukataza wengine wanaostahili kula wasile,wataishije sasa?mgonjwa hata kama ni muislam anatakiwa ale ndipo atumie dawa,msafiri hana ndugu anahitaji ale munafunga migahawa!mtoto mdogo anahitaji ale,mwanamke aliye ktk hedhi pia hatakiwi kufunga,sasa kuzuia watu hawa kula kwa kuwapiga na kuwafanyia vurugu hayo siyo mafundisho ya islam.ifike wakati serikari iache siasa katika mambo yanayotishia usalama wa nchi na iwaadhibu wahuni hawa bila huruma.